Wazazi inakuaje mwanafunzi anapata mimba?

Raynavero

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
38,413
55,987
Salaam members...!!
Naomba kuuliza wazazi na walezi wenzangu, hv inakuaje au inawezekanaje mtoto wako akapata mimba halafu ni mwanafunzi wa shule ya msingi au secondary halafu mpk inafikia miezi saba hujui?

Hv kweli tuko serious na malezi ya hawa watoto?!!!
Hv hata mabadiliko ya mwili huyajui we mzazi?!!Au ndo ubusy na uzungu tunaoiga tunawapa sana uhuru hawa watoto?!!

Hv hatujui kua kufeli kwa mtoto na wewe mzazi umefeli?!!
Mtoto anapopata mimba failure wa kwanza ni wewe mzazi...ukubali, ukatae...

Anashindwaje bint kumaliza form four kwa sababu ya mimba?!!
Siongelei wa kubakwa hapa tafadhali
Unahis ataweza kumkanya mwanawe baadae asome kama yeye miaka minne kukituliza alishindwa?!!

Kuna tofauti kubwa kati:
Kumaliza shule
Kufaulu shule
Kupata mimba shuleni.
Huyu wa mimba ni failure yumkini baadae anaweza kua na good life kuzid wote hapo Juu ila bado jinamiz la mimba analo.

Ndugu zangu sisi ni waafrica tuzingatie maadili yetu na mila zetu zinavyotaka mimba za utoton zinaumiza sana
Unalea mwana na mjukuu!!!

Niwaombe radhi wote waliopata mimba shuleni au wenye watoto wenye hizo hali!
Lengo tuelimishane na kujifunza!!!

My own brand!!
 
jinsi mtoto kupata mimba maana alifanya mapenzi na mshenzi mwenzie, tena wengi wanaopata mimba ujue huo mchezo kauanza muda tuu...yaani hapo watu washabrashi hadi imekuwa na uwezo na kupenya hadi kazoea na hadi kaamua kufanya ngono zembe....huyo mkubwa..
 
Ni kweli mtoto kupata mimba asilimia kubwa wazazi tulaumiwe.

Ila gen hawa unaosema wanaiga uzungu watoto wao hawapati mimba kiurahisi. Wanaopata ni wale wa maisha ya chini ambao wengi wao hata uzungu hawaujui.

Amini leo Tanzania kuna mzazi hajui mwanae analala wapi. Kuna mzazi hajui ratiba ya mwanae ndani ya siku na akirudi nyumbani ni sawa na asiporudi ni sawa kwake.
 
Hahaha...!mpk imepenya

Usemayo ni kweli ila hawa wanaiga wapi malezi hayo ya hovyo?!!!
Kuna wazazi wana mambo ya ajabu mpk shetani anawashangaa!!! Yaani huku uswahilin hali ni mbaya kabisa mama analala nje mtoto analeta bwana ndani

My own brand!!
 
Mwanafunzi kupata mimba inatokana na malezi kwa asilimia kubwa,sikuhizi wazazi wamekosa muda wa kuwahimiza watoto waende kwenye nyumba za ibada,huko kungesaidia watoto hata kua na hofu ya Mungu na kujua zinaa ni dhambi.Pia uhuru wa kijinga unaotolewa na wazazi unakuta saivi mwanafunz wa form one ana smartphone, kutwa kucha kuperuzi ujinga na mzazi hata hana mda wa kukagua simu.Watoto weekend wanaenda picnic za ajabu mzazi hana hata mda wa kufuatilia.Je unadhani huyo mwanafunzi na hayo mazingira hatarishi anayopitia ataacha kubeba mimba. Jamii iamke kwenye malezi bora ya watoto mimba zitapungua na kuisha kabisa.
 
Hizo simu ndo shida siku hz ni kama fashion wazazi kuwannulia watoto wa!!!! Na ht km hajamnunulia ht akimuona nayo hamuulizi!!!!!

My own brand!!
 
Hizo cases zipo kwa asilimia ngapi?

Isije ikawa umeandika kwa kuchukulia mfano mmoja pekee
 
Ni kweli mtoto kupata mimba asilimia kubwa wazazi tulaumiwe.

Ila gen hawa unaosema wanaiga uzungu watoto wao hawapati mimba kiurahisi. Wanaopata ni wale wa maisha ya chini ambao wengi wao hata uzungu hawaujui.

Amini leo Tanzania kuna mzazi hajui mwanae analala wapi. Kuna mzazi hajui ratiba ya mwanae ndani ya siku na akirudi nyumbani ni sawa na asiporudi ni sawa kwake.
Hata maisha safi wanapata mimba, tena sana tu. Wengi wao wakipata mimba wazazi wanafanya haraka kuzitoa as wapo na "exposure", mtoto anapelekwa Marie Stopes shaaap anapewa ile tablet maarufu mzazi anaomba two days off, baada ya hapo mtoto anarudi shule bila wasi.
 
Oouh,
Wengi huitumia saana hiyo njia ila utashangaa hapa ukiitaja hupati like hata moja
 
Back
Top Bottom