Wazazi Wanaolalamika Wamefeli?

Wazazi Wanaolalamika Wamefeli?

Siku moja binti yangu wa pili aliniomba pesa, nikampa kidogo, akalalamika, nikamuonyesha bill nilizonazo! Alichoniambia sijakisahau mpaka leo!!!
" Aliniambia, Baba hayo ni majukumu yako, pambana", Kweli nikaongeza bidii ya kupambana.
Alikueleza ukweli kwamba hizo bills hazihusiani na pesa anayokuomba ni majukumu yako ya lazima usitafute kisingizio na huruma upambane 😁😁😁
 
Kujuta kunatokea pale ambapo alijitoa sana KWAAJILI yako halafu umekuwa unamuonesha dharau

Kwa mfano wewe umesema ushawahi kuzinguana na dingi wako so dingi IKABIDI akukumbushe hata wema aliokutendea ili urudi kwenye mstari Ila bro ukakaza

Sasa hapo atachaje kujuta ikiwa hela ya ada aliyotumia kukusomesha wewe kuna wengine kipindi hiko hiko walitumia kulia gambe na kutekeleza watoto wao
Una uhakika kwamba nilimletea dharau au ndo Ile misemo yenu kwamba mzazi hakosei?
 
Umekosa hekima.

Wazazi ni watu wa kuwaheshimu, achilia mbali pesa walizotumia, haujui ni mara ngapi hawakulala usingizi kwasababu yako.

Tafuta hela wewe binti, ungekua na ukwasi usingekuwa na muda wa kujibishana na wazazi mambo basic kama hayo
 
Huko tunakoenda kitaibuka kizazi korofi Sana ambacho mtu kabla hajazaa impasa afikirie mara tatutatu
Exactly, kwa Sasa watu wanazaa kama panya alafu Wana misemo Yao ya kujifariji kwamba kila mtoto anakuja na riziki yakee
 
Kama wazazi wako huwa wanalalamika kuwa walijinyima sana kwa ajili yenu, basi umezaliwa na wazazi waliofeli vibaya sana. Watu hawapendi ukweli, yaani kuwaza tu hivyo wanaona tayari wanapata laana. Mtu anajinyimaje kugharamia matokeo ya furaha na starehe zake.

Watoto ni matokeo ya starehe zako, hakuna mtoto yoyote aliyeomba umzae. Halafu unakaa kabisa kumuambia mtoto eti niliuza shamba usome.

Wee shenzi nini🤣 Uza chochote aisee si ulitaka mwenyewe. Ungetuliza 'genye' unadhani huyo angekuwepo? Na wewe unahaha kwa mikopo kama mwehu kusomesha utitiri wa wadogo zako kisa eti mzazi alijinyima kwa ajili yako. Ulitaka nani ajinyime kwa ajili yako.

Watoto siyo biashara wala bima ya maisha, tunazaa tu kufurahia na siyo kuwafanya pensheni ya uzeeni. Achana na huu mtazamo uliosababisha turithishane umaskini kwenye jamii nyingi.
Kuna watu wamezaa kwa peer pressure ukiwauliza kwa nini umezaa mtoto hawawezi kukupa jibu ka kueleweka, usifanye kama watu wetu huko huwa wanafikiria sana kabla ya kuzaa.

Wangefikiria sana pengine hata wewe usingekuwapo hapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom