Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 14,176
- 25,919
Ilikuwa hivi, tarehe 12 January, wazalendo wa Zanzibar, karibu wote weusi, walichukua silaha za jadi na kuteka ghala la silaha kisha kfanya mapinduzi kuuondoa utawala wa Kiarabu visiwani. Wakiwa wamejaa shamra shamra za mapinduzi walianza kuwachinja waarabu na kufanya mauaji makubwa mengi yasiyo hata na sababu.
Wanamapinduzi wa Zanzibar walifanya mapinduzi dhidi ya serikali ya Kiarabu ambayo iliwekwa pale na utawala wa kisultan wa Oman. Waarabu wengi walikimbia na wengine kwenda Oman.
Sasa sasa Zanzibar wakawa wameliamsha. Oman walipopata hii habari, kwamba mapinduzi yamefanyika na ndugu zao wameuwawa, wakaanza kuandaa manowari za kijeshi kuja Zanzibar kufanya counter revolution. Wakiwa na hasira na kujaa kisasi, walinuia kuja kutoa fundisho ambalo Zanzibar wasingelisahau. Wanamapinduzi wa Zanzbar wakaingia hofu kubwa sana, wakijua mwisho wao umefika, na kwamba watu weusi Zanzibar wangepigwa mizinga na waliosalia kuchinjwa wote na wanajeshi wa Oman.
Ndipo Karume akamwomba sana Nyerere awasaidie, awaokoe. Nyerere akasema siwezi kutoa jeshi ili kupigana na Sultan wa Oman katika suala ambalo ni jambo la ndani la Zanzibar. Lakini akamwambia, njia rahisi, ni kwamba serikali ya Zanzibar iungane na Tanganyika.Tukifanya hivyo Oman hawezi kuipiga Zanzibar, kwa kuwa watatakuwa wanavamia nchi huru inayojitegemea inayojumuisha Tanganyika na Zanzibar.
Karume akafurahi sana kusikia busara hizi za Nyerere. Akasema sawasawa mwalimu, basi tutangaze tumeungana, wewe raisi mimi makamu wako, na kuanzia sasa Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika. Nyerere akacheka, akasem sio rahisi hivyo Abedi. Pamoja na uharaka uliopo, hatutaki tuonekane Tanganyika tumewameza Zanzibar. Lakini pia hatuna muda, maana manowari za kijeshi za Oman ziko njiani kuja kufanya counter revolution.
Basi wakafanya makubaliano ya muungano haraka haraka ambayo kimsingi hayakuwa majadiliano, bali mapendekezo ya Nyerere,mambo kama 11 hivi ya muungano. Karume yeye alikuwa anakubali kila kitu, akihofia Wazanzibar wote kuuwawa na utawala wa Sultan wa Oman.
Ndio maana mapinduzi Zanzibar yalifanyika tarehe 12 January 1964, na kama miezi miwili baadae tarehe 26 April 1964 muungano ukatangazwa rasmi, kwamba sasa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
Kusikia hili Sultan wa Oman ni kweli alirudisha manowari zake za kivita na kuachilia mbali mpango wa kuja kufanya counter revolution, na watu wa Zanzibar wakawa wameokoka kipigo na kuchinjwa kwa kisasi cha Oman. Lakini bado waarabu wa Oman wliapa kwamba watatafuta namna ya kulipiza kisasi, hawatasahau.
Sasa Wazanzibar wanapaswa kukumbuka hili wanapotupigia kelele watu wa bara kuwa tumewatawala nk. Bila hii plan ya haraka haraka leo Zanzibar isingekuwa na mtu mweusi hata mmoja. Nyerere aliwaokoa, na hivyo badala ya kuwalaumu bara Zanzibar wanapaswa kuwashukuru sana, labda kama wanaolalamikia bara ni wale wenye asili ya uarabu ambao siku zote watamlaani Nyerere. Kumbukeni Nyerere alitumia busara sana kuweka makubaliano ya muungano katika kipindi kifupi sana ili kuinusuru Zanzibar. Ni kweli baadae kuna mambo yalipaswa kurekebishwa taratibu, lakini msichukulie kama bara waliitapeli Zanzibar. Huko ni kukosa shukurani.
Hivi huko Zanzibar mna sanamu ya Nyerere hata moja kama kumbukumbu ya kuwaokoa na kuchinjwa wote?