Wazee wa baraza wasema 'Lulu' ameua bila kukusudia, Jaji kutoa hukumu Novemba 13

sasa kama ameua bila kukusudia inakuwaje hukumu inasubiri november 13?
Hukumu inaandikwa kwanza summary na ndiyo inasomwa siku ya hukumu. Hiyo inahitaji muda kidogo kuiandaa. Wakati mwingine unaweza kuambiwa una hatia alafu hukumu siku nyingine
 
Again ,maadam tunaishi kwenye nchi ya kusadikika hata maamuzi yake yatakuwa hivyo,kwa ushahidi gani uliotolewa mahakamani ?hakuna ripoti ya doctor?hakuna foresinc report kuhusiana na kesi hii,hakuna ripoti inayotuambia Kanumba alikufa kwa sababu zipi;na elewa ni muhimu jaji ajiridhie bila shaka kuwa mtuhumiwa aliuwa;ndio tatizo za mahakama zetu nazo kuendeshwa kimihemko.
Katika kesi ya mauaji ni lazima ioneshwe huyu mtu anayedaiwa kuuawa aliuuwa kweli na kifo chake kilitokeaje.

Hatuwezi kila jambo mkuu, mambo mengine yanapita bila kuyasikia au kuyaona. Nina imani ropoti ya Daktari ipo na iliwasilishwa mahakamani
 
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Kama kichwa cha habar kinavyojieleeza hapo

Yule ngul wa sheria kibatala amepanga kukata rufaa haraka na mapema ili kumuokoa mteja wake asipigwe mvua zisizo na idad na jaji lumanyika

Kibatala kayaongea hayo nje ya mahakama alipokuwa akizungumza na waandish wa habar kuhusu kes ya mteja wake

Kibatara kadai hakuna ushahid wa moja kwa moja ambao umemukuta lulu na hatia ya kuuwa sema wazee wa mahakama wametoa mamuz kwa mihemuko


LONDON BABY
Wametoa main I na siyo maamuzi
 
Kihalali hata hicho kifungo cha nje sio haki kwa Lulu, yangekua ni mazingira ya sumu tungeamini kua Lulu alifanya yake lakini sio tukio kama lilivyoripotiwa kutokea. Lulu kwa umri na umbo alilokua nalo kipindi kile ni vigumu kuiaminisha jamii kua anaweza kumua Kanumba kwa kipigo.
Kwani inasemwa aliua kwa kipigo?
 
Kwa haki kabisa , huyo Lulu sijui dhahabu atafungwa tena mvua ya miaka au maisha.

Labda Goli la Mkono lihusike. Kwa sababu, ukiangalia gazeti la Mwananchi toleo la tarehe 23 maelezo ya Lulu hauoni kabisa anavyoweza kutoka kwenye kesi. Maelezo kwa kifupi ya Kesi hii hapa kutoka gazetini.

Lulu asimulia yaliyomsibu nyumbani kwa Kanumba

Tena, Lulu angeelewa mapema hili jambo kuwa siyo rahisi kihivyo, angesema kuwa
"" kanumba alimuita home kwake, akataka kumbaka na hakuwa na mahusiano naye bali bosi wake. Sasa katika kufukuzana ndani ili abakwe ndiyo huyo kanumba akaanguka na kufa maana pia, alikuwa amelewa.


Ila Lulu ameongea mambo yote tena mahakamani ya kumtia hatiani kwa uwazi kabisa.

Kwa kifupi, miaka 30 au maisha hatavikwepa. Lakini, hukumu ikiwa, vinginevyo, basi nitaamini huu usemi uliotapakaa kuwa "" All lawyers are liars""

Kesi ya lulu gazetini.

Lulu asimulia yaliyomsibu nyumbani kwa Kanumba
 
Nadhani sector pekee iliyo bakisha kuonyesha pia imetawaliwa na drama, usanii na ujanja ujanja usio na haki ni hii sector ya sheria.. Kwa kesi hii kama lulu hatofungwa kwa maoni ya wazee wa mahakama, ushahidi wake kukinzana na ukweli wa kesi...naongeleamvua si chini ya miaka 30 jela basi nothing is fair. Tanzania is not fair. Na familia ya kanumba isikubali. Sisemi lulu afungwe bali huo ndio ukweli.
Hakuna ujanja hyo kesi ..
Felony inamfunga ..lulu mwenyewe kajifunga.


Mwaka 2005 marafiki zangu watatu walihukumiwa miaka 25 jela kwa kuuwa bila kukusudia.. Walienda club moja usiku wakiwa watano. Baada ya kunywa vinywaji viwili vitatu waliamua kurudi nyumbani ila walipotoka nje kuna ugomvi ulitokea mmoja wao akauliwa wakakimbia wanne wote kwa kutumia gari la mmoja wao. Na kesi ikawa inazunguka ushahidi kama hii. Mwisho wa siku ikala kwao.
Lulu ukipona washukuru chadema unaotembea nao. Wakijinadi hufungwi. Usipopona usirudie kwenda na foleni za magari mahakamani mchumba. Hujui siasa imekalia wapi. Attitude za watu pia.
 
Again ,maadam tunaishi kwenye nchi ya kusadikika hata maamuzi yake yatakuwa hivyo,kwa ushahidi gani uliotolewa mahakamani ?hakuna ripoti ya doctor?hakuna foresinc report kuhusiana na kesi hii,hakuna ripoti inayotuambia Kanumba alikufa kwa sababu zipi;na elewa ni muhimu jaji ajiridhie bila shaka kuwa mtuhumiwa aliuwa;ndio tatizo za mahakama zetu nazo kuendeshwa kimihemko.


Report ipi unayotaka? Dr aInno Moshi (Pathologist) wa MNH aliitwa Mahakama kuu kufanya nini?
 
Kama unamiliki gari dada unaweza kugonga mtu na ukapatwa na kesi..... Usiongee kwa wepesi kama kunyw maji au kunywa chai na boflo
Kwa nini nigonge mtu. Jamani nilipata leseni yangu baada ya kupitia mafunzo. Tena nina international leseni. Nafata sheria za barabarani. Why nigonge mtu ? Prevention zipo Jamani. Acheni kuishi Kwa nadharia.
 
Kwa nini nigonge mtu. Jamani nilipata leseni yangu baada ya kupitia mafunzo. Tena nina international leseni. Nafata sheria za barabarani. Why nigonge mtu ? Prevention zipo Jamani. Acheni kuishi Kwa nadharia.
Umeona mange amekachamba,,tena kasema wasimchokonoe asijeongea ya marehem seki ,,inaonekana lulu ana kitu sio bure
 
Back
Top Bottom