Mapinduzi yalikuwa, kwa kiasi fulani ni kisasi dhidi ya utumwa, yaliofanywa na watu na kufanyiwa watu ambao hawahusiki na utumwa.
Yasmin Alibhai-Brown
Fikra ya uzalendo ya Pan-Africanism ambayo ilikuwa ikiongozwa na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa kila asiye Muafrika ni mgeni Afrika na kwa hiyo asiyekuwa na asili yenye kutoka bara la Afrika basi ni mgeni Zanzibar hata kama alizaliwa na alikuwa na mizizi mirefu ndani ya nchi hiyo. Na aliyekuwa ana asili ya Kiafrika na hata kama hakuzaliwa na wala hana mizizi mirefu Zanzibar basi ana haki zaidi juu ya kuitawala Zanzibar kwa sababu ni Muafrika.
Neno Afrika linatokana na neno
Ifriqiya, ambayo kihistoria ilikuwa ni jimbo la Kaskazini ya Afrika katika nchi ambayo leo inajulikana kwa jina la Tunisia. Ibn Khaldun, mwanafalsafa wa historia maarufu duniani na baba wa sayansi ya jamii (sociology) aliyeishi miaka 676 nyuma, anamtaja katika kitabu chake Mfalme wa zamani wa Yemen Afriqus b. Qays b. Sayfi, ambaye aliishi wakati wa [Nabii] Musa au labda kidogo kabla yake na kuwa wanahistoria wanajisemea kuwa ndie alieivamia Ifriqiyah.1 Ibn Khaldun hakuwa anashuku kuwepo kwa mfalme kutoka Yemen ambaye akijulikana kwa jina la Afriqus ambalo inawezekana sana likawa moja wapo wa asili ya jina la Afrika. Wako wenye kusema neno Afrika linatokana na lugha ya kienyeji ya Afrika ya Kaskazini iitwayo Berber.2 Lini bara la Afrika lilianza kujulikana kwa jina la Afrika ni jambo liloanzishwa na wakoloni wa kizungu na ni suala linahohitajia kuthibitishwa kwa ushahidi wa kiutafiti.
Fikra zilizozagaa ni kwamba Zanzibar ni ya Muafrika mweusi mwenye asili ya bara peke yake kuliko Muafrika mwingine yeyote hata kama amezalika huko Zanzibar kwa daraja nyingi. Fikra hii inatokana na fikra nyengine iliyokalishwa kwenye fikra za wengi yakuwa Bara la Waafrika ni Bara la watu weusi tu, na labda tuseme la Mungu Mweusi. Na watu weusi wenyewe ni wanaotokana na asili ya Kibantu na Wabantu wenyewe wawe hawana asili au uhusiano wa karibu na Waarabu.
Na mizizi ya Waafrika ni Wabantu peke yao inalitenga kundi kubwa la Waafrika wa Afrika ya Kaskazani, Ethiopia, Somalia, Djibouti, Eritrea, Mauritius, wazungu wa Afrika Kusini, au Zimbabwe, Kenya, pamoja na Mayahudi na Wahindi wazalendo wa Afrika, na makabila yote ya kibinaadamu ambayo yana chimbuko lao Afrika.
Hapana shaka yoyote kuwa Afrika imedhulumiwa na Waafrika weusi bado hawajachukuwa dhamana ya kushiriki kwa machifu na makabila yaliyoshiriki kuwatia utumwani Waafrika wenzao. Haya yameelezwa kwa ufasaha ndani ya kitabu
Zanzibar: Kinyangayiro na Utumwa na mwaka 2009 kimetoka kitabu muhimu chenye kichwa cha maneno
Its Our Turn to Eat (Sasa ni Zamu Yetu Kula) ambacho kinaelezea kwa undani namna ufisadi ulivyokumbatiana na ukabila nchini Kenya.3
Historia yote na kharita (ramani) zenye kulionyesha bara la Afrika kabla halikupewa jina la Afrika huonekana kuwa haina maana. Kwa hiyo kharita za miaka ya 1860 na za nyuma sana kabla ya hapo, zenye kuonyesha eneo la Afrika Mashariki kuwa likijulikana kama ni Ethiopia au mwambao wa Azania au Sudan au Zinjibar huonekana ni dalili tosha za ushahidi wa ubeberu kabla ya Waafrika kujitawala baada ya Wazungu kulipa bara lote jina la Afrika.
Tawi la uafrika ni mtu mweusi lina mzizi mrefu katika kuyakana makabila mengine ya Kiafrika ambayo yaliwasili mwambao wa Afrika hata kabla ya kuwasili Wabantu Pwani ya Afrika ya Mashariki. Anaelezea Profesa Ibrahim Noor Shariff:
Kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa Waafrika wote ni Wabantu na kuwa kila asiyekuwa Mbantu ni mgeni Afrika Mashariki. Ukweli ni kuwa Wabantu ndio katika waliofika Afrika Mashariki, khasa sehemu za Pwani karibuni kabisa. Kwa mfano, Wabantu Wagiriama wamewasili Giriama Kenya kama miaka mia tatu iliyopita. (Soma kitabu cha chifu wao R. G. Ngala kiitwacho Nchi na Desturi za Wagiriama. E. A Literature Bureau. 1949. Ukurasa wa 2).4
Mohamed Said ni msomi wa kwanza kabisa aliyeweza kuweka mkono wake juu ya mpigo wa moyo wa propaganda ya TANU kuhusu suala la Ubantu na wasio Wabantu, yaani, Waislamu. Kwa mujibu wa Mohamed Said:
Katika mwaka 1955, kikundi cha TANU Bantu kiliundwa makhsusi kukabiliana na tatizo la udini kutokana na hisia za baadhi ya Waislam ndani ya TANU. Tangu kuundwa kwa TANU, kulikuwa na hisia ya kupinga Ukristo ndani ya chama. Tatizo hili la udini lilikuwa likichemka pole pole na chini kwa chini ndani ya TANU.
Ilikuwa kazi ya kikundi cha TANU Bantu kuwafichua na kuwapiga vita wanachama wa TANU waliokuwa na hisia kama hizo. Bantu ilifanikiwa sana katika hili hadi kudiriki kupiga marufuku mamkuzi ya Waislam ya Asalaam Alaikum (Amani iwe juu yako) baina ya Waislam kwa msingi kuwa ilikuwa inawabagua Wakristo na hivyo inawatengaMamkuzi yale ya Kiislam yalionekana kama yanakwenda kinyume na imani ya TANU na ilishauriwa kuwa salaam aleikum ipigwe marufuku isitumike. Ikiwa mathalan kwa kusahau Muislam mmoja atatoa salaam kwa Muislam mwenzake, kwa kawaida angejibiwa Alaikum salaam maana yake Amani iwe juu yako pia. Badala ya majibu haya mazuri, majibu yaliyobuniwa na Bantu yalikuwaAhlan tabu maana yakeah tabu tu!5
Lengo la Bantu Pan-Africanism si kuutumikiya uhakika wa historia au kuwapenda Waafrika na kuwachukiya Waarabu, bali ni kulipuuza suala zima la makabila, tamaduni, na staarabu na dini ya Kiisilamu zilizokuwepo Afrika ya Mashariki kabla ya kuwasili kwa Wabantu na khasa kwa Ukristo kutoka Ulaya. Mgeni mmoja kutoka Umoja wa Mataifa aliyekwenda kuitembeleya taasisi ya kihistoria ya kitaifa iliopo Dar es Salaam, alisikitishwa sana kuona historia ya Waarabu Tanzania imeshirikishwa na kitu kimoja tu: utumwa. Wanahistoria na wataalamu wa ilimu ya athari (archaeology) wanashindana na kuukiuka au kuuficha ukweli wowote ule wenye kuonyesha kuwa hakujakuwepo makabila yasiyo ya Kibantu Afrika ya Mashariki kabla ya kuwasili kwa Wabantu.
Ile historia ndefu ya Bahari ya Hindi yenye kuiunganisha Afrika ya Mashariki na ya Kati na Bara Arabu, Uajemi, Bara Hindi, Uchina, Misri, n.k, huwa inaonekana haina maana kwa sababu haikidhi haja na hoja za kisiasa. Au kama itatambulikana itakuwa kujengea hoja kuwa ilikuwa historia ya kibeberu iliyokuwa na kituo chake Zanzibar. Marejeo ya historia ya Afrika ya Mashariki yaliyoandikwa na akina Ibn Battuta, au
Muruj al-Dhahab wa Maadin al Jawhar cha Al-Masudi, au
Kilwa Chronicles iliopo jumba la makumbusho la Uingereza, hayapitiwi na wasomi wengi wa Tanganyika waliojazwa na kujaa chuki dhidi ya makabila mengine yasiyo ya Kibantu ya Afrika ya Mashariki.
Katika utangulizi wa kitabu chao
Mapambano ya Ukombozi Zanzibar, B.F. Mrina na W.T. Matokke wa Chuo Kikuu cha Chama, Kivukoni, wanafafanuwa kuwa: Madhumuni ya kuandika kitabu hiki ni kujaribu kukusanya pamoja
data kwa ajili ya kuweza kufundishia. Jitihada zilizofanywa zilikuwa na lengo la kupata maandishi ambayo yanaweza kutumiwa na walimu na wanafunzi katika Vyuo vya Chama Cha Mapinduzi.6
Pia katika sifa iliyopewa kitabu na kampuni ya uchapaji,
Tanzania Publishing House, ni hii propaganda bila ya kizoro ambayo nainukuu kwa urefu:
CC:
gombesugu Khawarizm wabara Bill Cosby