mmh, kono kono na kaa kipi bora?,
nikikuambia Pweza anatia kinyaa hata kuona kuliko kono kono utabisha? Mbona hushangai wala panya na wala mbwa hapa hapa tanzania?, mbona haushangai wala popo na wala panzi (senene na nzige)?
Kwa taarifa yako hakuna kiumbe mwenye nyama asieliwa! Ila huwa nashangaa wala kuku maana ni kiumbe wa ajabu mwenye kichwa kibaya, mdomo mbaya na ana macho yasiyokua na ushirikiano kutazama! Hahah
Hawa jamaa wanakula konokono.Wanachemsha na kunywa supu,kwakuwa konokono wapo kwenye vijumba wanatumia stiki(vijiti) wanachomoa na kutupia mdomoni. Yaani ukitafakari unaweza tapika! Makala ya watu hawa ilikuwa inaoneshwa Startv leo mchana.
mmh, kono kono na kaa kipi bora?,
nikikuambia Pweza anatia kinyaa hata kuona kuliko kono kono utabisha? Mbona hushangai wala panya na wala mbwa hapa hapa tanzania?, mbona haushangai wala popo na wala panzi (senene na nzige)?
Kwa taarifa yako hakuna kiumbe mwenye nyama asieliwa! Ila huwa nashangaa wala kuku maana ni kiumbe wa ajabu mwenye kichwa kibaya, mdomo mbaya na ana macho yasiyokua na ushirikiano kutazama! Hahah
Mueleze kuwa watu wanakula ruba na mafunza ya kwenye magogo yalooza, itakuwa konokono!
Tena konokono mtamu kama nini with garlic source .............:A S-confused1:
Ndiyo nini hiyo?
Mchuzi wa Vitunguu Swaumu. Ndiyo maana midomo ya Wayahudi...... teteteteee....
Alaaa kumbe!
Mami wewe ushawahi kula mapaja ya chura?
Ndiyo nini hiyo?
Vitu "tofauti" ambavyo nimesha kula:
- Konokono, frog leg, swallows nest, shark fin, farasi (restaurent)
- nyoka, mamba, wide viriety of caterpilars (dried or smoked)
including hao alio wataja Gaijin hapo juu (in local communities, kazini)
Mengine yanayo onekana ya kawaida kwetu ila yanachefua wageni:
- pweza, senene, mchwa na cricket (home)
Nilipewa ila nilishindwa kula:
- nyani, mbwa, paka, fukwe, panya wa kawaida/rat and mouse,
guinea pig, Panya buku/ field mouse, caterpilars (fresh)
Nina rafiki wengi hawawezi kabisa kupika kuku akiwa mzima mzima, hata wale wa supermarket. Lazima wawe wamekatwa katwa ndio waweze kuwapika. Wanona huruma, wengine wanachefuka.Kuna dada mmoja alikuja Bongo akaona kuku anavyochinjwa...laana la leo kuku hamli.
Pezi la papa, nyangumi, mkunga, pweza, ngisi, kaa, mayai mabichi ya samaki na vyenginevyo vya pwani nishakula sana na kusema ukweli ninavipenda
Nyama ya farasi, ngamia, mamba, mbuni, njiwa, konokono, vijidudu vyenye mbawa......nimewahi lakini sina uzoefu navyo
Chura, nyoka, panya, paka, mbwa bado na nia sina lakini siapi, siku moja inaweza tokea
Sasa yeye anaona tunakosea, kula mnyama tulie "mzowea", sio?Kuna watu mbuzi wanawafuga kama pets na wakisikia sisi kwetu mbuzi ni bonge la kitoweo hawaamini na wanatuona tuko wakatili sana.
Kuna wakati mmoja nilienda vijijini (majuu) kutafuta mbuzi. Nikakutana na mdada mmoka akaniambia kwao wana mbuzi mmoja. Nikamwomba aniuzie akakataa akasema ni 'family pet'. Aliponiuliza kwa nini ninatafuta mbuzi, nikamwambia nataka nikamchinje halafu nimchome.
Bi dada wa watu almanusra azimie.
Sasa yeye anaona tunakosea, kula mnyama tulie "mzowea", sio?
bora sisi tuna heshimu vinyama. huko kwao farming is so cruel!
calfs wanazaliwa na kuchinjwa bila kutembea, kupreserve nyama iwe laini
wanapewa antibiotics ili wasipate magonjwa (because they live too confined)
yani kuku, n'gombe, nguruwe, kondoo, wanapakizwa midawa wakati hawaumwi!
Nikiangalia utaratibu wa farming ulaya naona ni bora mtu awe zake vegetarian
bora huku kwetu nakula kuku, nilimuona akitotoka, akikua, na hadi namla najua anatoka wapi!
Making Hay: Investigations