Watumishi wa Idara ya Elimu (Sekondari) Wilaya ya Ulanga wanafanya kazi kwa mazoea

Amaizing Mimi

JF-Expert Member
Feb 2, 2019
477
1,066
Habarini za muda huu ndugu zangu,

Malalamiko yangu ni kwa Idara ya Elimu Sekondari katika wilaya ya Ulanga. Hawa jamaa sijui ni uzembe au kujisahau katika majukumu yao.

Kumekuwa na utofauti wa ulipwaji stahiki mbalimbali kati ya idara ya msingi na sekondari. Mfano, suala la ulipaji nauli za likizo kwa watumishi.

Idara ya Msingi huwa wanalipa muda muafaka kuliko Idara ya Sekondari. Mfano, nauli ya likizo ya mwezi wa 12 mwaka jana, Idara ya Msingi walilipwa mwezi ule ule wa 12 lakini Idara ya Sekondari hadi leo hawajalipwa.

Lakini pia, nauli ya likizo ya mwezi huu wa 6 Idara ya Msingi wameshalipwa lakini Idara ya Sekondari hata hawaeleweki.

Naomba waache kufanya kazi kwa mazoea.
 
Public bureaucracy is inefficiency mkuu. Hakuna ushindani so tegemea Huduma mbovu kwa hao Incompetents Education Officers.


It's non profit . Over
 
Idara ya elimu ilishajifia siku nyingi sana, tunasubiri tangazo tu majengo tukafugie bata.
 
Sio ulanga tu, idara ya elimu sekonfari nchi nzima hawajaripa Nauru ya juni 2020 na DEC 2020
 
Kikubwa ulienda safari likizo na ulirudi salama pigakazi ,nilipeleka fedha yenu shambani tikiti zikagoma ,vumilieni
 
Back
Top Bottom