Wawekezaji wasaidie kujenga miundombinu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Viwanda vikubwa vinahitaji
1. Umeme mwingi na wa uhakika
2. Reli imara
3. Bandari kubwa zenye miundombinu ya kisasa
4. Wananchi wengi wenye uwezo wa kununua na kutumia bidhaa za viwanda hivyo.

Sasa hivi uwekezaji mkubwa nchibi unatoka nchi za China, Uingereza, Kenya, South Afrika, uturuki,.......

Tanzania, watanzania, mabalozi wetu, tuwaombe watu hawa wanaowekeza nchini kwetu watusaidie katika ujenzi wa miundombinu yetu hii hata kwa makubaliano ya kuwapunguzia kodi kwa muda fulani kama sehemu ya kurejesha gharama zao hizo.Yaani tuwaombe wawe kama wamelipa kodi kabla ya kuuza. Tusidanganyane, Waziri Mpango hana hela ya kutosha kuijenga miundombinu yote hii kwa hela zetu wenyewe kwa speed tunayoitaka sisi. Miundo mbinu hii ijengwe kwanza kwa kuzingatia tu maeneo ya uzalishaji mkubwa na masoko makubwa ya bidhaa hizo.

Hela ya Waziri Mpango itumike zaidi katika kuongeza uwezo wa wananchi katika kufanya manunuzi ya bidhaa zitakazozalishwa na viwanda hivyo kama vile kuinua kilimo, masoko, uvuvi, ufugaji, mishahara ya watumishi wake.

Mabenki yetu yawe na uwezo wa kukopesha wananchi wanaopenda kununua bidhaa zitakazozalishwa na viwanda hivyo kwa riba ndogo sana kama wanavyofanya nchi za viwanda. Nchi zote za viwanda watumishi wake wanalipwa vizuri sana na mabenki yanatoa mikopo ya bei nafuu kwa wananchi ili waweze kununua bidhaa za viwanda vyao. Bila kufanya hivyo tunaweza kupigania viwanda viwepo lakini vitakavyoshindwa kuhimili ushindani kwa masoko, ubora na bei za bidhaa.
 
Mabeberu wawajengee miundombinu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wenzenu wanafanya hivyo, wanakulipa kodi kabla na kuipeleka kwenye uwekezaji wa miundombinu. Lakini hii itawezakana Tu kama ukiwa na watu wasiofikiria negative kama wewe.
Utaamini pale utakapoona kiwanda kimezalisha tiles nyingi zilizorundikana kwenye maghala bila kufika sokoni au kukosa wanunuzi au umeme hakuna.
 
Back
Top Bottom