Makamee
JF-Expert Member
- Nov 29, 2013
- 2,029
- 1,201
- Thread starter
- #41
Naanza kuona wazanzibar kuogopa kitu mlichokidai miongo kadhaa,ila kusema labda mpewe mda mwingine mjiandae hilo siwashauri make ni lazima mkubali kuanza na mda ndo huu,yasafisheni mapito ya bwana ili mfike kanaani salama.
Wahenga wanasema usitukane mamba wakati mto hujauvuka.
Sisi wazanzibar tushawapa Watanganyika kila aina ya majina mabaya,
1.Wakoloni weusi
2.Wanyonyaji
3.Machogo
4.n.k
Lakini tukajisahau hawa nao ni binadamu wenzetu wanaumia kwa ukali wa maneno yetu ambayo ndani yake ilikua na dai moja tu la kutaka Muungano uvunjike.
Kwahiyo tulio wengi hasa viongozi toka Zanzibar tulijaribu kupaza sauti kutaka Zanzibar huru bila kujishughulisha kujua vipi tutaendesha serikali nje ya Muungano.