Upi utaratibu mzuri wa kufuata ili kulinda haki ya mtoto anayetuhumiwa kushibisha mimba mwanafunzi?

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
861
1,384
Namaanisha mwanafunzi wa kiume mwenye umri wa miaka 14
Ni kidato Cha pili!

Mwanafunzi huyu anatuhumiwa kumpa mimba Mwanafunzi wa kike kidato Cha kwanza miaka 13 ya umri

Mwelekeo ni kwamba wote wanapaswa kufukuzwa shule! Naam wamefukuzwa leo!!

Hoja yangu Ni kwamba Ni ushahidi gani uwe wa msingi kuzingatiwa ili kumfukuza shule mtoto wa kiume?

Hoja yangu umejikita kiumeni kwa kuwa upande wa kike Kuna ushahidi wa vipimo vya mimba

Kwa mhusika huyu ninayomzungumzia anatiwa hatiani na kufukuzwa shule kwa kutajwa kwake na msichana mjamzito, pia walihojiwa baadhi ya wanafunzi wa karibu wa msichana na mvulana (wenye kesi) na baadhi yao walikiri kuwepo uhusiano wa mapenzi baina yao (wenye kesi)

Hawa wote ni wanafunzi wa shule moja ya kata!

Je, ushahidi umetosha kumuondoa mwanafunzi wa kiume shuleni?

Nipeni fikra zenu please!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nuwafunde watoto wenu kuhimili,kuheshimu,kuogopa na kusubiri muda stahili wa kufanya mapenzi/ngono.Saa hizi tunachoshana tu.
Hongera kwako uliomaliza kuwafunda wanao!
Ila usisahau kuwaruhusu kutoka nje ya geti. Kwani Hii dunia ni yetu sote tuivinjari

Haina maana ya kujisifu kuwa umewafunda halafu kutwa umewafungia getini, unawapeleka na kuwarudisha shule kwa gari, shule unazowapeleka Ni za board zenye ulinzi mkali

Halafu unajigamba umewafunda watoto wamefundika!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hongera kwako uliomaliza kuwafunda wanao!
Ila usisahau kuwaruhusu kutoka nje ya geti. Hii dunia yetu sote tuivinjari

Haina maana ya kujisifu kuwa umewafunda halafu kutwa umewafungia getini, unawapeleka na kuwarudisha shule kwa gari, shule unazowapeleka Ni za board zenye ulinzi mkali

Halafu unigamba umewafunda watoto wamefundika!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Siyo suala la kushindana.Funda watoto waelewe na waweke vichwani mwao. Ngono utotoni huleta hasara zaidi kuliko furaha ya dakika mbili.Mtoto wako amefikisha miaka 14 na amemtia binti mimba. Subiri tuone tafsiri ya sheria kama itambeba au atakuwa ni mtoto mtukutu.
 
Sijaleta hoja ya vipi Sheria inambeba au la!

Dogo hayupo mahakamani na haendi mahakamani,
Hoja ya msingi kujua Kama ushahidi uliotumiwa na shule kumfukuza umetosha au la?
Nikukumbushe kuwa malezi ya mtoto yapo kwa jamii kwa asilimia kubwa, na sio kwa mzazi
Jamii iliyoharibika Kama hii inahitaji majaliwa ya Mungu ili mwanao anusurike,
Usijidanganye kuwa mzazi ana nguvu za kutosha za kumfunda mtoto akafundika!

Hio ndio sababu watoto wako umewafungia getini,. Umejua nguvu yako ya kufunda haitoshi chochote, hivyo umeomba nguvu ya geti lako,

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hizi ni sheria za kikoloni ndizo zilizotumika kuamua kesi hii,mtoto wa kiume na wa kike wote wangeendelea na masomo kama kawaida,mwenye mimba angeruhusiwa kujifungua na kurudi shuleni,elimu ya uzazi ndio njia ya kufuata,condoms,injections etc etc viruhusiwe ili kuzuia hizi mimba zisizopangwa
 
Ndugu mzazi mwenzangu,

Kuna msemo usemao, tulipotambua ya kuwa amani ni bora kuliko ushindi, tuliwaacha washinde ili tubaki na amani.

Kwenye swala kama hilo, hakuna uthibitisho wa moja kwa moja. Ila taarifa za mwanafunzi wa kike kumtaja aliyemtia mimba, naye kuridhia kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana husika basi hiyo ni hatua ya mwanzo.

Hata kama hakumtia mimba kama unavyotaka ushahidi kamilifu, lakini kuwa na mahusiano ya kimapenzi ni kosa. Na adhabu yake ni kufukuzwa shule.

Basi kama una ualakini wa adhabu aliyopewa kwa sababu ya kumtia mwenzake mimba basi kosa la kuwa na mahusiano na mwanafunzi mwenzake linaadhibiwa kwa adhabu hiyo hiyo ya kufukuzwa shule. .

Ridhia kwamba mwanafunzi kakosea, kaa naye mfunze. Kumkingia kifua kutaka kuwapo na uthibitisho kamili ni kumtia kiburi na kujiona hajakosea.

Cha kufanya tafuta shule nyingine na umhamishie mwanao. Achana na kutaka kudinda kuwa hakustahili kufukuzwa.

Hata mtu baki akituhumiwa na mwanafunzi kuwa ndiye aliyemtia mimba basi hakunaga ushahidi mwingine, bali kushikiliwa na uchunguzi huanza. Na pengine wanahukumiwa bila uthibitisho wa DNA za mtoto atakayezaliwa.
 
Hakuna kuwachukulia hatua. Wote ni watoto, serikali ikapambane na mambo yanayochochea ngono kama vile videos za siku hizi pamoja na kublock sites za porno, ukizingatia kuwa umri wao hapo walipofikia ni foolish age na huwa unachochea sana kutizama porno. Nadhani hii itakuwa na tija zaidikuliko kuwafukuza shule.

Waendelee na masomo, na mtoto wa kike mimba ikishakuwa kubwa apewe nafasi ya kwenda kujifungua na baadae kuruhusiwa kurudi kuendelea na masomo, hakuna jinsi, yameshatokea.
 
Sijaleta hoja ya vipi Sheria inambeba au la!

Dogo hayupo mahakamani na haendi mahakamani,
Hoja ya msingi kujua Kama ushahidi uliotumiwa na shule kumfukuza umetosha au la?
Nikukumbushe kuwa malezi ya mtoto yapo kwa jamii kwa asilimia kubwa, na sio kwa mzazi
Jamii iliyoharibika Kama hii inahitaji majaliwa ya Mungu ili mwanao anusurike,
Usijidanganye kuwa mzazi ana nguvu za kutosha za kumfunda mtoto akafundika!

Hio ndio sababu watoto wako umewafungia getini,. Umejua nguvu yako ya kufunda haitoshi chochote, hivyo umeomba nguvu ya geti lako,

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Subiri jamii ikulelee mtoto ili uongeze emojs za kuchekelea.
 
Back
Top Bottom