Wazanzibari Wenyewe Mnajirudisha Nyuma: DR. Salim | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibari Wenyewe Mnajirudisha Nyuma: DR. Salim

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Jun 28, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika (OAU) Dk. Salim Ahmed Salim amewataka wazanzibari kushikamana katika kudai haki zao na kuacha kutumia visingizio visivyokuwa na msingi ambavyo vinaweza kuongeza joto la kisiasa na kukwamisha maendeleo ya Zanzibar.

  Dk. Salim ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuzindua kitabu kilichotungwa na Professa Thomas Burgess, Ali Sultan Issa na Maalim Seif Sharif Hamad kiitwacho ‘Race Revolution and the Struggle for Human Rights in Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika ukumbi mpya wa Al- Yamin Funguni Mjini Zanzibar.

  Alisema tofauti za kisiasa hazina budi kuwachwa kwani zinaweza kuchangia migogoro katika nchi hali ambayo inaweza kusababisha machafuko kama nchi nyingi za Afrika ambazo zimeingia katika vita bila ya kutarajia kutokana na kushindwa kuvumiliana na kuendekeza mambo madogo madogo ambayo hayana faida kwa taifa.

  Dk. Salim alisema njia moja iliyo sahihi kwa wazanzibari kabla ya kushugulikia mambo mengine ni kuungana kwa lengo la kudai haki katika muungano na kuacha kuleta visingizio ambavyo havina msingi wala nia ya kujenga mustakabali mzuri katika nchi na wananchi wake.
  “Kabla ya kushughulikia mambo ya msingi kwanza tuungane kwani watu wanataka haki zaidi katika muungano na tusiwasingizie watu wengine ni mambo yetu wenyewe kama hili la upemba na uunguja, tumejiingiza katika mambo ya kijinga kabisa yasiyo na msingi, wewe CCM wewe CUF hayana maana yoyote” alisema Dk Salim huku akiungwa mkono na washiriki kwa kupigiwa makofi.

  Dk. Salim ambaye kwa kiasi kikubwa alizungumzia umuhimu wa mshikamano miongoni mwa jamii alisema wapo baadhi ya viongozi wa Tanzania Bara ambao hawautaki muungano kama ilivyo kwa baadhi ya wazanzibari lakini alitahadharisha hali hiyo na kusema ni hatari katika dunia ya sasa.
  “Tufahamu katika dunia ya leo watu wanapenda tuweke mshikamano hata katika nchi kubwa tunaona wenzetu wan chi za ulaya wanavyoungana na kuunda European Union” Alisema kiongozi huyo.

  Alisema licha ya kuwepo dosari za msingi za hapa na pale katika muungano lakini hakuna mtu mwenye akili timamu atakayeukataa muungano kwa sasa ambapo umetimiza zaidi ya miaka 45 ambapo alisema dosari hizo zinapaswa kuzungumzwa na kupatiwa ufumbuzi ili kuwa na hali ya usalama nchini.
  “Katika muungano kila mtu anasema kuna kasoro lakini hilo sio kama haliwezi kuzungumzwa ni jambo la busara kwanza tuungane wenyewe na baadae tukae kulizungumza” alisisitiza Dk. Salim.

  Awali katika hafla hiyo washiriki walisema kumekuwepo na unafiki mkubwa kwa baadhi ya viongozi Zanzibar waliopo madarakani hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kukosekana haki ya wazanzibari katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Washiriki hao wamesema mbali ya kuwepo usiri, woga na unafiki lakini pia baadhi ya lawama zimetupwa kwa viongozi wa Tanzania bara ambao wanaikandamiza Zanzibar kwa makusudi jambo ambalo Dk Salim alisema kwa sasa hakuna haja ya kumtafuta mchawi kwani wachawi ni wazanzibari wenyewe ambao hawataki kuleta umoja na mshikamano katika nchi yao.
  “Mimi ni CCM ni Seif Sharif ni CUF lakini mchango wake ni mkubwa katika nchi hii mbona tunakaa pamoja kwa nini isiwezekane kwa wengine mimi nadhani tuanzie hapa” alisema Dk. Salim huku akipongezwa na washiriki.

  Akizungumzia suala la uandishi wa vitabu Dk. Salim aliwapongeza walioandika kitabu hicho na kusema kwamba wakati umefika wazanzibari wenyewe kuandika historia ya nchi yao kwani baadhi ya watu wamekuwa mahodari wa kuiandika historia ya Zanzibar lakini mara nyingi wamekuwa wakipotosha baadhi ya ukweli.

  Katika hatua nyengine Msaidizi wa Maalim Seif, Ismail Jussa amelelemikia kitendo kilichofanywa na mawaziri wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na viongozi wa CCM kukataa kuhudhuria katika hafla hiyo licha ya kupewa mwaliko.
  “Mara nyingi mawaziri wa SMZ na CCM huwa hawataki kuhudhuria shughuli tunazowaalika wakati sisi wanapotualika tunakwenda lakini hili wanajua kabisa kuwa kitabu hiki kitazinduliwa na Dk. Salim wamekataa kuja kwa makusudi pamoja na kuwa ni kiongozi wao ndiye tuliyemualika kuwa mgeni rasmi” alisema Jussa.

  Katika hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi na watu mbali mbali mashuhuri wakiwemo viongozi wa vya upinzani, watu waliopigania uhuru wa Zanzibar pamoja na Nassor Hassan Moyo ambaye ana ushawishi mkubwa wa kisiasa visiwani Zanzibar.

  Viongozi ambao hawakuhudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna, Waziri wa Maji, Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Ali Mzee Ali, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Machano Othman Said na wengineo.


  SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Salimu anaonyesha ukomavu wake kisiasa na nafikiri angetufaa sana kama angepewa nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania, labda angeweza kukemea ufisadi kuliko serikali tuliyo nayo sasa ambayo inakumbatia sana ufisadi au niseme ni sehemu ya ufisadi. Ni kweli tatizo la Wazanzibar ni kuwa na umoja na kuwa na sauti moja lakini tatizo lao ni kwamba kila mtu anashika lake halafu at the end of the day wanalaumu wanaburuzwa na Tanganyika (sikukosea kutoandika Tanzania).

  Tiba
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Baada ya Kongamani hili ndio Prof Othoman Hourob ndio alikwenda nyumbani na Kufariki Dunia
   
 4. nkawa

  nkawa Senior Member

  #4
  Jun 28, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na alikuwa na tiketi ya ndege na Dr. Salim tayari kwa safari ya Algeria kwenye mkutano....Tusio na imani tutafikari wamemmaliza........ labda ni tatizo dogo la kiafya.

  RIP
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jun 28, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sina uhakika kama Wanzazibar watamuelewa Dr Salim Ahmed Salim...! Chuki za wewe Mpemba Na wewe Mmakunduchi, wewe CCM na wewe CUF... Mmh! Kuna kazi kubwa sana miongoni mwa Wanzazibar kulielewa hili.
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hao waliokataa kuhudhuria hafla hiyo wameidhalilisha demokrasia, tatizo la CCM - ZNZ ni umbumbu wa viongozi na mentality ya kila kinachofanywa na CUF ni kibaya
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Jun 28, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..Salim Salim naye amenyimwa haki gani ktk Muungano huu?

  ..wasitusumbue hawa.

  ..dawa ya kuondokana na kadhia hii ni kuvunja muungano.
   
 8. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwa mana hiyo unataka nchi irudishe jina lake asilia la TANGANYIKA ?
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Harakati hizi haziwezi kukoma kama uhuru wa kweli na mabadiliko ya kweli hayapo
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Salim ana vipaji vyake na uzoefu wa hali ya juu lakini sidhani kama anafaa kuwa raisi. Kipaji kikubwa na ujuzi mkubwa wa Salim uko kwenye diplomacy na hatu hitaji raisi awe kama waziri wa mambo ya nje. Salim akiwa raisi nguvu yake itakuwa kwenye kuconcentrate kwenye kujenga urafiki na mataifa makubwa na kukazania foreign policy. Kwa wakati huu Tanzania inahitaji raisi atakae kazania mambo ya nyumbani na ambae anajua siasa za nyumbani vilivyo. Pia mimi naona Salimi ni generation iliyo pita sasa hivi Tanzania we need a new breed of leaders who are not a result of the independence struggle, ujamaa nk.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Jun 28, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Sonara,

  ..Aboud Jumbe pamoja na kufukuzwa uongozi amejibanza Mjimwema.

  ..marehemu Sheikh Idris Abdul-Wakil Nombe tulikuwa naye Buguruni miaka nenda rudi.

  ..Mzee Mwinyi ana mashamba kibao Morogoro na mkoa wa Pwani.

  ..Salim Salim ana kasiri na kutisha maeneo ya Masaki.

  ..halafu leo wanaitana Zanzibar ati waungane kudai haki zao ndani ya Muungano. haki gani walizonyimwa hawa? mbona wana maisha mazuri kuliko wazee wetu wa-Tanganyika kama akina Apiyo na wengine wengi tu?

  ..na hicho kitabu walichoandika nina wasiwasi sana kama hakijaa lawama na masimango dhidi ya wa-Tanganyika.

  ..dawa yao hawa ni kuwarudisha makwao. baada ya hapo turudishiwe TANGANYIKA yetu.
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Chuki chuki chuki! this is uncalled for kinacho kukera sio maisha mazuri na "makasri" ya hao wastaafu ulio wataja. Kwanza huwezi kuwalinganisha marais na waziri mkuu mstaafu na katibu mkuu kiongozi mstaafu hata pensheni na stahiki zao ni tofauti kabisa. Una lako jambo hutaki kulisema na mwenendo wa michango yako of late inaonyesha your true picture.

  Hayo malalamiko ya muungano yapo pande zote mbili za muungano sisi wabara tunalalamika sawa na wao wanavyolalamika. Migongano kama hii haitatuliwi kwa "kuwarudisha kwao", hili ni miongoni mwa mawazo ya kijinga kupata kuyasoma hapa JF. Unaumizwa na maslahi wanayoyapata wazanzibari kwenye muungano unasahau upande wa pili kuna wabara wengi wamefanikiwa na kujijenga Unguja na Pemba je nao "warudishwe kwao?" Na ukitazama kwa darubini kali utakuta hao akina Mwinyi unaotaka "warudishwe kwao" hio kwao yenyewe ni Mponga - Mkuranga!.

  Tunapojadili masuala nyeti kama hayo tuache ushabiki na chuki zisizo na maana tuweke utaifa mbele. Salim anasema wakubwa wa Ulaya wanafikiria kuungaana sie tunafikiria kuvunja muungano. Jokakuu wa JF anasema "warudishwe kwao" as if ni wakimbizi.
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Masatu,
  Operative word hapa ni "haki". Na ukishasema hilo neno ni kwamba kuna hisia upande mmoja unaonewa katika muungano. Mimi ni muumin na life supporter wa muungano. Lakini nikisikia upande mmoja unalalamikia haki, nigependa kujua ni wapi wanapoona kuwa wanaonewa ili haya mambo tuyaweke bayana. Na hata kama hukubaliani na maoni ya Jokaa Kuu, si uungwana kuyaita maoni yake ya kijinga. Anye one enisoka Majita!
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jasusi ndio maana nikasema kuna malalamiko kutoka kwa pande zote mbili za muungano iweje leo tunaona ya wazanzibari tu?

  Ni kweli sikubaliani na maoni ya Jokakuu kwa asilimia 100 lakini na nilichoshambulia ni hoja sio mtu. I choose my words very carefully. Enyi one nsoka Zanzibar!
   
 15. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naskitika kwa Pro. Haroub.- Ni mzanzibari, akiiipenda nchi yake. tutaendeleza?.
   
 16. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  si wamesema wanamafuta na hawataki ku share na bara

  kinachotakiwa ni serikali moja
  unguja mkoa na pemba mkoa
  total population ya zanzibar ni sawa na mkoa wa kinondoni
  lakini znz kuna raisi, mawaziri na viongozi kibao halafu kazi hamna...

  lakini kama muungano huu wa znz wana rais halafu bara hawana haufai, wala serikali tatu no....
  wakati umefika wa serikali moja au basi lakini haya mambo ya znz kila siku kusema sisi ndio tunawanyima maendeleo haiwezekani......

  embu fikiria mwanza ni kubwa kuliko znz, ina watu wengi mara mbili ya znz, uchumi wake ni mkubwa kuliko znz lakini znz kuna wabung 50 na mwanza 13
  halafu bado wanaonewa na bado kuna baraza la wawakilishi...
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Semilong yani hapa tuna mawazo sawa kabisa. I have to say I agree with you 100%. It's time tuwe na serikali moja and it's time Zanzibar stop using the Union as a scapegoat to all it's problems.
   
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Jun 29, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ukuwahi kusikia ule msemo... kifo cha mdomo mate utawanyika?

  Basi na tuubirie tuone mwisho wake...!
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Jun 29, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Masatu,

  ..Wazanzibari wanadai wananyimwa haki lakini hawaishi kungangania huku Tanganyika.

  ..kama kweli Tanganyika na wa-Tanganyika wangekuwa wabaya kiasi hicho, na wanawanyima haki basi, wangeisha ondoka kurudi kwao.

  ..tena wanadai "Wazanzibari tuungane kudai haki zetu" sasa nini kinakufanya wewe uamini kwamba wao na sisi tu wamoja?

  ..unadai tuweke UTAIFA mbele, sasa of all the ppl Salim Salim kwenda kutoa kauli ile "Wazanzibari tuungane kudai haki zetu" hivi unaona ameweka utaifa mbele? au tunaotakiwa kuweka utaifa mbele na wa-Tanganyika tu?

  ..binafsi sioni ambacho Mtanganyika anaweza kukipata huko Zanzibar ambacho hawezi kukipata hapa Tanganyika. Mtanganyika hana maslahi yoyote yale na muungano huu.

  ..ni kweli kwamba wakubwa wa Ulaya wanasisitiza sana masuala ya muungano. lakini tukumbuke kwamba wana sababu zao.

  ..kabla ya Watanganyika kurukia tu mawazo ya wakubwa, tunapaswa kuchunguza faida wanazozipata wakubwa hao kwa kuungana.

  ..WATANGANYIKA TUNAPATA FAIDA GANI KWA KUUNGANA NA NCHI YENYE WATU WACHACHE, ENEO DOGO, NA RASILIMALI KIDUCHU, KAMA ZANZIBAR?

  Jasusi,

  ..watu kama Masatu huwa nawapa "thank you" hata wakinitukana!!

  ..and I never reply in kind kwa matusi yao.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jun 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jokakuu,
  Mkuu kwanza ni lazima uelewe kile alichozungumzia Slaim A. Salim. kabla hujaanza kubwatuka..
  Hakuna swala la Ubara na Uzanzibar zaiodi ya tofauti ya mke na Mume ktk nyumba. Mke akiomba haki zake haina maana katoka ktk ndoa na wala akikaa kimya haina maana hakuna kasoro ktk ndoa... Muhimu utambue kwamba hatukuwa Tanzania bila Muungano, hili neno usilichukulie juu juu tu kwa sababu wewe unajiona bwana ktk Muunganoi huu..
  Anachozungumzia Salim ni kwa Wazanzibar kuungana wenyewe ili kuweka hoja zao pamoja ili kurahisisha ufumbuzi wa matatizo yote lakini kinachofanyika sasa hivi Zanzibar kama mwanamke mnafiki husema nje kuhusu mabaya ya Mumewe na mara zote hataki kusikiliza upande wa pili isipokuwa yale anayoyataka yeye na kibaya zaidi haihusiani na mabaya isipokuwa ndoa yenyewe...

  Kinachokera zaidi ni mambo ya Siasa kama vile Zanzibar hudai kuonyeshwa hati ya Muungano as if ile hati ndio inayowaweka ktk muungano huu..Sasa fikiria mkeo anasema nionyeshe cheti cha ndoa wakati mke huyo huyo akidai taraka!..Sasa taraka ya nini ikiwa wewe huitambui ndoa na bado uko ndani ya nyumba kama mke.. Na mara nyingi basi utaoona wakidai haki za mke kwa sababu wamevaa pete ya harusi.. wanakumbuka vizuri kuvaa shera, furaha ya harusi na kadhalika lakini maneno yote yanawatoka kwa sababu hawana furaha ndani ya ndoa hii kutokana na mume kuwa mweka hazina, mwenye sahihi ya account Bank..

  Sasa kwa mtu kama mimi mwenye kufikiri nje ya box najua fika kabisa watu kama Maalim Seif hawana nia nzuri na wananchi wa Zanzibar kwa sababu hatuwezi kugombana kwa sababu ya cheti au mwenye sahihi Bank, sahihi ambayo inahusu zaidi nani anaruhusiwa kutoa fedha za jamhuri Bank..Hiii ndio vita yao kubwa ya wanasiasa wa Zanzibar pamoja na kwamba wanayo account yao. matumizi makubwa wanataka kuvuta zaidi toka account ya pamoja (kitaifa) kwa sababu Mikopo mingi na misaaada huingia ncxhini kwa jina la Tanzania lakini wao wakichukua mikopo huingia kwa jina la Zanzibar, bara hatuna mkono ndani..

  Kwa hiyo Kisiasa wanaposimama majukwaani kuwatangazia Wazanzibar hupenda sana kutumia lugha za kuonewa, kunyanyaswa na pengine hata kupangiwa matumizi wakati wananchi wa bara pia hupangiwa matumizi na serikali hiyo hiyo wanayoipigia makelele.. wanajua fika jinsi Viongozi bara wanavyofisadi nchi, wao poia wanataka mkono ndani.. na ndsio maana huoni wakipinga Ufisadi.. Kina Karume wamechukua majumba ya serikali tena nasikia kachukua yale majumba yaliyojengwa na serikali ya marehemu baba yake kule Michenzani na kuzifanya zake..Sijasikia Maalim Seif akiwashusia CCM Zanzibar kwa ufisadi wanaoufanya kuuza Beach areas (Privatise ardhi) na sehemu muhimu za Historia ya nchi ile (utumwa) kwa wageni..Argument yao kubwa It's all about the Union!

  Matatizo ya ndani tu yanawashinda kuyaweka wazi na kuwalaumu vviongozi wahusika badala yake wanatumia UNAFIKI kutafuta mchawi toka bara na sii visiwani. Nguvu na povu la kinywa humtoka Maalim Seif ktk maswala ya Muungano zaidi ya matatizo ya ndani kwa sababu anajua hawezi kuweka upinzani dhidi ya viongozi wa Zanzibar wakati yeye ni mwakilishi mkuu wa CUF Zanzibar.. Aghlab kumsikia akizungumzia maswala ya Zanzibar na Ufisadi kama kina Dr. Slaa hata akiwa Bungeni..

  Kwa hiyo, Salim mbali na kuzungumzia haya kwa lugha ya Kiungwana - to be Politically Correct..kawastahi viongozi wa pande zote mbili ambao wanautumia Muungano kama kisingizio cha matatizo yao wenyewe.. Always ikiwa hakuna maelewano ktk ndoa basi wakosa ni binadamu walioingia ndoa hiyo na sio ndoa yenyewe kuwa sababu ya matatizo yao..I mean hata kwa kutumia logic tu haiwezi kuingia akilini..
  Tatizo letu sisi wote tunafikiri kwamba Muungano ndio wenye matatizo badala ya kujitazama sisi wenyewe tuliounda huo Muungano..Ni sisi tunaoweza kuuweka Muungano ktk hali yoyote ile na siii Muuungano kutupeleka sisi.. What happens imetokana na sisi wala sii Muungano hata kidogo, kwani matokeo yoyote ya Muungano (mabaya/mazuri) yanatokana na sisi tulioingia ktk ndoa hiyo....
   
  Last edited: Jun 29, 2009
Loading...