Watumishi wasiopenda ilani ya CCM waondoke

Watumishi wasiopenda ilani ya CCM waondoke

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Musoma. Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amewataka watumishi wa umma wasiopenda ilani ya Chama cha Mapinduzi kuacha kazi mara moja kwakuwa kufanyakazi ya umma huku wakichukia ilani hiyo ni kupoteza muda.

Byabato ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Februari 26, 2021 wakati akizungumza na watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Mara juu ya mikakati ya kufanikisha majukumu ya watumishi hao.

Amesema kuwa mtumishi wa umma anayechukia ilani ya CCM na chama chenyewe anajidanganya kwakuwa anatakiwa kutekeleza ilani hiyo ambayo ndiyo dira ya kufanya kazi yake kwa ufanisi.

Amesema kuwa hata yeye kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa mtumishi wa umma na alikuwa akipenda ilani ya CCM pamoja na chama chenyewe baada ya kubaini kuwa haiwezekani kutenganisha ilani hiyo na utumishi wa umma.

"Kama kuna mtumishi haipendi ilani ya CCM anajidanganya na niwatake tu waache kazi kwavile watatukwamisha kwenye utekelezaji wa ilani hiyo tuliyoinadi kwa nguvu zote na kukubaliwa kisha ikapokelewa na hatimaye ikapigiwa kura na wananchi" amesema Byabato.

Ametolea mfano wa mwanafunzi mwenye imani tofauti ambaye anasoma shule ambayo sio ya imani yake lakini ni lazima afuate sheria na taratibu za shule anayosoma huku akisema kuwa hakuna sababu ya kukwamisha kazi kwasababu ya kuchukia ilani hiyo ambayo ndiyo dira yao.

"Haiwezekani usiende msikitini wakati unasoma shule ya Kiislamu eti kwasababu wewe sio Muislam kama hauwezi ni vema ukahama kwenye shule hiyo tofauti na hapo lazima ufuate sheria na taratibu za pale" amesema.

Ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kuboresha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kujamii ili kufanikisha hilo ni lazima ilani ya CCM ifuatwe na Serikali haitakuwa na huruma kwa atakayejaribu kukwamisha utekelezaji huo.

Amesema kuwa ili kufanikiwa kutekeleza majukumu ya kiutumishi wafanyakazi hao hawanabudi kupenda kazi zao huku akifafanua kuwa ni vigumu kufanikiwa kwenye utumishi kama mtumishi atakuwa hapendi kazi yake.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa huyu mbona anaongea tofauti na mwenyekiti wake,mwenyekiti anasema hawakuchaguliwa sasa ilani ilikubalika vipi na kupigiwa kura!
 
Tuache kazi kwani alitusomesha yeye? Au alitutafutia hizo kazi yeye? Ilani ya ccm ndiyo takataka gani? Wangekuwa wanatawala kwa haki wangechukiwa na nani?

Wanaendesha nchi kwa misingi ya ubaguzi, uonevu, dhuluma, unafiki na kila aina ya ujanja ujanja halafu wategemee kupendwa na watumishi wa umma! Wametufanyia nini ndani ya miaka sita sasa zaidi ya mateso?

Akafie mbali huko.
 
Wafanyakazi hawakuajiriwa kwa ilani ta ccm. wana job description na mikataba ambayo wali sign.
hakuna mahali kwenye job decription waliandikiwa wafuate ilani.

wafanyakazi waendelee kufanya kazi kwa kufuata job decription na sheria za nchi
 
wafanyakazi hawakuajiriwa kwa ilani ta ccm. wana job description na mikataba ambayo wali sign.
hakuna mahali kwenye job decription waliandikiwa wafuate ilani.

wafanyakazi waendelee kufanya kazi kwa kufuata job decription na sheria za nchi
Well said.
Hawa wapambe wanajipendekeza kwa jiwe kuu mpaka wanabaribu.
 
Ilani ya ccm ipo kwa miaka 5 tu.
Lakini watumishi wa umma wapo kwa miaka 60.
Kamuulizeni kama analifahamu hilo?

Wakipata madaraka, hulewa. Imbecile!!
Ndugu watu wenye mandate ya kuendesha nchi ni chama tawala; jukumu la civil servant m ni ku-implement namna sahihi ya kuitekeleza ilani yao.

Ndio maana nimemuelewa Magufuli kumteua Dr Bashiru kama katibu mkuu kiongozi; civil servant don’t understand their obligations na chama kilichopo madarakani.

Kwa mtazamo huo nadhani you should know who is the imbecile.
 
....Ukiwa unasoma shule ya Kiislamu lazima uende Msikitini?

Hivi wanafunzi Wakristo pale chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro wanalazimishwa kwenda Msikitini vinginevyo waache chuo?
Au Waziri anataka kuchafua taasisi za dini fulani kwa vile yeye si muumini wake?
 
Wafanyakazi hawakuajiriwa kwa ilani ta ccm. wana job description na mikataba ambayo wali sign.
hakuna mahali kwenye job decription waliandikiwa wafuate ilani.

wafanyakazi waendelee kufanya kazi kwa kufuata job decription na sheria za nchi
Huyo waziri nadiriki kusema kabisa HANA AKILI
 
Maendeleo yana Chama
Ndugu Zangu
Hapa Dar es Salaam
Palichelewa Sana Huwezi Kumpa Chakula Mtoto Wa Jirani, Utampa Wa Kwako
Nafurahi Sana Dar es Salaam Imenizalia Mtoto
Wote Ni Ccm Jiji Linapendeza Sana Ndugu Zangu.
😅😄😃🤣😂😁😀
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Back
Top Bottom