Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Hivi hawa watu ambao kila mambo yakimchachia Jk huwa anawaokota na kuongea nao ni akina nani?
Mbona hushangilia sana hata kama sio pointi?
Ni kwanini aongee na wazee tu na sio wananchi?
Ni kwa nini iwe Dar es salaam tu?
 
wanampiga kampan mheshimiwa,mkija nyie wakereketwa mtazomea badala ya kushangilia blabla zake!
 
Kila nikiwaza sipati picha halisi ya juu ya kile ambacho kimeitwa''kuongea na wazee wa Dar es Salaam''. Katika hili sina tatizo na kuongea na wazee wa Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza,Shinyanga, Arusha n.k kwa vile ni kama kutakuwa na utaratibu wa wazi na wenye misingi isiyolenga ubaguzi wa aina yoyote. Hakika kwa vyovyote vile kuwaita hawa ni wazee wa Dar es Salaam kama ndiyo njia ya kuwasiliana na watanzania wote ni danganya toto kwani hakuna taswira wala uwakilishi wa taifa. Kama kweli ni taswira ya taifa mbona hata siku moja hatujaona yeye akiongea na wazee wa MIKOA mingine? je, ni kweli huko hakuna wazee wenye umri kama wa wale wa Dar es Salaam? Suala hapa la msingi ni vigezo vipi vinavyotumika kuwapata hawa ''wazee'' make wengine ni mabinti na vijana wenye umri kati ya 25 hadi 30. Nashauri kuwepo vigezo vya wazi ili kutoa wasiwasi juu ya dhana iliyojengeka kuwa ni Wajumbe wa CCM na makada kwani hapo nyuma kulidaiwa kuwa ni wazee wakati wote walikuwa wamevalia KIJANI tupu. Je, kusema kwamba wazee wote wa Dar es salaam ni wafuasi wa CCM? karibu tujadili wana JF
 
vigezo ni km vifuatavyo;
uwe unashinda vijiwe vya kahawa
lazma uvae kibarakashia
lazma uwe chuma ulete
 
uwe mwanachama uliyetukuka wa CCM Na uwe tayari kushangilia kwa kupiga makofi wakati wote.
 
Nimemuona na mzee wa upako mchungaji Anthony Lusekelo nae alikuwepo,nimejiuliza bila kupata jibu. Hivi huyu mchungaji nae ni Mzee? Labda utakuwa uzee wa heshima sio wa umri. Kuna ulazima wa kuambiwa kuhusu vigezo vinavyotumika kuwapata hao wanaoitwa wazee anaokwenda kuongea nao.
 
hao wote ni wale wanaomuunga mkono ktk kuwanyanyasa wataalamu wetu,ni watu wasio na elimu ya kutosha kazi yao ni kupiga makofi tu pumbafu kabisa
 
ni wazeee wa chama cha ccm.........dar es salaam ndo big city kuhusu kuongea na wazeee ni kwamba wazee wana busara sana
 
hawa.wazee ni wale waliotelekezwa na familia zao hawana.ishu choka mbaya wanapewaga msimbaz wanapiga makofi pambav zao
 
Kwa muda mrefu sasa tangu labda hata awamu ya kwanza, nimekuwa nikisikia kuwa Rais ataongea na "WAZEE" wa Dar es salaam. Ikifika siku utaona ukumbi umejaa wakimsikiliza Rais na kuchangilia hasa anapojibu hoja za mbalimbali. Mimi huwa najiuliza
1:Hawa wazee ni wapi? Mbona sijawahi kusikia tangazo linalowaita wazee wa Dar maana pale kwangu nina Mzee wangu na hajawahi kupewa mwaliko. Ndio, MWALIKO, maana Mkuu wa Mkoa wa DSM wakati akitoa ufafanuzu wa kuahirisha mkutano alisema wale waiopata mwaliko waje kwa wingi

2: Sijawahi kusikia wazee wa DSM wamefanya kikao kujadili mstakabali wa nchi na wametoa tamko, au wamemwita Rais kumshauri.

3: Hivi kwingineko mikoani hakuna wazee wa kuongea na Rais?

3. Mbona Rais anatumia mikutano hii kama kujisafisha na kubeza mawazo ya wengine kama juzi alivyobeza wanaharakati.Nikajiuliza mbona hajawahi kufanya mkutano na "Intelectuals" kama Wasomi, wachambuzi, wanaharakati na kuruhusu maswali ili kuliko kusemea "uani" kuhusu wanaharakati ukasemee "sebuleni"

4. Unapozungumza na mtu it's a two way trafic, mbona wazee hawapewi nafasi ya kuchangia? kwa nini kupoteza pesa na muda wa kuandaa mkutano kwa jambo ambalo angehutubia taifa tu.

Kwa mtu ambaye anayeweza kunielimisha niko tayari kujifunza.
 
Hivi hawa watu ambao kila mambo yakimchachia Jk huwa anawaokota na kuongea nao ni akina nani?
Mbona hushangilia sana hata kama sio pointi?
Ni kwanini aongee na wazee tu na sio wananchi?
Ni kwa nini iwe Dar es salaam tu?

Si hilo tu ila huyu mwenyekiti wa wazee alichaguliwa lini kwenye kikao kipi kilichosimamiwa na watu gani na iwekwe bayana majukumu ya wazee hao na vigezo vya kuwatambua maana mimi binafsi ninamiaka 35 ila watu ninaowasimamia kazi wananiita mzee je ni sawa kushiriki? inawezekana kuna ujanja ujanja unaofanywa na baadhi ya viongozi kwa kivuli cha umoja wa wazee maana nchi hii kila mtu akipata nafasi ya kupiga bao anapiga. Wazee hawa ambao hukutana tu diamond baada ya kupewa jero ili kupiga makofi hata pasipohusika ni udhalilishaji wa wazee wetu!!! aina ile ya wazee wengi wao ni wale ambao wamechoka kwa ufukara sio uzee wa umri!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom