Kiama kwa wezi wa Fedha za umma kinakuja, Rais Samia hataki kulemba

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,137
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Wezi wa Fedha za umma kaeni mkao wa tahadhari.

Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Dr.Mwigulu Nchemba,Serikali imesema inaandaa mswaada wa sheria kwa ajili ya kuwashughulikia wezi wa Fedha za umma.

Kwenye sheria mpya wezi/wazembe wa Fedha za umma si tuu kwamba watakuwa wanaondolewa kwenye vyeo vyao bali watashushwa na mishahara yao tofauti na awali ambapo watendaji walishushwa vyeo huku mishahara yao ikibakia palepale.

Kwa hili Samia ameonyesha yuko serious na kupambana na wezi,wazembe na wanaopanga kukwamisha ufanisi wa serikali yake.

Hongera Sana SSH kwa kuupiga mwingi,Kazi iendelee.

-----
Katika kuongeza uwajibikaji, Serikali imetangaza kuwachukulia hatua kali watumishi wa umma wanaochezea fedha za miradi ya maendeleo.

Onyo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba alipozungumzia mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, akisisitiza kuwa hakuna mradi utakaosimama kutokana na uzembe wa mtu mmoja au kikundi kidogo kinachousimamia.

“Watakaokiuka utaratibu uliowekwa, wataendelea kunyofolewa serikalini na tayari hatua zimeshaanza kuchukuliwa na zitaendelea kuchukuliwa,” alisema Dk Mwigulu.

Hatua za sasa, alisema zitahusisha za kinidhamu na kisheria kwa watu wanaokwamisha miradi inayowalenga wananchi wengi, badala yake wanazikwepesha fedha zilizotengwa kwa manufaa binafsi.

Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, kwamba mtumishi aliyebainika kuhusika na upotevu wa fedha za umma alikuwa anaondolewa kwenye nafasi yake lakini mshahara wake hauguswi, alisema Serikali inakusudia kubadilisha sheria ili kila anayeharibu awe anajipunguzia na mshahara wake pia.

“Tegeni macho na masikio yenu, mtawaona. Wataondolewa mmojammoja. Wapo waliokuwa wanaondolewa kwenye vyeo baada ya kuvurunda mambo lakini wanaendelea kulipwa mishahara ya awali, sheria hiyo inafanyiwa kazi ili kuwaadhibu kadri inavyotakiwa.

Hatua za kisheria na kinidhamu zitaendelea kuchukuliwa kwa watu wote watakaofanya uzembe katika usimamizi wa fedha za umma,” alisema.

Wengine walioonywa katika utekelezaji wa majukumu yao, waziri alisema ni wale wanaoisababishia halmashauri kupata hati chafu ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) lakini ilikuwa ikiadhibiwa halmashauri kwa kupunguziwa fedha za maendeleo, lakini mabadiliko yanayokuja yatawagusa waliosababisha hali hiyo huku miradi ya wananchi ikiendelea kutekelezwa.

Hata halmashauri ambazo zilikuwa zinapelekewa fedha za miradi lakini hazizitumii na mwisho wa siku zinazirudisha Hazina, alisema watendaji wakae macho kwa kuwa pia wataondolewa.

“Popote utakapobainika mchezo mchafu, Wizara ya Fedha na Tamisemi tunashirikiana kuandaa ripoti na kutoa mapendekezo ya hatua za kuwachukulia watu wanaohusika katika udanganyifu huo. Rais amesema watakaosababisha uchafu ndio watakaoondoka,” alisema Dk Mwigulu.

Matokeo chanya
Kuhusu utendaji wa Serikali kwa mwaka mmoja uliopita, Dk Mwiguli alisema hatua za kisera zilizochukuliwa zimekuwa na matokeo mazuri yaliyosaidia kuimarisha sekta ya fedha nchini.

Licha ya changamoto ya janga la Uviko-19 na vita vilivyoathiri uchumi wa dunia, alisema mikopo chechefu ilipungua kutoka wastani wa asilimia nane mpaka asilimia tatu kutokana na uamuzi wa Serikali kulipa madeni ya wazabuni, makandarasi na watoa huduma kwenye taasisi za umma.

Ulipaji wa madeni hayo, alisema umewawezesha wengi kulipa mikopo benki na wafanyabiashara walikochukua malighafi za kutekeleza miradi waliyoshinda zabuni.

Pamoja na hilo, alisema mzunguko wa fedha umeongezeka kwa asilimia 9.2 kutokana na mambo kadhaa yaliyofanywa, ukiwamo mkopo wa Sh1.3 trilioni kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) zilizotumika kujenga shule 12,000 kwa kuwatumia makandarasi wa ndani.

Mpaka Februari, alisema Serikali ilikusanya Sh15.9 trilioni kutoka vyanzo vya ndani, sawa na asilimia 93 ya matarajio, hivyo kuiwezesha kutekeleza miradi ya maendeleo na ile ya kimkakati.

Waziri pia alizungumzia kasi ya ongezeko la mfumuko wa bei kwamba unasababishwa na vitu vilivyo nje ya udhibiti wa Serikali na unaigusa dunia nzima, hivyo kupandisha gharama za maisha.

“Kwa kiwango kikubwa, mfumuko wa bei haujatokana na tatizo la kisera wala uamuzi wa kiutawala au uzembe, bali majanga ya dunia. Yanapotokea majanga haya hatutakiwi kunyoosheana vidole, ila kumwomba Mwenyezi Mungu kuyaondoa,” alisema.

Alisema Tanzania inaagiza bidhaa nyingi, hasa za viwandani, kutoka nje ambako gharama za uzalishaji zimeongezeka kabla hazijasafirishwa kuingizwa nchini na kisha zipelekwe mikoani.

“Rais ameona tuelimishane kwanza wakati tukiangalia mwenendo wa kupanda kwa bei mpaka Juni kuangalia hatua za kikodi tunazoweza kuchukua,” alisema.

Mabwawa ya umwagiliaji
Katika kuhakikisha majanga ya dunia hayaleti athari kubwa nchini, Mwigulu alisema katika bajeti ijayo, nguvu imeelekezwa kuimarisha sekta ya kilimo kwa kujenga mabwawa ya umwagiliaji katika kila halmashauri.

Alisema Serikali imeshatoa fedha za kununua mtambo wa kuchimba visima kwa kila mkoa na kutakuwa na mtambo wa kuchimba mabwawa ya umwagiliaji kwa kila mkoa.

Mitambo hiyo inatarajiwa kukuza kipato cha wakulima na kuajiri vijana wengi watakaokuwa wanavuna zaidi ya mara moja.

“Kila mkoa pia utakuwa na mtambo wa kupima maji ili kuepuka kuchimba kisima au bwawa sehemu isiyokuwa na maji ya kutosha. Kutakuwa na skimu nyingi za umwagiliaji. Benki pia zitakuwa na dirisha maalumu la mikopo ya kilimo,” alisisitiza.

Chanzo: Mwananchi
 
Hamna kitu mkuu hali itabaki ile ile tulio maofisini tunajua NI ngumu Sana hamuwezi kudhibiti hasa mhasibu zikiwa zinaiva na boss...pesa lazima ipigwe tu na ma auditors wakija wapewe bahasha zao.

Tanzania hii ya kuwa na mahakama ya mafisadi lakini mashauri yaliyoamuliwa na wahusika kuadhibiwa hayafahamiki hayazidi 10.

Angalia mtu kaiba mafuta kigamboni toka pipes za bandarini lakini mpk leo kimya hajulikani na hamna kesi.
 
Hamna kitu mkuu hali itabaki ile ile tulio maofisini tunajua NI ngumu Sana hamuwezi kudhibiti hasa mhasibu zikiwa zinaiva na boss...pesa lazima ipigwe tu na ma auditors wakija wapewe bahasha zao...
Hivi kwenye mtu ni mkuu wa kitengo anavurunda unamhamisha au kumshusha cheo lakini salary inabakia vilevile,wewe unaona ni sawa?

Hicho ndicho sheria inaenda kubadilisha,maana tuliwahi sikia unamtumbua DED afu anabakia kulipwa pesa kama ya awali,huu ujinga ndio unaenda kukomeshwa.
 
Hamna kitu mkuu hali itabaki ile ile tulio maofisini tunajua NI ngumu Sana hamuwezi kudhibiti hasa mhasibu zikiwa zinaiva na boss...pesa lazima ipigwe tu na ma auditors wakija wapewe bahasha zao...
Tena kuna ile tani 1 ya dawa za kulevya zilikamatwa na wanajeshi huko baharini walikuwa wapakistani kwenye boti ikapelekwa mahakamani kesi hiyo umesikia?
 
Hamna kitu mkuu hali itabaki ile ile tulio maofisini tunajua NI ngumu Sana hamuwezi kudhibiti hasa mhasibu zikiwa zinaiva na boss...pesa lazima ipigwe tu na ma auditors wakija wapewe bahasha zao.

Tanzania hii ya kuwa na mahakama ya mafisadi lakini mashauri yaliyoamuliwa na wahusika kuadhibiwa hayafahamiki hayazidi 10.

Angalia mtu kaiba mafuta kigamboni toka pipes za bandarini lakini mpk leo kimya hajulikani na hamna kesi.[ tuwache kusifia saana
 
tena kuna ile tani 1 ya dawa za kulevya zilikamatwa na wanajeshi huko baharini walikuwa wapakistani kwenye boti ikapelekwa mahakamani kesi hiyo umesikia?
Hamna kitu Tanzania NI shamba la Bibi milele na milele
 
Hivi kwenye mtu ni mkuu wa kitengo anavurunda unamhamisha au kumshusha cheo lakini salary inabakia vilevile,wewe unaona ni sawa?

Hicho ndicho sheria inaenda kubadilisha,maana tuliwahi sikia unamtumbua DED afu anabakia kulipwa pesa kama ya awali,huu ujinga ndio unaenda kukomeshwa.
Kwenye hili, Serikali ipo sahihi. Kwa ujumla sheria hiyo imechelewa.
 
Upuuzi mtupu, ccm hii au??

ccm ni nzuri akipatikana rais kama jpm utaona raha sana. fikiri jpm angemaliza miaka 10 mambo mengi mazuri tungeyapata. hakuna chama kingine kinaweza kutawala tanzania kuliko ccm.

Hao wengine ni vyama vya mitandaoni na matusi kama yote ukiwapa mkoa tu kuutawala mkoa mzima wanakufa na njaa na hakuna huduma watakayopata sembuse uwape watawale tanzania nzima
 
ccm ni nzuri akipatikana rais kama jpm utaona raha sana. fikiri jpm angemaliza miaka 10 mambo mengi mazuri tungeyapata. hakuna chama kingine kinaweza kutawala tanzania kuliko ccm. hao wengine ni vyama vya mitandaoni na matusi kama yote ukiwapa mkoa tu kuutawala mkoa mzima wanakufa na njaa na hakuna huduma watakayopata sembuse uwape watawale tanzania nzima
Huyo JPM wako alikuwa wapi kufanya haya anayofanya Samia?

Alikuwa wapi kufikisha wezi mahakamani?
 
Back
Top Bottom