Angalau umekiri "kipindi kile" hamkuweza kujisimamia kama nchi na hilo halina ubishi. Lakini tatizo linakuja pale ambapo baadhi yenu hamuishi kuitukana Tanganyika kila uchao pamoja na fadhila zote mlizotendewa. Chini ya mbingu ni mahali gani ambapo mZanzibari anaishi kwa uhuru tena bila nyaraka zozote za uraia kama Tanganyika? Ni wapi anapoweza kumili rasilimali zikiwamo ardhi, biashara, na nafasi nyingine za ajira kama Tanganyika?
Ni wapi pengine mZanzibari anaweza kuwa hadi Rais wa nchi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri, mbunge, na nafasi nyingine lukuki za uongozi kama Tanganyika? Ni Uarabuni? Ulaya? Marekani? Uchina? Ushelisheli? Labda Mzee
Barubaru atatuhadithia huko Oman aliko ana nafasi gani ya uongozi wa nchi ile ya kufikia. Au ni wapi Afrika ambako hilo linaweza kutokea? Hiyo nchi haipo na haitakaa iwepo baada ya Muungano huu ambao kimsingi umefikia "point of no return".
Nakubaliana na wewe kwamba mtoto akikua anastahili kuachwa ajitegemee; sawa, ila kinachokera ni jinsi mtoto huyu mpu.mba.vu tena wa kufikia asivyo na adabu kwa mzazi wake aliyemlea kwa jasho na damu. Kama wewe una dini naamini unajua dini zinasemaje kuhusu mtoto wa aina hii! Laana i miguuni pake!