Wazazi walalamika Wanafunzi wa shule tatu za Msingi kusomea chini ya miti Kigoma

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
MSAADA.jpg
Wanafunzi wa Shule za Msingi Muungano, Mvugwe na Kasasa katika Kata ya Makere, Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, wanalazimika kusoma wakiwa wamekaa chini ya miti na wakati mwingine kwenye sakafu kwa kile kinachoelezwa na wazazi wao na viongozi kuwa wamekosa madawati ya kutosha.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wazazi wakati Shirika la World Vision Tanzania kupitia mradi wa Buhoma likitoa madawati 150 katika shule hizo ili kusaidia kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunza na kukuza taaluma kwa wanafunzi.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Kigoma Mkama Nangu, amesema wataendelea kuunga juhudi za Serikali katika kusaidia watoto, ikiwemo masuala ya elimu na afya na kwamba katika bajeti ijayo wamejipanga kutoa madawati zaidi ya 700.

Awali, akipokea madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanal Izack Mwakisu ameagiza madawati hayo kuleta mabadiliko katika taaluma na kuhakikisha yanatunzwa ili kuhudumia Wanafunzi kwa kipindi kirefu na kuwasihi wadau wengine kuwekeza maendeleo kwa jamii ya wahitaji.

Chanzo: EATV
 
Huko tozo hazijawatembelea? maana ngonjera iliyopo ni kwamba tozo zinajenga madarasa...
 
Back
Top Bottom