Nina shaka na maono ya viongozi wa sasa kuhusiana na dhima ya ujenzi mkubwa wa Miundombinu nchini kama kwamba inarudisha kwenye zama za Utumwa na kutawaliwa.
Nakumbuka maono (Vision) ya rais Marehemu Magufuli aliweka juhudi kubwa katika Ujenzi wa Miundombinu hii sambamba na ujenzi wa Viwanda nchi kiasi kwamba aliwaalika hata matajiri wakubwa wa ndani kina Dangote, Bakhresa, Rostam, Aboud na wengineo katika mazao ya kilimo na madini kuwekeza katika viwanda ili kukuza uchumi wa ndani wakati Serikali yake imejikita katika kuboresha miundombinu nchini.
Hoja yangu ipo hapa – Viongozi wa leo wote toka rais aliyepo madarakani mpaka kina Kitila, Zitto na wachumi wataalam wengine wanazungumzia ujenzi huu mkubwa wa Bandari zetu na reli (Ushoroba) kwenda nchi jirani za DRC, Burundi na Rwanda kana kwamba haya ni Maendeleo tunayoyahitaji lakini deep down najiuliza sisi (Tanzania) tutasafirisha nini ikiwa dhima yake ni Usafiri wa bidhaa za nchi jirani kwankutegemea kodi na Ushuru?
Hivi, wafaidika wa uwekezaji huu mkubwa watakuwa kina nani? Je, haitakuwa nchi hizo na makampuni ya nje wakichukua nafasi ya utawala wa zama za Utumwa na hawa viongozi wetu watatumiwa kama Machief wa zamani enzi za Ukoloni. Tegemeo lao (Machief) na letu ni kutoza Kodi na Ushuru exactly kama walivyofanya kina Mtemi Mirambo!
Wakati ule wa Utumwa Bandari zetu za Mombasa, Bagamoyo, Zanzibar na Kilwa zilukuwa ngome za Wakoloni zikitumiwa kuchukua bidhaa toka Bara ikiwa ni pamoja na Watumwa, Pembe za ndofu dhahabu na kadhalika, wao wakituletea sisi shanga, nguo na viatu.
Hata Utawala wa Mjarumani na Muingereza nao walidai Pwani ya Afrika Mashariki kutoka kwa Sultan wa Zanzibar wakajenga miundombinu ya bandari na reli ili waweze kusafirisha bidhaa za ndani kutoka tawala zao kwenda makwao kwa maendeleo ya nchi zao.
Mjarumani hakujenga reli mpaka DRC, Burundi na Rwanda kwa sababu hayakuwa makoloni yake ategemee kodi na Ushuru.
Muingereza vile vile japokuwa tulikuwa na EAC alijenga miundombinu Kenya na Uganda zaidi zikiwa ndani ya koloni lake kwa sababu lengo ni kuvuna walichopanda sio kunufaisha nchi nyinginezo kwa kukusanya kodi na Ushuru.
Maoni hata ya viongozi wangu yanafikiriaha san, mimi nilitegemea uwekezaji huu mkubwa ni kwa ajili yetu sisi ili kukuza Uchumi wetu wa viwanda vya ndani tupate kuuza bidhaa zetu nje, lakini naona kama tuna facilitate control na mahitaji ya nchi jirani na za Magharibi?
Matajiri wakubwa wanatukimbia, wanawekeza nchi jirani kwa sababu mikataba yao ina nafuu kuliko sisi. Dangote, Rostam na wengine wanazitazama nchi jirani kama bora na nafuu kwao katika uwekezaji wa viwanda kuliko Tanzania. Tumefikaje hapa!
Hii itakuwa Biashara ya kuwafadhili kina Tippu Tip.