Mtu yeyote atakayekuja anaungana na sisi kwenye madai ya katiba huyo tuko pamoja naye, kama anazungumza lugha moja na Wananchi na Watanzania huyo tuko pamoja naye, "Bw. John Heche - Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA
Mtangazaji:
"Hivi karibuni tumesikia mara kadhaa wana CCM wakisema kwamba swala la Katiba si ajenda ya CHADEMA, ni ajenda yao. Lakini nanyi mlikuwa mkisisitiza kwamba mnataka Katiba Mpya, wanasema na wao pia wanataka Katiba Mpya. Hii ina maana gani hasa kwenu?"
John Heche:
"Kama wanataka Katiba kwa nini haiji? Kwa sababu wao ndio wamejimilikisha dola na kila kitu, wao ndio wana Bunge lao, wao ndio wana Rais, wao ndio wana madiwani wote, wao ndio wanaosimamia fedha za nchi hii, wao ndio wanaoweza kupeleka mswada Bungeni, wao ndio wanapeleka bajeti Bungeni. Kama wanataka Katiba, kwa nini bajeti ya mwaka huu haijaweka kifungu cha kuanza kuandika Katiba?"
Mtangazaji:
"Sura yake kwenye Ilani yao ipo."
John Heche:
"Tunataka Katiba kwenye Ilani au actual Katiba? Sisi tunataka Katiba halisi, sio maneno ya kwenye Ilani. Ilani yao hata ya Magufuli ilikuwa na hiyo. Magufuli anapoingia madarakani mwaka 2015 kwa mara ya kwanza, miaka 10 iliyopita, kulikuwa na kifungu kwenye Ilani ya CCM kilichokuwa kinataka Katiba. Imekuja? Leo ni mwaka wa 11, imekuja?
Kwahiyo nani anayekwamisha Katiba kama wanataka Katiba? CCM ndio tatizo kwa sababu ndio inanufaika na Katiba hii. Na juzi, ukitaka kujua hawataki Katiba, Emmanuel Nchimbi ambaye ni Katibu Mkuu wa chama chao/serikali yao hiyo, aliposema Katiba Mpya, umeona alivyotukana na wana CCM? Ametoka sijui Mwenyekiti wa Vijana amemtukana. Wewe unaamini kwamba Mwenyekiti wa Vijana yule anaweza kumtukana Emmanuel Nchimbi bila baraka za aliye juu yake?
Kiongozi sijui Mwenyekiti wa Vijana wao amemkemea Nchimbi. Sijui nani wamemkemea, wajumbe wa NEC wamemkemea. Kama wanataka Katiba, Nchimbi amesema tuandike Katiba... Sasa ni kipi kibaya hapo kama kweli wanataka Katiba? Kwa nini wamkoromee?"
Mtangazaji:
"Kwahiyo CHADEMA inamuunga mkono Katibu Mkuu?"
John Heche:
"Sasa tumuunge mkono... tunaunga mkono... Nisikilize, mtu yeyote atakayekuja anafanana na sisi kwenye madai ya Katiba, huyo tuko pamoja naye. Kama anazungumza lugha moja na wananchi wa Tanzania, huyo tuko pamoja naye."