Wazamiaji kiholela Afrika Kusini warudishwa

Wazamiaji kiholela Afrika Kusini warudishwa

Haramu kwa kwa Nani kwa Afrika ya kusini au kwa Tanzania? Kama Ni wahamiaji haramu Afrika ya kusini wewe Tanzania wamekukosea Nini? Kule Kuna Sheria zao na jela zao na mahakamani zao wewe yanakuhusu Nini?
Wameondoka nchini bila kufuata utaratibu hilo ni kosa.
 
Hapa ndipo nawapenda wanigeria .Mhamiaji haramu mnigeria ukimpa repatriation ukagonga passport yake PI yaani prohibited immigrant kwenye akifika tu Nigeria airport anaenda immigration moja kwa moja anaenda jaza kuomba passport ingine kuwa hiyo Ina doa la kugongwa PI .Anapewa pole na kupewa passport ingine aendelee na safari zake za kusaka fursa kokote Duniani

Nigeria wameachia hivyo kupunguza tatizo la ajira nchini mwao .Sisi tukamaa na vitu vidogo Kama hivi
Nigeria 🇳🇬 ni watu wajanja sana , Uchumi wao unaendeshwa na diasporas naona hata Kenya walishagundua hilo sasa hivi. Maisha ni kokote hii mipaka tumewekewa na wazungu tu ila ridhiki ya mtu haina mipaka.
 
Eee Bwana wee! Asante kwa taarifa Mshana Jr. Pongezi ziende kwa Rais Magufuli! Hawa jamaa walikuwa wanaishi huko SA maisha hatarishi ya kuidhalilisha nchi! Nawafahamu wengi walikuwa wanalala chini ya nguzo za barabara za juu (flyover) na kwenye makaravati wanaendesha maisha yanayodhalilisha utu na taifa letu. Hata nauli ya kurudi walikuwa hawana hata kurudi hawataki kwasababu ya aibu na kuingia SA kinyume cha utaratibu. Vijana komaa nchini mwenu! Haya mambo ya kuzamia nchi za watu bila utaratibu matokeo yake haya!
Unawafahamu? Mbona wamependeza kuliko wewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida wanayokabiliana nayo vijana hawa wakishafika huko,ni kwamba yale matarajio walitotegemea kupata inakuwa tofauti hivyo wanajikuta njia panda..nirudi nyumbani (nitachekwa)...option wanayobaki nayo ni kuendelea kuteseka na kulala mabarabarani
Uliwaona huko mabarbarani? Usiongee vitu usivyovijua. Barabara za South Africa unazifahamu????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba tuwakane sawa ndugu zangu hawa vijana waliorudishwa wamepewa case inayoitwa "IMMIGRATION CASE" ambayo inawahusu wale wote ambao wanaishi bila vibali maalum vya South Africa ambao wanawaita "ILLEGAL IMMIGRANTS" sasa unakuta mtu kaingia S.A na passport na kama inavyojulikana Watanzania tunaingia kwa FREE VISA ila tunapewa miezi 3 ambazo ni 90days ila sasa hivi border nyingi za S.A hawatoi hizi siku 90 unakuta mtu unapewa siku 7 au mwezi 1 hapo ndipo swala la "OVER STAY" linakuja unakuta kijana kashaingia hana tena mpango na passport yake atakaa hata miaka 5 bila ya kukamatwa na kuulizwa kuhusu document yake ila siku kukiwa OPERATION ya POLICE na HOME AFFAIRS (IMMIGRATION OFFICERS) ndio inaweza ikawa bahati mbaya kwako ukakamatwa na hata kama wakikukamata unao uwezo wa kujikatia tiketi yako ya ndege na kurudi kwenu na bila ya hivyo ndio utajikuta unapelekwa Camp ambayo inajulikana kwa jina la LINDELA hii ni camp ya REFUGEE wote wanaokamatwa na IMMIGRATION OFFICERS wa S.A mtawekwa hapo kwa muda wa miezi 4(120Days) mpaka mtakapojaa ndio Balozi atakuja kuwapeni karatasi za ku_sign ili muweze kurudishwa nchini kwenu na ndege ya umoja wa mataifa (UN) na ambayo ni free na hapo pia kuna hela mnahitajika mpewe ila hilo swala watu ukishafika hapa huwezi kupewa pesa bali wewe ndio utakae wapa wao pesa ambayo ni Elfu50 au Jela. Ila na hapo pia kipindi unaingia South Africa unao uwezo wa kwenda HOME AFFAIRS DEPARTMENT na ku_apply REFUGEE PAPER(ASYLUM SEEKER) na wanakupa muda wa kuishi nchini kwao kwa miezi mitatu halafu urudi tena HOME AFFAIRS kwa ajili ya kuongeza tena siku na inaenda miezi mitatu hlf sita hlf mwaka na baadae unapewa ya miaka3 na mpaka hatua ya Refugee I.D na hatua ya mwisho Citizenship sasa vijana wengi tuna_fail kwenye ufatiliaji wa kuishi kihalali na tatizo letu kubwa ni ELIMU NDOGO na DHARAU mwisho wa siku mtu unajikutua upo bongo nimeshaona watu wakirudishwa na nishakua nawatembelea sana kwenye hiyo CAMP (LINDELA) kwahyo tusidanganyane kuhusu hao vijana na kwenda kuwadhamini hawawezi kukwambia ulipe gharama za ndege na tukumbuke kuna wengine hapo wametokea jela kutumikia vifungo vyao ila document ya kuishi pale ishakua expired kwahyo ni lazima arudishwe nchini kwake na SERIKALI YA TANZANIA haichangiii chochote kwenye kuwarudisha bali ni UMOJA WA MATAIFA (UN) ndio wanaotoa gharama zote
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewahukumu Watanzania 30 waliozamia nchini Afrika Kusini na kurudishwa nchini, baada ya kukiri na kutiwa hatiani kwa mashitaka ya kuondoka nchini kinyume cha sheria za uhamiaji.

Washitakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo jana, walisomewa mashitaka hayo kwa mahakimu wawili tofauti.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mbando, aliwahukumu wazamiaji 16 kutumikia kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 300,000 kila mmoja baada ya kukiri mashitaka yao.

Washitakiwa hao ni Omar Kaulu, Dominic Fabric, Sefu Mohammed, Hamad Hashiri, Asbawi Omar, Abdallah Hamad, Razan Ally, Moosa Salimu, Mawki Ally, Daniel Joshua, Amari Abduli, Abdullah Ramadhan, Mohammed Tuwa, Aziz Mohammed, Rajabu Shamanism na Adam Seifu.

Alisema kutokana na makosa hayo kujirudia, kila mshitakiwa atatakiwa kutumikia kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 300,000.

Kabla ya kutolewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Godfrey Ngwijo, aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washitakiwa kwa sababu utaratibu wa kutoka nje ya nchi unafahamika.

Washitakiwa hao kwa nyakati tofauti waliomba mahakama iwapunguzie adhabu kwa sababu wamekaa sana gerezani walipokuwa Afrika Kusini na kwamba wameikosea Serikali ya Tanzania pamoja na serikali waliyotoka hivyo wapewe onyo na kupunguziwa adhabu.

Awali, akisoma mashitaka Ngwijo alidai washitakiwa hao walitoka nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume cha kanuni za uhamiaji namba 20 (3) (a) G.N namba 657 ya mwaka 1997 inayosomwa pamoja na kifungu namba 48 (2) ya Sheria ya Uhamiaji namba 54 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.

Alidai Januari 21, mwaka huu maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), washitakiwa hao wakiwa raia wa Tanzania walikutwa wakiwa wametoka nje ya nchi bila kufuata utaratibu wa kutoka nchini kwenda Afrika Kusini kwa kupitia mipaka inayojulikana.

Washitakiwa wote walikubali mashitaka hayo na upande wa mashitaka uliwasomea maelezo ya awali, ambapo ulidai tarehe zisizofahamika washtakiwa kwa nyakati tofauti walitoka Tanzania na kuingia Afrika Kusini bila kufuata taratibu.

Ngwijo alidai washitakiwa walikamatwa nchini Afrika Kusini na kuletwa Tanzania na kwamba walifikishwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na na kasha kupelekwa Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuchukuliwa maelezo.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally, aliwahukumu washitakiwa 14 kutumikia kifungo cha miezi 18 jela au kulipa faini ya Sh 50,000 kila mmoja, baada ya kukiri kosa hilo.

Washitakiwa hao ni Adam Luzz, Suleiman Saidi, Kapaya Fredric, Semboko Abubakari, Mambosasa Francis, Juma Mhina, Chale Othoman, Salehe Iddy, Mohammed Kassim, Hassan Ally, Boban Abed, Abdul Kessy, John Joseph na Mawazo Frank.

Baadhi ya washitakiwa wamelipa faini na kuondoka mahakamani hapo pamoja na ndugu zao. Hata hivyo, wakati washitakiwa hao walipofikishwa mahakamani baadhi ya wazazi walidai watoto wao walindoka nchini bila kuwaaga na wengine walilalamika watoto wao kubadili majina.

Chanzo: Habari Leo
 
Harakati za kupambana na maisha/kutafuta maisha ndio zinapelekea watu kuwa wazamiaji kwenye nchi nyingine.

Nadhani pia vigezo na masharti vya kutoka nchi A kwenda kuishi nchi B vinabana na vina gharama kubwa ndio maana wanaona bora wazamie.

Bora hizo fine zimekuwa ndogo, mtihani uliopo sasa ni wanaanzaje kupambana na maisha ya Tz ikiwa kila walichokitafuta pengine wamekiacha huko huko SA. Inakatisha tamaa lakini ila ndio maisha.
 
Back
Top Bottom