The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,508
- 46,717
Nimezungumza na mmoja wa watumishi wa mashirika ya kimataifa (one of UN agencies) huko Zanzibar jana usiku na kitu kimoja cha kunishtua kuwa alikuwa anasubiria "roll call'. Nilipomdadisi akasema kuwa siku hiizi baadhi ya mashirika ya kimataifa na hata ya ndani yameanza kuwataka wafanyakazi wao kutembea na radio call na ikifika majira ya jioni basi wanatakiwa ku 'call in' kucheck kuwa wapo salama... na pia mkubwa wao kuita radios za watumishi kuhakikisha wanajibu.. mfanyakazi ambaye katika muda husika hawezi kupatikana kwenye radio call yake husababisha msako...
Kweli Zanzibar imefika hapo...? Kuna wengine wenye experiences kama hii au ni one of the 'isolated cases" hizi?
Sijui sehemu nyingine lakini kwa hao jamaa wa UN Zanzibar huo ni utaratibu wao. Lazima wajaribu kama Radiocall zao zinafanya kazi vizuri ili hata kama kuna dharura imetokea na simu za mkononi hazifanyi kazi, wanaweza kuwasiliana kikamilifu na kwa uhakika. Lengo hapo ni kuhakikisha ufanisi wa mawasiliano.