Watumishi wa umma wakiwemo walimu, simamieni HAKI katika chaguzi zijazo 2024&2025.

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
17,704
27,186
Salaam, shalom!!

Leo ni mei mosi, siku pekee na muhimu Kwa wafanyakazi Nchini.

Watumishi wa umma wanasherehekea mei mosi katika mazingira magumu, mishahara isiyotosheleza, Kodi kubwa, kukosa motivation wakiwa kazini mf walimu ,kikokotoo Kwa wastaafu, mfumuko wa Bei, nk nk.

Kwa kuwa Sheria za Nchi zimekataza watumishi wa umma kujiingiza kushabikia siasa za vyama,

Kwa kuwa matatizo yote yanayowakabili Wananchi na watumishi wa umma wakiwemo ni ya kimfumo na yanatokana na SANDUKU LA KURA,

Na Kwa kuwa chaguzi zijazo 2024&2025 walimu Kwa kiasi kikubwa na watumishi wengine wa umma polisi nk nk watahusika kusimamia uandikishaji wa wapiga kura na usimamizi wa uchaguzi wenyewe 2024 na 2025, ni Rai yetu sote Watanzania kusimamia Haki katika chaguzi zetu sawasawa na matakwa ya Katiba na Sheria zilizopo.

Kamwe, watumishi wa umma tusichukue upande wowote kisiasa, tutende HAKI, chama kikishindwa Kwa kukataliwa na wananchi , Si KAZI yetu kukisaidia kisianguke, Nchi ni ya vyama vingi, chama chochote kinaweza kuongoza Watanzania Kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi.

ANGALIZO: Tumewaalika Malaika Toka Mbinguni wenye panga zikatao kuwili kuwa waangalizi wa ziada wa chaguzi zetu Ili HAKI itawale juu ya nchi katika kuwapata viongozi wa Nchi.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Mungu wabariki walimu na watumishi wa umma Kwa ujumla wao.

Ahsanteni, na karibuni🙏
 
Ni ngumu sana kupata uchaguzi wa Haki kama msimamizi Mkuu wa uchaguzi wilaya ni Mkurugenzi (aliyechaguliwa na Rais), waandikishaji wa uchaguzi huo ni waalimu (Bosi wao ni Mkurugenz wa Halmashauri). Kwa mfumo huo Kamwe hatuwezi kupata UCHAGUZI ulio na Haki katika hii Nchi.
 
Ni ngumu sana kupata uchaguzi wa Haki kama msimamizi Mkuu wa uchaguzi wilaya ni Mkurugenzi (aliyechaguliwa na Rais), waandikishaji wa uchaguzi huo ni waalimu (Bosi wao ni Mkurugenz wa Halmashauri). Kwa mfumo huo Kamwe hatuwezi kupata UCHAGUZI ulio na Haki katika hii Nchi.
Lakini ni UKWELI Ulio wazi kuwa mkurugenzi hateuliwi na CCM Bali Rais aliyewekwa na Katiba na Sheria zilizopo za nchi.

Yapo majimbo mengi tu wamewahi kuongoza upinzani Kwa kutangazwa washindi na wakurugenzi Hawa Hawa uwaitao ni watumishi wa Rais.
 
Back
Top Bottom