Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Mkuu Maggid heshima kwako.

Mambo huenda na kubadilika,
Mwanzoni kabisa kabla ya uhuru kuna wazee kibao walianzisha vuguvugu la kudai uhuru na hata alipokuja kujitokeza Nyerere kama msomi kutoka "bara" wazee hawa walimkaribisha na kumuwezesha kwa kiasi kikubwa hadi uhuru kupatikana

Wakati wa kuunda serikali wazee hawa walikosa sifa za kupewa nafasi za kiungozi na kazi mbali mbali kwasababu ya ukosefu wa elimu na umri wao kuwa mkubwa sana.
Ndipo sasa Nyerere kwa kutambua umuhimu wao akawa ana waenzi kwa kuwaita katika kuongea na ku address issues mbali mbali za kitaifa, na hili alilifanya tu lakini halijaandikwa popote kama ni taratibu rasmi

Hivyo basi kwa enzi hizo wazee wa Dar se salaam, "maalwatan wa mjini" walikuwa wanajulikana na wengi wao walipigana hadi vita ya pili ya Dunia

Nyerere aliendelea nao akifuataiwa na Mwinyi kisha Ben na sasa JK bado anaendelea nao
Ukiangalia kiundani utaona toka enzi ya Mwalimu hadi JK ni wazi wengi sana kama sio wote walio kuwa maalwatan wameisha fariki dunia na waliopo wako hoi taaban kwa uzee

Sasa kwakuwa utaratibu wa kuwaita wazee uliendelea ikapelekea kuanza kuibuka "uzao" mwingine wa wazee kwasababu kadri siku zilivyikuwa zinasonga wazee wenye "original" walikuwa wanazidi kupotea

Hoja yako inaangukia zaidi kwenye hili kundi la wazee wa "uzao mpya" aka wazee wa mjini ambao kimsingi lina utata mkubwa namna linavyojipambanua, binafsi nashindwa kulielezea namna yake

Kuhusu nguo za kijani na njano, wakati ule wa Mwalimu tulikuwa na Chama kimoja kwa hiyo wazee hawa walikuwa ni waanzilishi wa TANU na CCM damu
Baada ya mfumo wa vyama vingi wazee hawa liendelea na u CCM wao wakiwa kwenye matawi ya chama wakipata "kitukidogo" kama wapiga kura za maoni za teuzi mbali mbali kuanzia ngazi za chini za chama,(WANAITWA WAZEE WA FITNA)
Na uzao mpya nao ili kujiahalalishia uzee wa Dar es salaam ikabidi nawao waanze kupita humo humo walipopita wazee original kujipatia uhalali....

Sote tunajua wazee hawa wengi ni hoi bin taaban kiuchumi na serikali kama kawaida yake inapenda kuonekana inafanikisha mambo yake kwa kujaza wahusika ukumbini, kinachofanyika matawi ya chama yanahamasiha wazee kuja kwa minajili ya bahasha za nauli, na wazee hawa wanachangamkia deal kweli kweli kupata "nauli"
 
Ni wale wazee wenye mawazo ya Kale yasiyobadilishwa na chochote. Dunia yao ni Dar es salaam tu. hutafuta habari za watu kwa watu na wakiwa vijiweni huzijadili. hawana busara ya kulea watoto na hupenda kuwatukana tusi la ****ge wee hadharani. Bado wana mawazo ya Chama Kimoja cha Siasa na huwaona wapinzani kama maadui wa nchi na waleta Vurugu. Hupendelea kuvaa Mashati ya Kijani na Baragashia wanapoitwa kuongea na Kiongozi.
 
yawezekana ni ulaji wa kikundi fulani,Hivi huwa kuna posho ya mahudhurio?
 
With our political madness, wazee wa daressalaam mbona wananitia simanzi na majonzi jinsi wanavyoonekana katika siku hizi za karibuni. Hakuna posho za vikao vya uzee wa dar kweli?
 
Ndugu zangu,

TANGU ‘Enzi za Mwalimu', kukiwa na jambo kubwa kitaifa, basi, Mwalimu aliliongea kupitia kwa " Wazee Wa Dar Es Salaam". Na mahali haswa wanapokutana ‘Wazee wa Jiji' kumsikiliza ' Mkuu Wa Kaya' ni pale Upanga kwenye Ukumbi wa Diamond.

Jambo hilo lililoasisiwa na Mwalimu sasa limekuwa ni utamaduni wa kisiasa. Mathalan, ni pale Upanga Diamond Jubilee ndipo Mwalimu alipotangaza vita dhidi ya Idi Amin kupitia Wazee Wa Dar Es Salaam.

Nilipokuwa mtoto pale Ilala, nilitamani sana nikue nije kuwa mtu mzima, kisha niwe mmoja wa ' Wazee wa Dar Es Salaam' ! Ndoto yangu hiyo imefutika! Naam, nimepoteza sifa ya kuwa ' Mzee wa Dar Es Salaam'!

Ndio, sifa ya kwanza ya kuwa ‘Mzee wa Dar Es Salaam' ni lazima uwe na zaidi ya miaka 50, uwe mkazi wa Dar Es Salaam kwa miaka isiyopungua 20 mfululizo! Hilo halijaandikwa popote lakini ‘Wazee' wenyewe wa jiji wanauzingatia utaratibu huo.

Siku za karibuni kuna "Kijana wa Dar es Salaam" kaninong'oneza kuwa wako mbioni kuwashawishi wazee wa jiji waongeze sifa za kuwa mzee wa Darisalama. Kwamba ili uwe Mzee wa Dar Es Salaam ni sharti, ama uwe umezaliwa na kukulia Dar, au umezaliwa nje ya Dar lakini ujana wako wote umeishi Dar. Hivyo basi, unapoteza sifa ya kuwa Mzee wa Dar es Salaam kama umekuja Dar ukubwani! Marekebisho hayo ya taratibu na sifa yakifanyika, huenda hata mie nitakuwa na sifa ya kuwa Mzee wa Dar es Salaam.

Na Wazee wa Dar Es Salaam wana Mwenyekiti wao. Kwa kawaida siku ya ‘shughuli' ya wazee, huvalia kanzu, kibagharashea na kizibau. Ndiye huyu ambaye huwa wa kwanza kumpokea ‘Mkuu wa Kaya' anapoingia ukumbini kuwahutubia wazee.

Ni kwa namna gani basi Mwenyekiti wa Wazee wa Dar Es Salaam anachaguliwa?

Jibu: Hilo ni swali la kizushi na usithubutu kuliuliza mbele ya ‘Wazee wa Dar es Salaam'- watakutoa mbio kwa bakora! Lakini lililo dhahiri ni kuwa, Wazee Wa Dar Es Salaam hawajawahi kuwa na Mwenyekiti mwanamke. Hata Bi. Titi Mohammed hakupata kufikiriwa. Heshima ya kumpa barabara kuitwa kwa jina lake ilitosha, na amshukuru Julius, wanasema Wazee ‘orijino' wa Dar Es Salaam.

Ndio, Mkuu yeyote wa Kaya katika nchi hii atashauriwa aongee mbele ya Wazee wa Dar Es Salaam kama ana kubwa analotaka liwafike wananchi. Ni mara moja katika miaka ya karibuni nimemsikia Rais wa nchi akilihutubia taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dodoma.

Inasemekana jambo hilo liliwashtua baadhi ya Wazee wa wa Dar Es Salaam. Na kuna siku nilitembea kwa miguu mitaa ya Kariakoo Kusini; Livingstone, Mahiwa, Swahili na mingineyo. Hatimaye nikafika kwenye kijiwe cha chai na kahawa pale Mtaa wa Lumumba. Nilianzisha mjadala juu ya Wazee wa Dar Es Salaam. Na hapo nikayasikia manung'uniko.

Ndio, baadhi ya Wazee wa Dar Es Salaam wanaamini kuwa Ilala ndio Dar Es Salaam. Na kwamba ni Wazee wa Ilala ndio waliompokea Julius Nyerere alipoingia mjini. Wanahoji; Iweje Wazee wa ‘mashambani' Kinondoni na Temeke nao waitwe Wazee Wa Dar Es Salaam? Swali linabaki; Wazee Wa Dar Es Salaam ni akina nani?

Maggid Mjengwa,
Iringa,

Hao ni kundi la watu washamba ambao hata shule iliwapita kushoto,a.k.a waliogopa umande,ni mapandikizi ya mafisadi ili kuhalalisha ufisadi na maamuzi ya ajabu ajabu,mind you ndani yake kuna wazazi na ndugu wa karibu wa viongozi waliopewa vyeo vikubwa hapa nchini kwa upendeleo na wenye mamlaka ya kugawa vyeo kwa yeyote anayeweza kuwaunga mkono viongozi wetu wakuu wa dora hata kama wameamua madudu,kwa vifupi ni mamuluki na wabakaji wa demokrasia hapa nchini Tanzania,hiyo ndo picha halisi,wengi wao ni watu wa pale pale pwani na Dar....maneno mengi lakini vitendo kidogoooooooooooo,nadhani unanielewaga nikitanabaishaga namna hiyooooooooooooooooo...................
 
I think dis z outdated and useless tradition to our country top leader! why not addressing direct through media?
 
Unazifahamu condom ambazo zimeshatumika? Nadhani umenielewa vema
 
Nenda kashuhudie mwenyewe ni kina nani siku ya mkutano wao na JK
 
Wana JF naomba nieleweshwe katika hili,Ili kuitwa mzee wa Dar es salaam na niweze kuhudhuria vikao vya JK na wazee niwe na umri gani au sifa gani?, nimeuliza hivi sababu naangalia mkutano wa JK na wazee wa Dar naona kuna wengine ni kina dada au mama wenye wastani wa miaka 40 wamo humu,na akina baba chini ya miaka 50 pia wamo humu.Pia utaratibu wa kuingia mlangoni pale diamond upoje,wanakuangalia usoni na kuamini we ni mzee unastahili?,or wanauliza umri wako?,wanauliza kitambulisho or?, please mnieleweshe ili mkutano ujao niwe wa kwanza kufika ukumbini japo umri wangu ni chini ya 40.
 
Kuwa mzee unatakiwa atleast kuwa na umri wa makamo hivi (60s)
Lakini umri wa kuwa mzee wa darisalama ni mpaka uonekane akili zako zimeanza kuchomoka kichwani
 
Vaa shati la njano/kijani/nyeusi kichwani weka baraghashia au kilemba hapo wewe tayari mzee wa dsm.......unapita
 
Mungi nimekupata,ila sijaelewa vizuri unaposema ili uwe mzee wa DSM lazima akili ziwe zimeanza kuchomoka kichwani?,
 
Kuongezea uwe na sauti ya kushangilia na ujue kupiga makofi
 
Kuwa mzee wa darisalama inatakiwa ukiambiwa kitu hata kama si kizuri upige makofi na kusema ndiyo bwana mkubwa!
 
Inabidi ushangilie pale JK anapolaani wanaharakati waliotaka serikali yake ishughulikie mgomo wa madaktari wakati yeye hakuona umuhimu wa kufanya hivyo
 
Back
Top Bottom