Wazazi wote piteni hapa (miaka 20 ya maumivu)

Wazazi wote piteni hapa (miaka 20 ya maumivu)

Years ago niliangalia documentary inaitwa My So Called Selfish Life,it's about watu walioamua kuishi KIDS FREE(By choice)..

Wanahojiwa watu(around the world)ambao wameamua kutokua na watoto,

I've learned that Wazazi ndio wanachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu akili ya mtoto,..

older generation has made life so difficult kwa watoto that the next generation has decided to be the last..

GenZ wajanja na elimu hizi nafikiri labda kizazi kijacho kitakua bora zaidi ya hiki..
 
Sisi tukitengana hasira tunahamishia kwa watoto, si baba yako hivi, si mama yako aliondoka, malezi yetu kivyetuvyetu
Unakosea sana,
Unakuwa kama mnyama asiye na utambuzi, watoto ni dhahabu ya kesho
 
Umeelezea vizuri mkuu, deep wounding plus mazingira, mazingira mabaya yakikukuta na deep wounding kuchomoka ni mtihani.
Exactly

Ni kama tu puto na mwiba. Deep winding ni puto na mazingira(au trigger) ni mwiba. Mwiba ukipata puto in kugusa tu mtu anapasuka na kuingia kwenye deep depression na uraibu kama temporary relief.
 
Elevenn mwishon utasema hata wanaume/wanawake Malaya wanaofanya Biashara wamekosa Upendo wa Baba zao.

Wakat Weng tu wanafanya ili kukidhi mahitaji yao na wengne wanatuma hela kutunza Baba na Mama zao + Watoto.

Unahisi ni Trauma ya Kukosa Upendo wa wazazi ndio ikafanya wawe Afisa mtoa Uroda?..
We jamaa una nongwa binafsi sasa. Hujaelewa nini?
 
Watu hawajui tu namna mazingira mabovu yanavyoathiri utotoni, Watu unaoishi na kuzunguka nao mtaani hasa Kipindi cha utotoni ni hatari Sana, mazingira ya nje pia yanaweza kukufanya ukaangukia upande upi, ukiwa na mzazi au wazazi wanaojielewa inaweza kukusaidia Kwa kiasi Fulani lakini siyo mara zote...
Hakika trauma inaweza kuwa event ndogo sana lakini ukikosa guidance inaharibu the rest of your life.
 
Kwa Kuongezea ulichosema,.

parenting hainaga formula,its almost like guesswork.You can give your kids the so called good parenting only for them to end up Vile hukupenda,,

You can also do the vice versa,nimeona watoto waliokulia in a hostile, unhospitable homes but they come out straight as my Big Black D*ck.

Kama Mzazi all you can do is your best and hope mtoto hatakua kichwa maji., Akiwa kichwa Maji its not your fault,you did your part.

Let nature do its part. And I dont think it has anything to do with environment or single parenting(sijasema single mother).

Samuya grew with both parents,Look what he has turned to become,..
Yes, mtoto anaweza pia kuharibiwa na jamii imzungukayo..
Nakubaliana na hoja
 
Ongezea nyama,maana kuna kitabu cha saikolojia nimesoma kuna line inasema Watoto wa kike ambao hawajaishi na Baba zao,wakikua they seek male validation in a wrong way,..nataka nisikie upande wa watoto wa kiume bila Mama,..
The same inakuwa kila mahusiano wanataka partner wao a play uhusika wa mama... Au kwasababu mtu alikosa upendo wa mama basi atamtreat huyo mwanamke na hostility kwa sababu hajawahi kushihudia baba akimtreat vyema mama yake.

Inaweza kuwa tofauti na hayo yote kulingana na how trauma imejijenga kwa muhusika
 
Ndio Maana nikauliza ni Malezi au Upendo.

Mtoto anaweza akapendwa na wazazi wote wawili, wakamsomesha had nje ya nchi. Ila Wakamlea Vibaya (kutomuongoza njia nzuri , nje ya Shule) na mtoto akawa waruwaru.

Kwahiyo mm hoja yangu iko pale pale. Kukosa Upendo wa wazazi hakufanyi ww uje uwe mcheza Porno.

NB:- umesema Wacheza Porno wenyewe ndio wamesema hivyo, ila Hata ukisikiliza Story za Mashoga, % kuwa watasema Wajomba zao ndio wamewafundisha. Kitu ambacho wanatumia kuelezea umma kuwa ni trauma ile ndio inawasumbua.
Kitu ambacho sio kweli, ni formula wanaieleza ili Jamii isikie Huruma.

Wakati Kiukweli % wao wenyewe wanataman kuwa mashoga na walikuwa wanatamani toka zamani.
Mkuu, kama unabishana na watu waliopitia hayo mambo wao wenyewe mimi sina cha kukusaida zaidi ya hapa. Labda ushauri wa mwisho ungepitia utafiti ulifanywa na chuo kikuu cha California kwa miaka 25 ambapo walifuatilia maisha ya watoto waliokuwa familia zenye wazazi wote na watoto waliokuwa na mzazi mmoja,kidogo moyo wako unaweza kufunguka. Ukiamua kubishana hadi na tafiti sasa itakuwa maamuzi yako. Hiyo research ipo online for free unaweza kujisomea
 
Umeongea Vizuri and mtoa maada kuna namna anachanganya Mambo tho ana point,,Hasa akiongelea addiction,.

Mimi nishakua an addict wa madawa kuna Uzi ulikua unazungumzia hayo niliongea the causes and withdrawal...

Tujue kua physical dependence na behavioral problem ni vitu viwili TOFAUTI,..
Addiction ni pana sana mkuu, experience ya mmoja sio lazima iwe experience ya mwingine ila at the end lazima kuna sababu inahusika. Cha muhimu ni kutambua namna ya kuwasaidia wahanga wote kulingana na mahitaji yao.
Pia kama uliwahi kuwa addict wa madawa na ukapona, pokea maua yako, YOU ARE A SUPERHERO. Sio kila mtu anaweza kushinda uraibu maana unakuwa unashindana na maelekezo ya ubongo wako. Hoongeraaa.
 
Aiseeeh umeandika kitu kikubwa na cha umuhimu sana haswa katika jamii hii iliyochanganyikiwa.

Ugomvi wangu mkubwa kwa wazazi ni kwa kuwa wabinafsi wakubwa ambao wanawahitaji au kuwapata watoto si kwasababu wako tayari kulea na kuwa wazazi, bali kwasababu tu selfish kama za kujiridhisha kingono, kupata nafuu ya kimaisha, kupata wa kuwalea uzeeni nk.

Lakini sasa, wahanga wakubwa wanakuwa watoto na matokeo yake tunaanza kuwalaumu hao hao watoto tulioshindwa kuwalea🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Aiseeeh umeandika kitu kikubwa na cha umuhimu sana haswa katika jamii hii iliyochanganyikiwa.

Ugomvi wangu mkubwa kwa wazazi ni kwa kuwa wabinafsi wakubwa ambao wanawahitaji au kuwapata watoto si kwasababu wako tayari kulea na kuwa wazazi, bali kwasababu tu selfish kama za kujiridhisha kingono, kupata nafuu ya kimaisha, kupata wa kuwalea uzeeni nk.

Lakini sasa, wahanga wakubwa wanakuwa watoto na matokeo yake tunaanza kuwalaumu hao hao watoto tulioshindwa kuwalea🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
Hapo kwenye ubinafsi wa wazazi nakazia hoja,tuna utamaduni mbaya hapa kwetu wa kuona kwa sababu umezaliwa basi una wajibu wa kuzaa hata kama hujaandaa mazingira ya kumlea vizuri mtoto. Sio kila mtu anatakiwa kuwa mzazi jamanii,wazazi wa hovyoo wanaleta kizazi cha hovyoo mwisho tunakuwa na nchi ya hovyoo. Tunazaa tu kutimiza idadi ila well being ya hao watoto hatujali. Mtu anabeba mimba ili amnase mwanaume, mwanaume anabebesha mimba ili kumkomesha mwanamke, mwingine anabeba mimba kama kitegauchumi awe anapata pesa za mwanaume, binti mwingine na uchizi wake anaenda kubeba mimba ya mstaafu wa miaka 60 ili ale pensheni.
Pia kuna ambao wanazaa kwa sababu nzuri tu ila hawataki sacrifices zinazohitajika kwa ajili ya kumlinda mtoto. Unakuta baba anakuwa na michepuko live na watoto wanajua na hajali hilo linaumiza watoto kiasi gani, baba mara anakunywa pombe mbele ya watoto,mama anatukana mbele ya watoto. Mwisho wa siku watoto wanaharibika hata kabla ubongo haujakomaa.
 
Strong ladg na Elevenn nawaona wakuu.hongereni sana.

Hivi vitu viko indeep sana ni vile watu huenda wasitake kuelewa kwa sababu huenda wameshatengana na wenza wao teyari.

Lakini suala la malezi watu wanapaswa kujua kabla hawajatupiwa wanajamii wengine linaanza kwa BABA NA MAMA.OutOf kila mtu atajilaumu na kujifariji ujinga maisha yake yote.
Asante mkuu, ninahitahidi kufikisha kwa jamii kile kidogo nachofahamu maana hii topic inaathiri watu wengi ila ni kama mwiko kuiongelea kwahiyo watu wanateseka kimyakimya kumbe ilitakiwa watoke wapate msaada.
 
Asante mkuu, ninahitahidi kufikisha kwa jamii kile kidogo nachofahamu maana hii topic inaathiri watu wengi ila ni kama mwiko kuiongelea kwahiyo watu wanateseka kimyakimya kumbe ilitakiwa watoke wapate msaada.
(realjoke).What if lijinga flani limemwacha baba wa familia kisa muuza duka la simu wa makumbusho,ATAKUELEWA?
 
Hapo kwenye ubinafsi wa wazazi nakazia hoja,tuna utamaduni mbaya hapa kwetu wa kuona kwa sababu umezaliwa basi una wajibu wa kuzaa hata kama hujaandaa mazingira ya kumlea vizuri mtoto. Sio kila mtu anatakiwa kuwa mzazi jamanii,wazazi wa hovyoo wanaleta kizazi cha hovyoo mwisho tunakuwa na nchi ya hovyoo. Tunazaa tu kutimiza idadi ila well being ya hao watoto hatujali. Mtu anabeba mimba ili amnase mwanaume, mwanaume anabebesha mimba ili kumkomesha mwanamke, mwingine anabeba mimba kama kitegauchumi awe anapata pesa za mwanaume, binti mwingine na uchizi wake anaenda kubeba mimba ya mstaafu wa miaka 60 ili ale pensheni.
Pia kuna ambao wanazaa kwa sababu nzuri tu ila hawataki sacrifices zinazohitajika kwa ajili ya kumlinda mtoto. Unakuta baba anakuwa na michepuko live na watoto wanajua na hajali hilo linaumiza watoto kiasi gani, baba mara anakunywa pombe mbele ya watoto,mama anatukana mbele ya watoto. Mwisho wa siku watoto wanaharibika hata kabla ubongo haujakomaa.
Kweli kabisa mkuu, tuna kizazi cha wazazi wa hovyo balaa. Yaani hayo yoote ya kuzalisha ili kukomoa, kujibebesha mimba ili uolewe sijui ili upate unafuu wa kiuchumi ni matokeo ya malezi mabovu tunayowapa watoto wetu.

Matokeo yake watoto wanajilea, wanalelewa na watu baki kama house helps au ndio tuwatelekeze boarding schools tangu wakiwa chekechea🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Kiufupi mwanamke usimchoke mumeo kwa sababu huyo ndio mzigo wako na mwanaume mwenzangu iwe vivyohivyo pia…
Ikiwa mmoja kati yenu ninyi wawili mmepishana katikati ya familia,kubarimi kuwa wote mmekosea then tengenezeni kama watoto ndio majudge wa kesi zenu.(hawapaswi kujua chanzo cha ugomvi wenu la hasha).Kunanamna ya kumshtakia mwenza wako kwa watoto bila kuwaambia A-Z na wakaelewa tatizo ni nini na wanajua ni jinsi gani ya kusolve…otherwise mtaua futures zenu na za watoto kwa mambo ya kijingajinga
 
(realjoke).What if lijinga flani limemwacha baba wa familia kisa muuza duka la simu wa makumbusho,ATAKUELEWA?
Hapo ndo kuna member mmoja kasema ubinafsi. Wewe ukiamua kuwa mzazi ,ujue maamuzi yako yote yajayo yanatakiwa kwanza kuzingatia ustawi wa watoto wako. Kuwanyima watoto haki ya kuwa na mzazi wao kwa tamaa zako mwenyewe ndo kutengeneza wahanga tunaowaongelea hapa.Kuna msemo wa kiingereza unasema " zawadi kubwa zaidi unayoweza kuwapa watoto wako, ni kumpenda mwenzi wako". Watoto kabla ya chochote wanahitaji wazazi wanaioshi pamoja kwa upendo ( kama wote wapo hai) hayo mengine ni ziada. Kama hitaji hili muhimu likikosekana, hata uwape nini haiwezi kuwa mbadala wake.
 
Juzi kati baada ya kusoma bandiko la mlevi min -me la kuhusu bintiye na kukosa upendo kwa mama yake, ambaye Wali kuwa separated na kumfanya min kuwa single father, so mtoto kukosa motherly presence ila fanya amchukie..

actually, ile issue ilinifanya nijione ndani yake.

Why..?

Kwa sababu scenario hiyo ilinifanya nibebe maumivu kwa takriban miaka 20, ya maumivu, na kuanza kuona kuwa ili stem from family issues..

Sitaki kueleza stori yangu, because Nitakuwa nafanya repetition na ni ndefu sana.. Ila ukweli useme ya kuwa...

Zawadi pekee na bora utakayo mpa mtoto wako ni kumfanya ajihisi anatosha, anapendwa, anaweza, na ana deserve kile anataka kutimiza... Ili mradi kiwe na manufaa both kwake na jamii inayo mzunguka.

Binadamu yuko so hardwired kwa ajili ya connection(ukaribu na watu au jamii imzungukayo)... Ila hii huwa inakaziwa sana akiwa bado yu mtoto. Yaani mwaka wa kwanza hadi wa 7.. Na Aristotle alishawahi kuliweka wazi hilo...
View attachment 3646873

Ila bado hiyo sio kigezo mtoto yaani akiwa under 18 bado hajapevuka both psychological and emotional...

Ngoja niwape siri wazazi, wengi hupenda kudhani kuwa trauma and depression inatokea pale unapo mwdhibu mtoto au kumnyima mahitaji, la hasha.. Mtoto huumia zaidi pale Atakapo achwa kusikiliza, atapo nyimwa uhuru, atakapo fanyiwa kujiona hafai...

Ubaya ni kuwa mtu akiumizwa na trauma, ku reverse au kupona juea ni almost impossible... Maana ile crack inaenda deep na inaficha na shade aspect...

Unashangaa mtoto ana zamia madawa ya kule ya, ushoga, umalaya, kuvuta ganja, anakuwa mtu mwenye hasira, aside shaurika.... Inshort ni kuwa hii demage hata yeye mwenyewe hawezi kuitrack... Na ata akijaribu huwa anaishia kupata maumivu kwa sababu reality ya ndani inakuwa tayari imesha kuwa ngumu kubadilika.

Binafsi niliingia katika uraibu mbaya sana wa porno graphics... Mimi ni soo sensitive person, na as I said before malezi kidogo ilikuwa changamoto. Sikupata ile fatherly love ya kunikanya vyema, soo nikawa soo reserved, badala ya kufuata stimu za nje kama pombe(japo nilijaribu ila sikuipenda), wala kufatilia mademu(nilitokea kuwachukia kwa sababu ya kuishi na step mother.. Alinifanya niwachukie wanawake).. So basically nilikuwa exposed kingono at a very young age. Kufupisha stori kwa sababu ya hate na insecurity nilokuwa nayo kwa wanawake sikupendelea sana kuwa kwenye mahusiano. Niliingiwa kwenye uraibu wa sheria mkononi. Na kwa kuwa huwa nina sensitivity kubwa haikuwa shida kwangu kufika climax.

Na hiyo ni just one aspect ya madhara ya childhood wounds.. Ila nikianza kueleza how deep this rabbit hole goes. Itabidi niweke iwe series.. Ila ni kuwa matokeo ya maumivu ya utotoni hubadilisha world view ya mtoto akuwapo mtu mzima. Na tena hawezi kutambua maana inaingia kwenye operating system yake, anaishi na kuona dunia kupitia lens ya hayo maumivu.

Wazazi mlio na watoto wadogo, nawaomba sana mzingatie kidogo nilicho andika... Muhimu ni kuwa mtoto akiwa na shida hasa ya mahusiano na nyie kama wazazi angalieni na mtoe msaada wa kihisia mapema iwezekanavyo, wakubwa mtoto alisha pita umri wa labda miaka 15 hvi huwa ni kama haiwezekani tena kurudi.

Kuna hii tabia ya wazazi kuwafanya watoto wabebe msalaba yao, yaani just because alipitia maisha flani, basi anasambza hiyo trauma kwa wanawe ili nao wawasambazie watoto wao.

Tuache huu ujinga, ni waambie tu ya kuwa ukifanya upendo na kutosambaza hiyo trauma uliyo nayo... Kwa kiasi kikubwa Uta heal pia japo itakuwa soo gradual ila utaona mabadiliko pia.

Mimi sio mtaalamu wa kisaikolojia ila hata hii industry kwa huku kwetu imekaa kiupigaji tu, hawajui chochote ila kumezeshwa tu vitu visivyo akisi uhalisia. Wazazi ndo mnajua watoto wenu vizuri, jitahidini kuwa mwanga kwa kizazi kijacho, acheni kufanya vitu kwa mihemko na kukua ego zenu. Ni ujinga na ushamba, which mtoto wako akikuwa atakuchukia na utakufa vibaya tu

Mabadiliko ya naanza na wewe mwenyewe sio mzazi tu hata wewe dada, kaka, mjomba, shangazi... Do good to these innocent souls...

Nawishi huu ujumbe ueleweke watu wasirudie nilicho pitia kwa miaka 20.

In peace and light..

de Gunner

binti kiziwi Tsh Mshana Jr mshamba_hachekwi ShesRise_1 Binti wa zamani Me and me Yoda Joanah
pole mdau!
few questions,
so sasa umesharecover? una girl friend? au mke?
any impact unaiyoiona kwa kujichukulia sheria mikononi?
 
Kiufupi mwanamke usimchoke mumeo kwa sababu huyo ndio mzigo wako na mwanaume mwenzangu iwe vivyohivyo pia…
Ikiwa mmoja kati yenu ninyi wawili mmepishana katikati ya familia,kubarimi kuwa wote mmekosea then tengenezeni kama watoto ndio majudge wa kesi zenu.(hawapaswi kujua chanzo cha ugomvi wenu la hasha).Kunanamna ya kumshtakia mwenza wako kwa watoto bila kuwaambia A-Z na wakaelewa tatizo ni nini na wanajua ni jinsi gani ya kusolve…otherwise mtaua futures zenu na za watoto kwa mambo ya kijingajinga
Na wewe mume usifikie stage ya kuchokwa na mkeo, timiza wajibu wako ipasavyo na usiumize hisia zake. Vivyo hivyo kwa mke, asiumize hisia za mwenzie, mambo yakiwa magumu ongeeni, pigeni magoti pamoja ,muombeni Mwenyezi awape hekima ya kuyatatua kwa upendo.
Changamoto kwenye mahusiano hazikosekani, ila kama wote mna nia njema na ndoa yenu,hakuna atakaemchoka mwenzie mkuu.
 
Back
Top Bottom