Wazee wa baraza wasema 'Lulu' ameua bila kukusudia, Jaji kutoa hukumu Novemba 13

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,832
Wazee wa baraza ambao pia ni washauri wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wameeleza kuwa msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' ameua bila kukusudia.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Sam Rumanyika amepanga kutoa hukumu Novemba 13 mwaka huu.

Elizabeth Michael 'Lulu' anakabiliwa na kesi ya mauaji bila kukusudia kwa msanii mwenzake, Stephen Kanumba yaliyotokea April 7, 2012. Jaji anaesikiliza kesi ya Lulu, Sam Rumanyika alisoma ushahidi wa pande zote mbili kisha kusikiliza maoni ya wazee wa baraza.

Katika maoni yao, wazee wa baraza wote watatu wamesema Lulu ameua bila kukusudia, mzee wa kwanza ajulikanaye kama Omary Panzi amesema ni kutokana na ushahidi wa mdogo wake Kanumba, Seth Bosco ambae alielezea ugomvi uliotokea baina ya Lulu na marehemu.

Mzee wa pili, Bi. Sara amesema Kanumba alikufa kutokana na ugomvi ambao shahidi pia kaueleza kulikuwa na giza. Mzee wa tatu, Rajabu Mlawa amesema kutokana na sababu zilizosomwa ameridhika na hakuna ubishi kuwa Lulu ana kosa la kuua bila kukusudia.

 
Wajuzi washeria tupeni muelekeo wa awali wa hukumu hii itakavyoweza kuangukia.
Tayari baraza la wazee wa mahakama limeamua hivi.
4db53f7ce5e149b3b7da30e13681ce98.jpg
 
sasa kama ameua bila kukusudia inakuwaje hukumu inasubiri november 13?
 
Again ,maadam tunaishi kwenye nchi ya kusadikika hata maamuzi yake yatakuwa hivyo,kwa ushahidi gani uliotolewa mahakamani ?hakuna ripoti ya doctor?hakuna foresinc report kuhusiana na kesi hii,hakuna ripoti inayotuambia Kanumba alikufa kwa sababu zipi;na elewa ni muhimu jaji ajiridhie bila shaka kuwa mtuhumiwa aliuwa;ndio tatizo za mahakama zetu nazo kuendeshwa kimihemko.
 
Back
Top Bottom