Khawarizm
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 203
- 230
Ina maana wazungu ndio waliowaita weusi washenzi na sio waarabu?.hebu rudia ukweli shenzi ilitumiwa na waarabu katika minajili yakuonyesha ujinga wa zanj people(weusi)
Eti waarabu hawakuwatesa weusi je umepata kusikia habari za zenj rebellion? Ikiwa ilitokea mnamo karne ya 8 au9 hao weusi waliokuwa kwenye mabonde ya Iraq ya sasa walizaa wapi na wameishia wapi? Washenzi walikuwa ni wa zanj ambao ni babu zetu regardless anatoka wapi.ikiwa babu yako ni mwarabu basi hakuwa mshenzi ila kama ni mweusi alikuwa mshenzi kama babu yangu mimi.
Unaishia kusema tu wapo weusi walioenda uarabuni kisha majina hakuna.mbona America inafahamika more than 14% ni blacks weusi wa uarabuni waliyeyuka?
Unapoongelea swala la shule hakuna wazee wa Tanganyika waliosoma? Shule kama ya mwambao primary school iliyokuwa inajulikana kama marien schule iliyojengwa na wajerumani huko bagamoyo haikuwafunza waafrica?
kwanza hili neno Mshenzi si la Kiarabu nitolee ushahidi mmoja kama hilo neno ni la Kiarabu.
Pili kwa mujibu wa huyo huyo W. Ingrams katika kitabu chake amesema kuwa hili neno Mshenzi ni la kiswahili na walikuwa wakiitwa watu kama wao hasa wao wazungu na mwanzo liliwakera ila baadae liliwafurahisha kwani maana yake halisi ni sifa ya mtu mweledi aliebobea (Expartriate) so sio tusi.
Ila kwa fikira za watu wengine wa zamani nilowauliza wanasema hili neno linatokana na hao wakoloni wa Kijerumani kuwaita Waafrika Schwainz yaani Nguruwe na badala yake Waafrika wakalitohoa kilahaja na kulitamka Shenzi na pengine hao hao Waafrika waliwageuzia wazungu kibao na kuwaita wao Shenzi na walipoulizwa maana wakajibu kuwa ni Ubingwa ( kwa ile kawaida ya asiejuwa maana haambiwi maana na ukila na kipofu usiumshike mkono) teh teh teh
Wakush ( Cushites) ndio wametawanyika kila upande hasa baada ya gharika Nuhu Safina ilipotua na wengine bado wako huko huko Iraq ndio wanajulikana kama Zang na ndio wengine kule Iran wanaishi katika jimbo la Shiraz na Waliokuja kusini wakafika katika bara la Africa ndio hao Afariks (Afars wa Djibouti) na Amonites (Wa Amu walisambaa katika visiwa na ukanda wa Afrika Mashariki).
Hawa Afars ndio chimbuko la wasomali, wahabeshi, wasudani, wanubi, wamasai, wapare, wachaga na watutsi na wengineo.