Watumishi wa Umma kupunguza Ufanisi wa kazi kwa sababu ya nafasi za kisiasa?

SUTAGI-

Senior Member
Nov 9, 2018
195
376
Maslahi ya mtu mmoja mmoja yana nguvu kubwa kuliko uzalendo katika kumhamasisha mtu kufanya kazi. Ni sababu mbili kuu Kati ya hizi au zote kwa pamoja zilizowasukuma wengi kwenda kuchukua fomu za Ubunge

Ndiyo maana tumeshuhudia Wakuu wa mikoa, Wakurugenzi na Watumishi wengine wakiacha kazi hizo na kwenda kutafuta Ubunge ambao hata hawajui kama watafanikiwa kupenya nyavu.

Je, hili linaathiri vipi ufanisi Wafanyakazi wengine hususani Watumishi wa umma?

Mosi watumishi wa umma wataanza kujihami kutafuta Maisha mazuri kama wenzao waliobahatika kuingia kwenye nafasi za kisiasa, watataka watembelee magari ya kifahari na kuishi nyumba nzuri nk.

Katika kufikia lengo hilo wataanza kufanya kazi za nje ya majukumu ya ajira kama Biashara, kilimo ufugaji n.k, suala hili litawapunguzia concentration kwenye kazi za kiutumishi wa umma na kupunguza ufanisi.

Pili wapo watakaoacha kazi za utumishi kutokana shughuli zao nyingine kuwalipa vizuri zaidi ya ajira zao.

Tatu tutatengeneza kizazi ambacho kitakuwa na muelekeo wa kupata pesa hata kwa njia za rushwa au udanganyifu bila kuangalia madhara yanayoweza kuwakuta.

Nini kifanyike?
Kwa kipindi Cha Magufuli kinachoisha tumeona picha tofauti kidogo na zamani ambapo Wanasiasa waliopo serikalini wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii hasahasa Mawaziri kwa umoja wao. Hili linatakiwa liendelezwe awamu ijayo.

Wabunge wawajibike kwa majukumu yao na wafanye kazi kwa ufanisi ili mishahara na posho wanazopata ziendane na uhalisia wa kazi yao.

Mfano wa Wabunge katika Bunge lililopita ambao hatukuwa na taarifa rasmi za wapi walipo lakini hawaonekani katika shughuli hizo ni pamoja na Mheshimiwa Nimrodi Mkono na Prof. Muhongo. Hawa wawili wanawakilisha sehemu ya Wabunge wengine ambao uwakilishi wao Bungeni unatiliwa shaka kutokana na kutokuonekana na wananchi kutokuwa na taarifa rasmi ya sababu za kutokuonekana kwao (huenda Spika alikuwa na taarifa rasmi lakini Wananchi hawakupewa taarifa hizo)

Mfano mwingine ni Mh. Joshua Nassari, huyu alitoweka Bungeni na kwenda Masomoni bila hata ruhusa Wala taarifa kwa Spika wa Bunge na aliwajibishwa baadae sana, Je kipindi hicho chote alichokuwa nje ya Bunge si aliendelea kupata mshahara wake? Posho nk?

Kwanini watumishi wengine wa serikali wakikosa kwenye vituo vyao vya kazi ndani ya siku Tatu bila taarifa wanaweza hata kufukuzwa kazi? Je haya siyo matabaka? Haya mambo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili watumishi kupitia nafasi za kisiasa na wale wa kawaida wawe na miongozo inayofanana.

Mwaka fulani Bungeni Mh. Peter Serukamba alitoa maneno machafu kwa Mbunge mwingine wa CDM bungeni "F..u..c..k.. y..o..u." lakini sikuona hatua zozote za kinidhamu alizochukiliwa na endapo angekuwa ni Mwalimu katoa kauli hiyo kwa Mwalimu mwenzie hali ingekuwa tofauti kabisa.
 

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,486
2,377
Tuache kulia lia. Tuendelee kupambana ,hatimae kutakucha tuu kitaeleweka. Ukweli utajuweka wazi wenyewe na watu watajuwa kuwa wanaongopewa na kulaghaiwa na ccm.

Hapo ndipo watakapomtafuta commander wa kuongozi mapambano wamkose ndio watajua kuwa walifanya makosa kumtenga Mbowe na Maalim Seif na wapambanaji wengine.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom