Hili somo la utafutaji kwa vijana wetu inawezekana tulipeleke mashuleni kuanzia darasa la tatu mpaka la saba na sekondari mpaka vyuo vikuu liwepo pia. Ni wakati sasa wa vijana kufundishwa maisha sio Tanzania au Mtwara na Mbeya pekee bali wanaweza kujitafutia maisha popote pale duniani kuanzia Afghanistan, Pakistan, China, Congo DRC, Israeli, Madagascar, Comoro, Yemen, USA, Norway, Brunei, Jamaica nk huko kila mahala kuna fursa zake twendeni tukahangaike tuzikomboe familia zetu na jamii ya Kitanzania kiujumla.