Wazamiaji wa miaka ya 90

Wazamiaji wa miaka ya 90

Mkuu inchi zinazotoa allowance kubwa kwa raia wake kwa mwezi ni France,,,Italy,,Belgium,, Finland,,Denmark,, Austria,, zingine nimesahau,, ila mfano France,,,ukiwa unafanya kazi unakatwa pesa Fulani kwa mwezi ,,,kwa ajili ya kusaidia kuwalipa wale ambo hawana kazi,,,ukiwa si mfanyakazi wanakula euro 800,,,na wale wanafanya kazi wakistaafu wanakula euro 1300 kwa mwezi,,France wana benefit nyingi sn kwa raia wake,,,mfano ukiwa na mtoto anapewa euro 300 kila mtoto kwa mwezi,,,back to schools,,,kila family itapokea euro 400 kwa kila mtoto kwa ajili ya mtoto kurudi shule,,,,family inapoamua kuhama makazi family itapokea euro 900 kusaidia kuhama kwa watoto 3,,,na ni watoto kuanzia 0 aged to under 20 ,,,mfano mfaransa akiwa jela,,,,atalipwa euro 20 ndani za kujikimu kila mwezi,,, na miezi sita kablahajatoka anaandaliwa mazingira ya kazi huko nje na anaandaliwa nyumba mpya na kodi ya miezi 3 analipiwa akitoka anafikia kwenye nyumba hiyo kama Hana pa kwenda.....
Duuuuuuuuh walllah npo tayar kufia huko France, lazima nizamie hukoooh
 
Kuna rafiki yangu mmoja, kati ya mwishoni mwa miakaya 90 na mwanzoni mwa mwaka wa 2000 alizamia kwenda Ulaya. Safari za kipindi hicho ilikuwa za kibabe kweli mtu anaanza safari hana hata passport. Safari ilimpeleka mpaka Libya lengo ni kwamba ilikuwa aingie Morroco then wavushwe kuelekea Spain.

Katika safari hiyo alikutana na majanga mengi sana sana. Amenusurika kufa zaidi ya mara 20 tena akiwa ameshaona kaburi.

Sasa anadai akiwa Libya, anadai walibya ni wabaguzi sana hasa kwa Waafrika wenzao weusi. Anadai ukipanda usafiri wa umma wanawake walikuwa wanaziba pua. Anasema muda mwingine ulikuwa ukipita mtaani unaona mama anaokota jiwe anampa mwanae akurushie.

Anadai sasa kimbembe uje ukutane na vijana walikuwa wanajiita Aska Boys (sina hakika kama nimewapatia). Anasema walikuwa wanatabia wanakuja na magari wanakuweka mtu kati, wanafungua boot wanatoa marungu, watakupiga mpaka ufe.

Sasa anasema akiwa Libya, alikuwa hana pesa kabisa na kutoka Libya ili uvushwe uende Morocco mpaka upande boat kuendelea na safari, ilikuwa inahitajika pesa nyingi. Yeye kwa muda huo aliikuwa ashageuka kuwa kama chokoraa. Na kipindi hicho mauaji kwa wageni yakawa yameongezeka.

Anadai katika kundi lao allikuwepo jamaa katoka Ethiopia ni Muorthodox alikuwa akisali sana sana. Jamaa akamfuata akamwambia amsaidie pesa kidogo ili aweze kuondoka pale maana wenzake walikuwa wengi wao wana mpango wa kuondoka baada ya hali kuwa mbaya.

Jamaa eti akamuuliza, huna mtu anayeweza kukutumia pesa. Jamaa akamwambia sina ila kuna kaka yangu ana pesa nyingi sana ila hawezi kunipatia pesa maana hata hii safari nimeianza kwa kumkumbia yeye alikuwa anataka kuniua. Jamaa akamwambia, usiku njoo nikufanyie maombi, lakini iwe saa tisa usiku.

Kweli usiku wa saa tisa akaenda, eti jamaa akachora chora mviringo sakafuni akamwambia aingie kati, kisha wakaanza kumuombea yeye na wenzake.

Baada ya maombi akamwambia asubuhi kampigie simu kaka yako, mwambie akutumie dollar 2000, atakutumia. Usipunguze na wala usiongeze. Jamaa anadai kesho yake akaenda sehemu ya kupiga simu akampigia simu kaka yake, alipomueleza hakubisha kabisa ila akamwambia atamtumiaje ile pesa.

Kipindi hicho anasema Libya kulikuwa hakuna huduma za Western Union, wala Money Gram. Anadai watu walipokuwa wakitaka kupokea pesa, kulikuwa na mzungu raia wa Spain pale ana ofisi iko kisiwa cha Lampedusa, hivyo pesa inatumwa kwenda Lampedusa, akiconfirm imefika kule unaenda kwake anakupa cash pale Libya.

Basi jamaa akawa ametumiwa pesa akaondoka pale. Japo huko mbele alipata majanga mengine.

Jamaa alifanikiwa fika Mexico, Equador na huko pia alipata majanga hadi akapoteza korodani baada ya kuanguka mikononi mwa drug dealers.

Mmhhh huyo baharia wako amezamia miaka ya 2000?? Mie nakumbua real "STOROWAY" (STOWAWAY) walikuwa miaka ya 70's-80's.
 
Kubaniwa pua na wamama wa Libya ndiyo kutaka kuuwawa?
 
Mmhhh huyo baharia wako amezamia miaka ya 2000?? Mie nakumbua real "STOROWAY" (STOWAWAY) walikuwa miaka ya 70's-80's.
Alianza safari yake mwaka 96 na ametua Tanzania mwaka 2004 napo alikuwa depoted to Kenya from South Korea
 
Mkuu inchi zinazotoa allowance kubwa kwa raia wake kwa mwezi ni France,,,Italy,,Belgium,, Finland,,Denmark,, Austria,, zingine nimesahau,, ila mfano France,,,ukiwa unafanya kazi unakatwa pesa Fulani kwa mwezi ,,,kwa ajili ya kusaidia kuwalipa wale ambo hawana kazi,,,ukiwa si mfanyakazi wanakula euro 800,,,na wale wanafanya kazi wakistaafu wanakula euro 1300 kwa mwezi,,France wana benefit nyingi sn kwa raia wake,,,mfano ukiwa na mtoto anapewa euro 300 kila mtoto kwa mwezi,,,back to schools,,,kila family itapokea euro 400 kwa kila mtoto kwa ajili ya mtoto kurudi shule,,,,family inapoamua kuhama makazi family itapokea euro 900 kusaidia kuhama kwa watoto 3,,,na ni watoto kuanzia 0 aged to under 20 ,,,mfano mfaransa akiwa jela,,,,atalipwa euro 20 ndani za kujikimu kila mwezi,,, na miezi sita kablahajatoka anaandaliwa mazingira ya kazi huko nje na anaandaliwa nyumba mpya na kodi ya miezi 3 analipiwa akitoka anafikia kwenye nyumba hiyo kama Hana pa kwenda.....
inaonekana france kuna bata balaa sasa balotel nn kinamshnda mpaka anasema anataka kurud africa na atacheza ligi za africa
 
Mkuu sikutaka kukaa ulaya,,,nikuwa Italy na Spain mwaka 2015 /2016 nikarudi bongo,,nikaenda tena Swiss nikawa France 2019 kwahyo mm sikutaka kukaa kule,,,sababu ya shughuli zangu,,,.now nipo kwenye mandonga,,,,
mandonga ndo nn mzee
 
Si kila inchi ulaya inalipa pesa,,,ndy maana watu wanatafuta inchi nzr ya kujipiga,,,ili upate benefit baadae,,,mfano,.France,, Belgium,, Italy,,Finland,,Denmark,, Austria,,Sweden,,Greece,,swiss,, nk..kila ichi ina benefit zake kwa raia zake,,huwa hazifanani...lakini hizo inchi zinatoa pesa kwa raia,,na hata migrants

Vipi kuhusu nchi ya Canada
 
Huu uzi ungekuwa mzuri kama ndugu mhamasishaji wa mambele huko angekuja kutoa vitu vyake no matter what please mzee pita hapa Parabora
 
  • Thanks
Reactions: amu
Mkuu hebu elezea kidogo maisha ya turkey yapoje?yaan hii nchi natamani sana kufika
Mkuu Mimi nilikaa kama miezi sita hivi,, pale maisha yanategemea kufanya kazi viwandani mfano viwanda vya nguo,,,nk,,au kuhangaika mitaani,

,ni inchi nzr kwa raia,,lakini kwa wageni ni ngumu kidogo,,, maana kuna migrants wengi wakitokea Syria,, hata Egypt kwa njia za panya,,,pesa ,,, strong hazipishani sana na dola.,,,,,,

pale nilishindwa sababu ya haraka zangu,,nikaelekea Greece,,

sababu sikuwa na viza ya Greece,,, nilikuwa na viza ya Turkey tu,,na Turkey sio inchi ya shengen ,,,ikanibidi nijiunge na migrants wanaokwenda Greece kwa njia za panya,,

Zilikuwa njia mbili za kuingia Greece,,baharini au kupitia mtoni,,,
zote ni dola 500 kila migrants mmoja,,,
nikachaguwa njia ya kuvuka mto,,
niliona ndy salama zaidi,,

Turkey ipo border na Bulgaria,, na Greece,,upande fulani,,kuna mji unaitwa Izmir,,, upo close to Greece,,,tofauti yake ni mto tu,,,

Tulifungiwa kwenye fuso moja tukiwa kama migrants 100 hivi,,,
tulitembea usiku kwa usiku toka Istanbul hadi Izmir kuanzia saa mbili usiku hadi saa sita usiku tukafika lzmir,,,

ilikuwa winter time hatari,,jinsi nilivyo vaa ni kama begi zima lipo mwilini mwangu.,,,nilikuwa nimevaa jeans tatu na track suit ndani,,na fulana tatu ,sweater na koti kubwa la ngozi,na soksi ya kuzuia baridi juu,,still bado baridi hatari.

Baada ya kufunguliwa mlango wa fuso,,,
ilikuwa baridi haswa,,
eneo lote lilikuwa jeupe kwa theluji,,,
basi haraka haraka tukaambiwa tuiname chini,,,,
pale pale wale wa Turkey wenye connection za kutuvusha,,,wakatoa boat ya kujaza kwa upepo,,
wakaijaza pale baada ya kama nusu saa wakaiweka mtoni,,ulikuwa mto wa upana kama wa mita 50 hivi,,,huo mto unatenganisha Turkey na Greece,, na huwa unalindwa pande zote wakati wa summer time,,
lakini unakuwa haulindwi wakati wa winter time...kwahyo winter ndy watu wanakatisha hapo,,basi nikaingia kwenye boat,,ikapigwa kasia hadi upande wa greece ni kama dk 10 tu nipo upande wa Greece,,,

Baada ya kumaliza kutuvusha,,tukaanza safari kuitafuta mjini,,,tulipewa maelekezo na wale jamaa kwamba tufate maandishi ya kigiriki,,,
maana maandishi ya kigiriki na maandishi ya Bulgaria ni tofauti lakini yanafanana sana,,so tufate barabara ambayo inaelekeza maandishi ya kigiriki,,,tukifata tofauti tutakuwa mikononi mwa askari wa Bulgaria,,
na wakasema lazima tukamatwe na police wa kigiriki,, ili watupeleke vituoni,,
tusipokamatwa tutatembea umbali mrefu sn kwa miguu,,,
tusihofu tukiona police,,,

basi tulitembea kuanzia saa nane usiku hadi saa mbili asubuhi,,, tukaanza kukamatwa kwa makundi na kupelekwa kituoni,,ule mji nimesahau kidogo,,, baada ya muda wakatupeleka camp,,,nika complain kama raia wa somalia,,baada ya week mbili za pale camp,,,
nikatolewa nikapelekwa kuna mji mmoja unaitwa ethlonic hapo tukapandishwa train,,,
wakatwambiya you are free to go,,,

Mwandende nikaingia Athens au Athena,,,
huo ndy ulikuwa mwanzo wangu wa kuingia ulaya,,,2011.,.hivyo tu mkuu,,,ktk harakati za mbongo,..
 
Back
Top Bottom