Ni kama kuvunja miiko ila hakuna namna, Wazazi tutumie mbinu zipi kuwaelimisha watoto kuhusu mapenzi kuwalinda na kizazi hiki

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Kwakweli kwa tamaduni zetu hili suala limekuwa likifumbiwa macho na la kukwepa, ila angalau zamani tunapobalehe wavulana tulienda jandoni na dada zetu walienda kufundwa unyango, kwa sasa wavulana na wasichana wanakuzwa peku peku bila hizi elimu muhimu, ni jambo hatari sana.

Binafsi nakumbuka nina wazazi wote wameelimika na walikuwa watumishi serikalini lakini huwezi amini ni mara moja tu nikiwa nimemaliza likizo narudi shuleni form 3, mzazi moja ndio aliniambia kaa mbali na wasichana, yani ndio hivyo tu. hatukuwahi kukaa hata kwa dakika 5 tu anipe elimu.

sizungumziii elimu ya kwamba mzazi kumpa gazeti mtoto wake akajisomee ama amwambie aende semina ya vijana wadogo LA HASHA !! Hapa elimu nayozungumzia ni ile mlezi na mtoto wake wanakaa meza moja, mzazi anampa mwanae a,b,c,d kuhusu S*x, ni kwasababu maneno kutoka kinywa cha mlezi ndio huwa yana nguvu zaidi.

Tukija kwa kizazi cha sasa hali imekuwa mbaya,

watoto wetu wanatembea na smartphones zilizojaa mambo ya S*x
Miziki inachochea sana nyimbo za S*x
Mavazi yanahamasisha sana S*x

Kiufupi hali sio kama zamani tena,

mambo yamebadilika sana, Mzazi ukikaa kimya mwanao anaweza kuteleza na kuangukia raha za muda mfupi na kujutia muda mrefu.

Binafsi nimeona mtoto wa kiume mwenye miaka 14

  • Kashaanza kuota ndoto nyevu (ndoto za sex kwa kijana anaebalehe),
  • Kaanza mazoea na binti wa mtaani mwenye miaka 18
  • Simu yake huwa anasechi mambo ya ngono, ninajua kwasababu account yake ya google ninayo inaonyesha historia ya kila kitu.
  • Nina wasi wasi kashaanza kukwea mnazi (p*ny*to)

Hapa najua tayari gari limewaka na anatamani sana kus*x, mimi kama mzazi nitajilaumu sana nikisikia kapata magonjwa, kapachika mimba, n.k. nataka nichukue tahadhari mapema ila nahitaji mwanga wenu zaidi.

Ni njia zipi tunazoweza kuwaelimisha watoto wetu haya mambo iwe tahadhari ya mapema kabla ya kujutia ?
 
Ninadhani kunapaswa kuwa na kipindi maalum cha malezi na maadili ndani ya vile vipindi vya dini vya shule. Wakimaliza kusoma bible na Quran, basi wale viongozi wao wanapaswa kichomekea na hilo la mahusiano katika umri mdogo.
 
Hapo ni kwenda nao direct tu. Hakuna kingine zaidi ya kuwaelimisha na mimi kwenye hili suala sitakua mzembe kwa wanangu.

Mama angu alikua muuguzi kwenye hospital ya mkoa kwa hiyo kuna siku akanambia njoo hospital nikaenda akaninunulia msosi na soda ulipofika muda wa kuondoka kuna kiji magazine akanipa akasema naomba niwekee nitachukua wiki ijayo.

Nikaweka kwenye begi nikaondoka sasa nilipofika home nikaanza kukipekua ndio nakutana na elimu mule namna ya kujikinga, sijui namna ya kujizuia na hisia ilifika mpaka wameelekeza namna nzuri na sahihi ya kuvaa condom. Yan kilikua na mambo mengi ya kuelimisha na toka hapo nikaanza kushare na wenzangu wasome. Mind you hapo nilikua darasa la saba.

Sasa kwa hali ilivyo sahivi na huu utawandazi nahisi kama watoto wanawahishwa kujua mambo mengi kwa haraka sana kitu ambacho ni very dangerous kama tusipochukua hatua za haraka kama wazazi na walezi.
 
Umeandika neno sex kwa kificho inaonesha jinsi ulivyo na maadili mema. Hongera sana.
jandoni tulifunzwa kuongea kwenye hadhara kwamba hawapo vijana tu, inabidi uzungumze ukitilia maanani bali kuna watoto wadogo wanaoweza kuwa wadogo zako na watu wazima... nashangaa vijana wa sasa hata huko kwenye groups wanavyoongea utadhani kuna vijana tu.
 
Huwezi labda mkakae Lindi ndani ndani kule mtaa nnaokaa, watoto wadogo chini ya miaka 17 washaanza unga vikojoleo(wengi wakiwa sec)

ilihali mie nilianza sex nna miaka 26

sehem niliyopo hakuna binti 18+ asiye na mtoto, na wote ni singo maza
 
aisee haiwezekani kabisa,

utamfungia huko kote akifika chuo anakua huru

kupona chuo ni ngumu sana
Ndivyo tulivyoumbwa lakini mzazi ukimhusia mtoto wako mapema, maneno yako huwa yana uzito sana kuliko kumuacha tu, elimu unayompa walau kidogo inampa muongozo katika huo uhuru ataoukuta.

Na tena hawa wanaocharuka sana vyuoni mara nyingi ndio hawa ambao hawapewi elimu na walezi wao, wao wanachoambiwa wasome tu lakini huko kwenye mambo ya s*x ni weupe.
 
Usiruhusu mtoto kuwa na simu
Kwa vijana wa sasa ni ngumu sana, zaidi zaidi utamfundisha awe mbobezi wa kuificha na hutajua hata anachofanya kwenye simu.

Mimi nimeona nisande tu nikampa simu ila sijatoka mtupu, naweza kuona ni vitu gani anafanya kwenye simu.
 
Huwezi labda mkakae Lindi ndani ndani kule mtaa nnaokaa, watoto wadogo chini ya miaka 17 washaanza unga vikojoleo(wengi wakiwa sec)

ilihali mie nilianza sex nna miaka 26

sehem niliyopo hakuna binti 18+ asiye na mtoto, na wote ni singo maza
 
Bora huyo wako watakuambia ni rijali, kwa kua anazoeana na mdada, je ungekuta anawasiliana na mwanaume mwenzake mambo ya sex?
 
Ile club ya fema vip ? Wale jamaa enzi zetu tangu msingi wanakuja kutoa elimu na yale majarida yao yale ..

Kuna moja linaonyesha madhara ya magonjwa ya "pangusa" ukiona watu walivyo huwezi kufanya michezo...Ila sasa sijui imekuwaje .
 
Back
Top Bottom