Watu 4 Wapandishwa Kizimbani Wakituhimiwa Kuisababishia TRA Hasara ya Sh. Milioni 592

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,044
49,727
Pamoja na kuongoza genge la uhalifi,wanashitakiwa pia Kwa kuchapisha risiti fake za EFD

=======

DSM; WAKAZI wanne wa Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, wakikabiliwa na mashitaka sita ikiwemo kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya Sh milioni 592.3 na utakatishaji fedha.
-
Washitakiwa hao ni Salum Mbegu (38) Mkazi wa Majohe Mji mpya, Peter Ntikula (27) Mkazi wa Buguruni, Baraka Ntikula (37) Mkazi wa Mkuranga na Hamad Hamad.
-
Washitakiwa hao walisomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Gloria Mwenda akisaidiana na Upendo Mono, Medalakini Emmanuel na Hauni Chilamula mbele ya Hakimu Mfawidhi, Susan Kihawa.
-
Mwenda amedai washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kuongoza genge la uhalifu, kutumia mashine za kielektroniki za EFD kwa lengo la kuharibu mfumo na kumdanganya Kamishina, kutoa risiti zisizo halali za EFD, kukutwa na mali iliyoibwa au kupatikana kinyume na sheria, kuisababishia mamlaka hiyo hasara na kutakatisha fedha.
-
Imeandaliwa na Francisca Emmanuel, Habari Leo
 
...Waongee TU na DPP, watamalizana...!!!
 
Back
Top Bottom