Wazanzibar muungano tutaununua...

Wazanzibar muungano tutaununua...

Status
Not open for further replies.
Usiumize kichwa sana ndugu yangu kuhusu mimi na uzanzibar wangu cha msingi kaa ufikiri ni Zanzibar ya aina gani uionayo nje ya muungano. Unguja ukuu Tindini ndo Kwa baba.Konde Pemba ndo kwa mama.

Umekuja zanzibr kwa mbio za mwenge,saa ya ukombozi ni sasa ondoa woga,zanzbr kwanza.
 
Zanzibar wana gubu,tuitoe Zanzibar alafu tuungane na Comoro
We vipi? Kisha tuwagawie madaraka ya kutawala nchi yetu halafu watutukane kama wanavyofanya wazanzibari. Kwani hujui kinasaba na kitamaduni comoro na znz ndio hao hao?
 
Usiwe na wasi wasi ndugu yangu, Zanzibar itakuwa Singapore ya Afrika Mashariki ingawa mwanzo wake unaweza kuwa mgumu kidogo lakini baada ya miaka kama hamsini hivi kila mtu ataitamani Zanzibar.

Mbona comoro si kama hiyo sungapore unayosema mzee
 
Umekuja zanzibr kwa mbio za mwenge,saa ya ukombozi ni sasa ondoa woga,zanzbr kwanza.

Ndugu yangu hebu jaribu kuficha ujinga kidogo,hivi umesahau Zanzibar ni kisiwa na sote sisi ni wakuja? Jenga hoja vipi tutasimama kama nchi nje ya muungano?
 
Ni kweli, miezi miwili na nusu ya uhuru ilikuwa ngumu sana kwa marehemu Karume kushikilia dola ya visiwa viwili kama nchi moja - alishalemewa sana na hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe - kama historia inavyoonesha. Lakini kwa sasa mazingira ni tofauti na wakati ule tulipohitaji msaada wa Watanganyika ili kuepuka balaa baada ya Mapinduzi matukufu. Sasa tunaweza kabisa kujisimamia kama nchi. Historia imebadilika, watu wamebadilika, mazingira ya ki-dunia yamebadilika. Tunawashukuru Wabara kwa kupita nasi kipindi kile kigumu, lakini shukrani na heshima hii itapungua na kubadilika iwapo mtaendelea kufikiri mtoto akishakua anahitaji tena kutunzwa na kusimamiwa na mzazi. Mzazi mwenye busara humpa mtoto heshima na uhuru wa kujitawala muda unapofika kufanya hivyo!
Wakati ule karafuu ilikuwa ni kama mafuta kwa visiwa vya Zanzbar! Zanzbar ingeweza kujiendesha kiuchumi wakati ule lakini sio sasa! Mchango wa muungano kwa uendeshaji wa serikali ya mapinduzi ni mkubwa sana ila wengi wanaopiga kelele kuuvunja muungano ama hawajui au wana malengo yao binafsi!
 
kuna mawaziri wamelalamikia sana rasmu ya pili ya katiba kuja na muarobaini wa serikali tatu,kwamba watakuwa nje ya bunge la bara ambaro lina mvuto,lina changamoto,lina fursa,malipo yake makubwa,wanalia kwelikweli kuhusu kuwepo na serikali tatu na wanadai watapinga kwa nguvu zote serikali tatu ili waendelee kuwemo katika bunge la bara.wanadai bunge la zanzibar linafanana na kikao cha baraza la madiwani la halmashauri.
 
Ndugu yangu hebu jaribu kuficha ujinga kidogo,hivi umesahau Zanzibar ni kisiwa na sote sisi ni wakuja? Jenga hoja vipi tutasimama kama nchi nje ya muungano?

Historia inaonyesha zanzibar ilikuwa nchi na mamlaka yk, fedha zake, bendera na wimbo wa taifa watoto walikuwa wanaimba mashuleni kabla ya muungano huu wa kidhalim wa JMT, na Zanzibar iliweza kusimama kilivyo kama nchi.,

Nyerere ambaye Tanganyika ni baba yenu wa Taifa ndio alimshawishi karume kuungana kumbe alikuwa na lake rohoni, baada karume kugundua Tanganyika wanataka kuimeza zanzibar mukampiga risasi kumuua, kutoka hapo ilikuwa mtu yeyote akiutaja muungano alikuwa anaitwa muhaini kufungwa jela miaka isiyojulikana.,

Usizuge zuge watu unataka hoja gani., mbona munapenda kujitoa fahamu???
 
Ndo maana nikasema wazanzibar tulio wengi ni wafuata midundo inayopigwa na akina
Jussa na Maalim Seif,
Hata kama dhamira yetu ni kua nje ya muungano matusi,kejeli,dharau,kedi,kujisikia sisi bora kuliko wao havitusaidii.
 
Mkuu,

Angalia usije sema hata mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ya kikristo-kafiri,maana aliyefanikisha anaitwa mkristo-kafiri John Okello!Au naye mnataka kumfuta kwenye historia!

Poleni!Ila ndio ukweli mchungu huo!

Hakuna mkristo Zanzibar ambaye asili yake si mtanganyika, tembea kote na hizo zilikuwa mbinu za nyerere baada kumshawishi karume kuungana ili lengo lake 1 ni kuidhoofisha dini ya kiislam zanzibar.,

Na ndo mana sasa vichogo vimetapakaa zanzibar wakuria kutoka bara wamejenga makanisa maeneo mengi kutapakaza ukiristo dini ya kikafiri., kwani unafkiri wale uamsho wamesekwa ndani ni amri kutoka Tanganyika Kanisa ndio linalotuongoza kutoka bara, ndo mana wazanzibar wanadai nchi yao na mipaka yao ili mwisho wenu iwe chumbe.,
 
hongereni kwa mada nzuri. Ngoja kesho niwaulize jamaa zangu kino Moyo, vijana maarufu hapa mjini songea kama watarudi znz au watakuwa watanganyika ili nasi turithi kazi zao wazifanyazo hapa maisha yetu yanyooke! Jamaa wako vizuri na wapo hapa tangu siku nyingi tu. Nahisi hawatakubali kwenda zenj! Mie nashauri vyovyote itakavyokua, tuendeleze mahusiano yetu yaliyopo.

mahusiano mazuri kabisa kwa ndugu zetu wa tanganyika labda iwe ni kama vile wazanzibar wanaoish canada, uk, ama nchi nyengine ulimwenguni lakin siyo kama ilivyo hivi sasa wanaingia tu kiholea kujenga makanisa., na skuizi huwa wanakuja na madebe ya tindikali wanawamwagia watu alafu wanachomoka wanawasingizia wazanzibar na kuwapa majina mabaya ya ugaidi na alshabab
 
Tafadhali usiweke hoja za udini ktk hii mada.
Hata John Okello ameshirikiana bega kwa bega na kina Shamte,Thabit Kombo,Karume mbona hawakumtimua kwa dini yake?
 
Hakuna mkristo Zanzibar ambaye asili yake si mtanganyika, tembea kote na hizo zilikuwa mbinu za nyerere baada kumshawishi karume kuungana ili lengo lake 1 ni kuidhoofisha dini ya kiislam zanzibar.,

Na ndo mana sasa vichogo vimetapakaa zanzibar wakuria kutoka bara wamejenga makanisa maeneo mengi kutapakaza ukiristo dini ya kikafiri., kwani unafkiri wale uamsho wamesekwa ndani ni amri kutoka Tanganyika Kanisa ndio linalotuongoza kutoka bara, ndo mana wazanzibar wanadai nchi yao na mipaka yao ili mwisho wenu iwe chumbe.,

Mkuu,

Hivi unajua hakuna mwenyeji wa Zanzibar?

Hivi unajua Muarabu aliviokota visiwa hivyo vikiwa havina mtu aliyekuwa akiishi hapo?Au uniambie aliyakuta makabila gani visiwani hapo!

Hivi unajua nyote weusi mnaoishi Zanzibar ni uzao tu wa watumwa kutoka bara waliosafirishwa kwenda visiwani 'kupigwa bei'?

Hizo porojo za wakristo wanatoka bara muache kudanganyana,nyie nyote ni uzao wa watumwa wandengereko,wamakonde na makabila mengine kwa hiyo angalieni,unapombagua mkristo yawezekana unambagua KAKA au DADA yako!

Dini isikufanye BOGUS wakati hata dini uliletewa na walewale waliosafirisha Baba na mama zako na kubaka dada zako na wengine kuwauwa wakiwa kwenye misafara ya watumwa kuingia visiwani humo!

THING BIG!
 
TAFADHALINI HOJA ZA UDINI KTK HII MADA HATUZIHITAJI.

Wewe kama imekugusa lete hoja tunakoelekea ni kwamba muda wowote Tanganyika itakua na mamlaka yake na Zanzibar itakua na mamlaka yake nje ya muungano. Vipi tumejipanga kama wazanzibar kujiendesha kama nchi kamili na je yakitushinda haiwezi kua ndo mwanzo wa kuja kuwalilia watanganyika turudiane?
 
Tafadhali usiweke hoja za udini ktk hii mada.
Hata John Okello ameshirikiana bega kwa bega na kina Shamte,Thabit Kombo,Karume mbona hawakumtimua kwa dini yake?

Okelo hakushirikiana na uliowataja kujenga makanisa zanzibar, makanisa yameanzia na kuzidi utawala wa nyerere babaako wa taifa., hii ndio sababu 1 kubwa wazanzibar kuukataa muungano maadili ya wazanzibar yanapotea na kuporonyoka kila leo., sasa basi tunataka tupumue
 
Binafsi sifahamu kwanini likitajwa hiliwazo la zanzibar kuwa na mamlaka yake ndugu zetu wa Tanganyika wanakuwa na hofu kuwa zanzibar haiwezi kjitawala wenyewe,Hivi kwanini watanganyika wafikirie kuwa wazanzibar hawawezi kujitawala???

Halafu kuna hawa wanaosema kuwa sultan wa zanzibar alikúwa mkoloni,kwa muono wangu Sultan alikuwa sio mkoloni kama alikuwa ni mkoloni mbona kaomba ukimbizi United Kingdom(Uingereza) kwani asirudi kwenye nchi yake ya Oman,Ukweli familiy za hawa watu wamekaa Zanziabr zaidi ya karne mia 600,Tujiulise raisi wa kwanza wa zanzibar familiy yake ina miaka mingapi zanzibar

Nashukuru sana Internet kwa kuleta habari za kila upande kwani wakati tunasomeshwa na serikali ya mapinduzi propaganda zao za kisiasa ni kuwa warabu walikuwa ni watu wabaya na hakuna jema walilofanya zanzibar uongo hkama huo sasa uko wazi kila kitu kinapatikana kwenye internet.

Tuanatakiwa tufahamu kuwa zanziabr ni visiwa,visiwa vyote duniani kuna mchanganyiko wa watu,watu wote kwa ujumla wanaoishi visiwani ikiwa zanziabr au jamaika au seyshells ni wahamiaji,sasa kubagua kikundi cha watu kuwa ndio wenye haki ya uraia na wengine hawana haki ni ukiukwaji wa haki za binadamu ni ubaguzi wa rangi,hali hiyo aliiona Mandela na ndio maana hakufanya makosa waliyofanywa na viongozi wengine wa kiafrika kuwabagua raia wao kwa rangi zao za ngozi
 
Kuna lugha inasema " You never know the importance of a thing until you loss it" Kiingereza changu kibovu lakini nadhani nimeeleweka.
Mkuu, kweli kiingereza kibovu ila umeeleweka. Ukitaka kujua umuhimu wa ----, uwe na jipu!!
 
Mkuu,

Hivi unajua hakuna mwenyeji wa Zanzibar?

Hivi unajua Muarabu aliviokota visiwa hivyo vikiwa havina mtu aliyekuwa akiishi hapo?Au uniambie aliyakuta makabila gani visiwani hapo!

Hivi unajua nyote weusi mnaoishi Zanzibar ni uzao tu wa watumwa kutoka bara waliosafirishwa kwenda visiwani 'kupigwa bei'?

Hizo porojo za wakristo wanatoka bara muache kudanganyana,nyie nyote ni uzao wa watumwa wandengereko,wamakonde na makabila mengine kwa hiyo angalieni,unapombagua mkristo yawezekana unambagua KAKA au DADA yako!

Dini isikufanye BOGUS wakati hata dini uliletewa na walewale waliosafirisha Baba na mama zako na kubaka dada zako na wengine kuwauwa wakiwa kwenye misafara ya watumwa kuingia visiwani humo!

THING BIG!

Mkuu kweli unayoyasema,lakini nikukumbushe tu kabla ya mwarabu kuhamia zanzibar walikuwepo wareno,wareno wao hawakutawala lakini waliishi hapo kwa muda miaka 500 na walijenga na makanisa madogo madogo,historia ya zanziabr inasema kuwa warabu waliitwa na wenyeji wazanzibar ili waje wawatoe wareno tafauti iliyokuwepo kati ya wareno na wenyeji wa zanzibar ilikuwa dini wareno walikuwa wakrisro wenyeji walikuwa waislam.sasa jiulize hao wenyeji wa zanziabar kwa wakati huo walikuwa nani,au ndio kama unavyosema walikuwa watumwa

Sasa hizo tuhuma kuwa mwarabu alivikuta visiwa vitupu ziweke kando,pili ukiristo ulitokea zanziabr ndio ukafika Tanganyika,tatu wanzanibari walikuwa wanajitawala wenyewe kabla hawajatawaliwa na mwarabu,hizi habari zote ziko kwenye internet google utazipata
 
hapa umeichanganya historia.waarabu walianza kuja pwani ya east Africa kabla karne ya 5-7 kwa misingi ya biashara na si kuongoza ni kweli yawezekana kulikuwa na watu Zanzibar ila walikuwa wachache nao walitoka bara(sio Tanganyika pekee).mreno alikanyaga pwani ya kilwa karne ya 15 tena mwishoni na alikuta mwarabu akiendesha biashara ikiwemo utumwa katika ukanda huu.pengine unaweza ukajiuliza jambo dogo kwann mwarabu aliitawala sana Zanzibar tofauti na pwani ya bara? jibu ni dogo nani kama la mchangiaji niliyemnukuu visiwa hivi havikuwa na idadi kubwa ya watu hivyo kuwa summon na kuwa rule likawajambo rahisi.utumwa ulichangia kuweka idadi ya weusi kuongezeka ndani ya visiwa hivi.jamii yote ni moja ila imetenganishwa na mazingira.na wareno hawakutawala kwa miaka 500 hilo ni hapana walitawal kwa takriban karne 2 kisha waarabu mwishoni mwa karne ya 18 wakawatoa kwenye miji ya pwani za Zanzibar,kilwa na Mombasa.kwa wakati huo ukoloni haukuwa unatambulika kwenye maskio ya watu weusi na ile dhana ya kuwa weupe ni watu waliobarikiwa iliganda kweny vichwa vya wazee wetu.bado ukweli ni kama ule aliousema ndugu yangu hapo juu watu wa visiwa hivi ni zao la mchanganyiko wa watu wa bara.kuna wanyamwezi wengi tu Zanzibar na sio rahisi kumtambua mpaka akupe mwenyrwe ukweli
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom