Watumishi wa umma, wanasiasa na wafanyabiashara wanaiba na wataendelea kuiba kwa sababu tajiri Tanzania hafungwi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Ripoti ya CAG itaendelea kuwa Stori zisizo na funzo lolote Kwa Sababu wezi wamegundua kwamba ukiwa na pesa hakuna wakukuchukulia hatua.

Wanasiasa wote walioiba na waliobambikiwa kesi wapo uraia na wananchi wanampongoza awamu ya sita Kwa kuwaachia matajiri; lakini tujiulize NI maskini gani ameachiwa Kwa majadiliano? Kwanza Nani wakukuruhusu ukanyage red carpet kama umechoka?

Naandika huu ukweli kumaanisha kwamba si Bunge wala serikali watakashinikiza mwizi tajiri afungwe. Kelele zinazoendelea bungeni si za Leo, maisha haya yakukwapua yanaanzia Kwa watunga sheria.

Wapo wabunge wanalipwa posho Bila kuwepo kwenye vikao; wapo wabunge wanalipwa posho mara mbili mbili na naamini hata Leo hii wapo waliosaini posho mbili maeneo tofauti.

Unategemea huyu MTU anayemwibia mwananchi ndiye ashinikize mwizi akamatwe?

Lakini tujiulize kuna mkubwa gani asiyetokana na ukoo wa mkubwa? Watu wote wanateuliwa kutokana na connection; kama wapo watoa connection wanakosekana vipi wazima Shari?

Leo akionekana kwenye wezi yupo mtoto wa kigogo unadhani kuna uchunguzi utafanyika? Wajanja wote nchini wanaiba Kwa network na kwenye network Wana make sure yupo kigogo au ndugu ya kigogo; chunguza ufukuzwe kazi .Kamata ukamatwe. Hii ni dhambi iliyozalishwa na makuzi yetu. Hatujazaliwa Kula vya Haki tumezaliwa Kula vyakunyonga.

Hebu jiulize Mwanasheria Mkuu WA serikali anapotetea wanasiasa wapite Bila kupingwa anamtetea mwananchi? Huu ni mfano mdogo kwamba jamii yetu haitaki kuishi Kwa Haki, watu wanawaza ustawi WA familia zao siyo familia zetu.

Unaiba milioni Mia unakaa ndani miezi then unahukumiwa kulipa milioni tano, Nani ambaye ataogopa kufanya biashara yenye faida kubwa kiasi hiki?

Maskini wa Tanzania tafteni pesa hakuna tajiri mfungwa.
 
Hivi kazi kubwa ya TAKUKURU si ni kuzuia na kupambana na rushwa inakuwaje taasisi ya umma yenye wafanyakazi wanaolipwa mishahara kwa kodi za wananchi ipo na haizuii hizo rushwa zisitolewe kwenye nchi kama role au dhima yake ya kwanza ambayo iko kwenye mandate yao.Tukisema hii taasisi haina tija kwa nchi na walipa kodi wa nchi hii kwa kushindwa kuzuia huo wizi usitokee tutakuwa tunakosea?
 
Mtumishi wa Umma ukipata Nafasi IBA Sana. Kikokotoo kitakutoa Roho ukiStaafu. Waibe wajilipe Pensheni Yao wasijekufa Uzeeni Kwa Sonono. Nusu Bajeti tumieni Nyingine Mgawane. Safari Nje na Ndani Kwa Sana, Semina na Warsha msiache kupanga na kuhudhuria.
 
Nimeipenda hiyo sentence yako ya mwisho, tutafute fedha wakuu, KATIBA mpya ni muhimu maana itatupatia PP atakayetusaidia kutuletea utawala bora, kwa sasa ni shamba la bibi wa wote, ndio maana nchi imegubikwa na human trafficking syndicates, money laundering syndicates, drugs etc etc na ukiona wapopo wapo kwa wingi ujue kuna upigaji mkubwa wa pesa, TISS huu msala unaishia mlangoni kwenu, amkeni guy's
 
Mkuu hawo wafanyakazi wa serekali wanaoiba niwa central government hawa wa local government ukijaribu jela ninakuhusu
 
Nimeipenda hiyo sentence yako ya mwisho, tutafute fedha wakuu, KATIBA mpya ni muhimu maana itatupatia PP atakayetusaidia kutuletea utawala bora, kwa sasa ni shamba la bibi wa wote, ndio maana nchi imegubikwa na human trafficking syndicates, money laundering syndicates, drugs etc etc na ukiona wapopo wapo kwa wingi ujue kuna upigaji mkubwa wa pesa, TISS huu msala unaishia mlangoni kwenu, amkeni guy's
Amkeni Guys ! That’s a good advice to the good people I suppose !!!!
 
Jibu.

Katika dunia hii usipopambana masikini utabakia na umasikini na tajiri ataendelea kuwa tajiri....Vitabu vya kidini vinathibitisha hilo (Biblical theory)
 
Hivi kazi kubwa ya TAKUKURU si ni kuzuia na kupambana na rushwa inakuwaje taasisi ya umma yenye wafanyakazi wanaolipwa mishahara kwa kodi za wananchi ipo na haizuii hizo rushwa zisitolewe kwenye nchi kama role au dhima yake ya kwanza ambayo iko kwenye mandate yao.Tukisema hii taasisi haina tija kwa nchi na walipa kodi wa nchi hii kwa kushindwa kuzuia huo wizi usitokee tutakuwa tunakosea?
Hii ndiyo taasisi ya hovyo kabisa kuwahi kutokea
 
Ripoti ya CAG itaendelea kuwa Stori zisizo na funzo lolote Kwa Sababu wezi wamegundua kwamba ukiwa na pesa hakuna wakukuchukulia hatua.

Wanasiasa wote walioiba na waliobambikiwa kesi wapo uraia na wananchi wanampongoza awamu ya sita Kwa kuwaachia matajiri; lakini tujiulize NI maskini gani ameachiwa Kwa majadiliano? Kwanza Nani wakukuruhusu ukanyage red carpet kama umechoka?

Naandika huu ukweli kumaanisha kwamba si Bunge wala serikali watakashinikiza mwizi tajiri afungwe. Kelele zinazoendelea bungeni si za Leo, maisha haya yakukwapua yanaanzia Kwa watunga sheria.

Wapo wabunge wanalipwa posho Bila kuwepo kwenye vikao; wapo wabunge wanalipwa posho mara mbili mbili na naamini hata Leo hii wapo waliosaini posho mbili maeneo tofauti.

Unategemea huyu MTU anayemwibia mwananchi ndiye ashinikize mwizi akamatwe?

Lakini tujiulize kuna mkubwa gani asiyetokana na ukoo wa mkubwa? Watu wote wanateuliwa kutokana na connection; kama wapo watoa connection wanakosekana vipi wazima Shari?

Leo akionekana kwenye wezi yupo mtoto wa kigogo unadhani kuna uchunguzi utafanyika? Wajanja wote nchini wanaiba Kwa network na kwenye network Wana make sure yupo kigogo au ndugu ya kigogo; chunguza ufukuzwe kazi .Kamata ukamatwe. Hii ni dhambi iliyozalishwa na makuzi yetu. Hatujazaliwa Kula vya Haki tumezaliwa Kula vyakunyonga.

Hebu jiulize Mwanasheria Mkuu WA serikali anapotetea wanasiasa wapite Bila kupingwa anamtetea mwananchi? Huu ni mfano mdogo kwamba jamii yetu haitaki kuishi Kwa Haki, watu wanawaza ustawi WA familia zao siyo familia zetu.

Unaiba milioni Mia unakaa ndani miezi then unahukumiwa kulipa milioni tano, Nani ambaye ataogopa kufanya biashara yenye faida kubwa kiasi hiki?

Maskini wa Tanzania tafteni pesa hakuna tajiri mfungwa.
Na wataendelea kuiba sana kufidia muda wa wizi waliyopoteza awamu ya 5. Mama katoa kila ishara yeye kupiga hela ya umma ruksa. Eti uibe utosheke au ushibe. Yeye anasubiri watu watosheke kuiba😂😎
 
Hii ndiyo taasisi ya hovyo kabisa kuwahi kutokea
Hii TAKUKURU ni heri isiwepo kwani uwepo wake hauna tija ni upuuzi kuwa na hao TAKUKURU halafu maafisa wake wanalipwa mishahara kila mwezi halafu ubadhirifu wa fedha za umma uendelee kutamalaki mpaka Mh Rais wanamsababishia dhambi ya kuitukana hiyo mijizi stupid halafu wenyewe huko maofisini wapo tu wanamchora mama.Kama kirefu cha TAKUKURU ni taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa je wamewahi zuia lini kila mwaka report ya CAG inakuja na mafekenye ya upigaji wa kutisha
 
TAKUKURU huwa inawateja wake VEO, WEO, walimu na manesi
 
Back
Top Bottom