chabuso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 6,379
- 5,887
hapa umeichanganya historia.waarabu walianza kuja pwani ya east Africa kabla karne ya 5-7 kwa misingi ya biashara na si kuongoza ni kweli yawezekana kulikuwa na watu Zanzibar ila walikuwa wachache nao walitoka bara(sio Tanganyika pekee).mreno alikanyaga pwani ya kilwa karne ya 15 tena mwishoni na alikuta mwarabu akiendesha biashara ikiwemo utumwa katika ukanda huu.pengine unaweza ukajiuliza jambo dogo kwann mwarabu aliitawala sana Zanzibar tofauti na pwani ya bara? jibu ni dogo nani kama la mchangiaji niliyemnukuu visiwa hivi havikuwa na idadi kubwa ya watu hivyo kuwa summon na kuwa rule likawajambo rahisi.utumwa ulichangia kuweka idadi ya weusi kuongezeka ndani ya visiwa hivi.jamii yote ni moja ila imetenganishwa na mazingira.na wareno hawakutawala kwa miaka 500 hilo ni hapana walitawal kwa takriban karne 2 kisha waarabu mwishoni mwa karne ya 18 wakawatoa kwenye miji ya pwani za Zanzibar,kilwa na Mombasa.kwa wakati huo ukoloni haukuwa unatambulika kwenye maskio ya watu weusi na ile dhana ya kuwa weupe ni watu waliobarikiwa iliganda kweny vichwa vya wazee wetu.bado ukweli ni kama ule aliousema ndugu yangu hapo juu watu wa visiwa hivi ni zao la mchanganyiko wa watu wa bara.kuna wanyamwezi wengi tu Zanzibar na sio rahisi kumtambua mpaka akupe mwenyrwe ukweli
Mkuu naona umechanganya historia hapo..viziwa vya zanzibar hata Vasco Dagama amepita kuweka maji na kununu mali nyengine kwenye safari yake ya India,kuwepo na wenyeji kidogo hakufanyi kuwa hakukuwepo na wenyeji katika hivyo visiwa,wareno walishindwa kuweka makaazi katika hiyo miaka 500 kwasababu wenyeji walikuwa hawasikilizani na wareno tafauti kubwa labda dini,sasa ujiulize hawa wenyeji walikuwa wameshakuwa na dini ya kiislam huu Uislam kauleta nani hapo ,hapo ndio linakuja jibu lako kuwa warabu waliwahi kufika zanzibar kabla wareno lakini wao walikuwa wanafanya biashara zao na kupita.
Mwarabu alianza kutawala Kilwa,makao makuu yake yalikuwa kilwa kabla ya kuitwa kuisaida zanzibar kuwaondoa wareno,Kuhusu Watumwa walikuwa wanapita tu zanzibar baada ya kuuzwa kwa mnanda kwenye soko na mkunazini walisafirishwa na kupelekwa nchi za mbali,sioni hii kama inachangia kuwepo kwa watu wengi weusi hapo zanizibar.
Wanyamwezi, waliletwa na mwarabu kwani wanyamwezi walikuwa wafanyakazi wazuri na waaminifu kwa warabu hasa wakati mwarabu anaenda safari za ndani ya afrika kutafuta meno ya temba na watumwa na vitu vyengine
Wamanyema wameletwa na waraabu hili kabila lilipendwa sana na mwarabu wanawake wa kimanyema ndio waliokuwa wameolewa katika koo za kisulatani na wengi wao ndio waliokuwa wakifanya kazi za ndani katika nyumba za sultan
Sasa kuna kabila kama la kizaramo ambao vile vile wako wengi hapo zanzibar,hili kabila unaweza kwenda nyuma zaidi wakati wa Mwinyi Mkuu ambae mwarabu alimuhamisha kutoka shangani na kumepleka Bambi kama sikosei
Kwa matiki hiyo uataona kuwa wenyeji wa zanzibar kama walikuwa kidogo au wingi walikua ni makabila ya pwani ya afrika mashariki wagunya,wazaramo,wadigo,wasegeju.......haya makabila yalikuwa na utamaduni wakulala "dago" wakati wakienda kuvua sehemu za mbali,makabila mengine kama wanyamwezi,wamanyema na makabila ya mbali ya afrika ndio hao waliokuwa wakitwa wageni ijapokuwa walikuwa ni watu weusi...
Waswahili wa zanzibar walienda bega kwa bega na warabu wa Oman watu kama akina TipTip walikuwa waswahili wanafanya vitu sawa sawa na mwarabu na ndio maana wakathubuti kuwaia wawasaidie kumtoa Mreno na ndio maana wakawachia Warabu watawale nchi hii.
Kutoka na historia ya Zanzibar sioni kama Sultan alikuwa mkoloni kama propaganda za siasa zinavyosema,Ukiangalia picha za Sultani wa zanzibar utaona kuwa hawa jamaa ni warabu waliochanganya na watu wa makabila ya waafrika,yaani hawana tafauti kisura na akina Salim Moh'd Salim,Seif Shariff au Aman karume na hizo ndio sura za Visiwani,lamu,Mombasa,kismayu sura za watu wa pwani ya africa mashariki
source bibi yangu 🙂