Wazamiaji kiholela Afrika Kusini warudishwa

Wazamiaji kiholela Afrika Kusini warudishwa

Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini ina mkataba wa kubadilishana wahamiaji haramu.Kwa hiyo mara nyingi huwa ni nchi husika kulipia gharama za wahamiaji kuwarudisha kwao.Sisi pia hugharamia Wasomali,Waethiopia na wengine kuwarudisha makwao.Usihofu,kamdhamini nduguyo
Shukrani kwa taarifa.
 
Mimi ninachokiona hapo sio wazamiaji haramu,ninawaona watafutaji au tuseme wapambanaji...hiyo inaitwa ajali kazini.
Kabisa Ni watafutaji cheki wanavyokula Ni walivyotakata wenyewe afya Safi yaani Kuna huyo dogo hapo mbele nimemkubali mpambanaji kako fit tu kanajiamini
 
Unapokuwa nchi za ugenini usiwekeze sana na hata pesa yako usiweke kwenye bank zao ili siku kikinuka usipoteze kila kitu

Jr[emoji769]
 
Hapa ndipo nawapenda wanigeria .Mhamiaji haramu mnigeria ukimpa repatriation ukagonga passport yake PI yaani prohibited immigrant kwenye yako akifika tu Nigeria airport anaenda immigration moja kwa moja anaenda jaza kuomba passport ingine kuwa hiyo Ina doa la kugongwa PI .Anapewa pole na kupewa passport ingine aendelee na safari zake za kusaka fursa kokote Duniani

Nigeria wameachia hivyo kupunguza tatizo la ajira nchini mwao .Sisi tukamaa na vitu vidogo Kama hivi

Hii safi sana.
 
Unapokuwa nchi za ugenini usiwekeze sana na hata pesa yako usiweke kwenye bank zao ili siku kikinuka usipoteze kila kitu

Jr[emoji769]
Ajali kazini tu hiyo.Huwexi kwenda ukawrkeza kidogo wakati nguvu unayo .Na unajua ndilo eneo la kutokea.Hiyo Ni ajali tu kazini
 
Ni vyema tukaanzisha zoezi la kugawa passport bure kwa kila kijana aliyefikisha miaka 18 na kutoa ruhusa vijana waende kokote kule duniani kujitafutia maisha iwe kwa VISA FEKI, VISA HARALI cha msingi wafike tu huko waendako, hii inaweza kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wetu hapa bongo maana duniani hapa kuna nchi fursa ziko bwerere na hakuna watu.

Zipo nchi duniani hapa unatakiwa upenye ufike tu, ukishaingia tu kazi zipo na malipo mazuri ni ukakamavu wako tu. Kijana mmoja akitoboa huko ughaibuni anaweza kuvuta vijana wenzie hata watano, Cha muhimu tutoe elimu vijana wetu wapendane na kuthaminiana, lakini pia tuhakikisha vijana wengi wanapata elimu kwa wingi ili wakitokomea huko wasishangae shangae.
 
Kuna haja ya kutengeneza mkakati vijana wa kitanzania watapakae duniani kote na tuwe na muingiliano mkubwa na jamii nyingi duniani. Hili linaweza kutengeneza fursa nyingi kwa watanzania, maana wengi wakitoboa maisha watasaidia ndugu na jamaa huku na kuwekeza huku kiasi cha kutoa ajira nyingi kwa wenzao kwenye haya mapoli yaliyojaa yasiyo na kazi.
 
Unapokuwa nchi za ugenini usiwekeze sana na hata pesa yako usiweke kwenye bank zao ili siku kikinuka usipoteze kila kitu

Jr[emoji769]
Huwa nawaambia vijana,ugenini hatuweki pesa bank,unakuwa na Account ili udhaminike,lkn sio kuwekea pesa.Maana likitokea la kutokea pesa zote unaacha.Ugenini unakaa na pesa ndani,tena iwe kwenye mfumo wa dola!Ukiharibu unachanganya kongoro zako kurudi home
 
Back
Top Bottom