Sio wote mkuu, wacheza pornography wapo ambao wamechukuliwa kama watumwa kupitia biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu,na kuna wale wanaofanya kwa hiari. Hao wanaofanya kwa hiari wote wana majeraha ya utotoni mfano kuna waliobakwa wakiwa watoto, kuna waliolawitiwa na kundi kubwa ni waliokua kwenye malezi ya mzazi mmoja,na sio kwamba eti walikua na maisha magumu wamekosa ajira ndo wakaingia humo.
Halafu mkuu usijilinganishe wewe na wengine, wewe huko kwa bibi yako pornography ilikuwa inapatikana kiganjani? Most likely hukuwa exposed to pornography so huwezi kutamani.
Hao naoengelea ni kwamba wanakuwa exposed to porn,kwa watoto wengine wanaangalia out of curiosity na kuacha, ila wao mioyo yao inavutiwa zaidi na hizo video kutokana na kwamba kisaikolojia hawapo kawaida ndio maana wanakuwa waraibu.
Hata hapa kwetu ni vile porno sio biashara halali, ingekuwa halali wangeenda wengi tu kuigiza hizo movie, mfano mzuri ni Gigy Money. Gigy amekua kwenye mazingira ya ovyo na hakupata upendo wa baba toka akiwa mdogo. Kukosekana kwa upendo wa wazazi jumlisha mazingira aliyokulia ndio sababu Gigy Money kawa vile alivyo. Kuna ambao wanakosa upendo wa wazazi lakini hawakutani na mazingira mabaya( mfano wewe) ila kwa wanaokutana na mazingira mabaya kuchomoka ni ngumu.