Watumishi hewa 515 wagundulika katika mikoa mitatu

Watumishi hewa 515 wagundulika katika mikoa mitatu

Wacha porojo wewe huyo CAG ungemjuwa kama si Kikwete? Halafu unajuwa report ya CAG ya mwaka 2013/14 wa Kiserikali inawasilishwa lini?

Bila Kikwete mngeyajuwa hayo?
Unadhani naweza kubishana na shabiki wa mtu? Nina uwezo wa kujadili hoja na mtu mwenye uelewa na anae hitaji kujadili uhalisia na sio nadharia zenye kushabikia mtu.kila la heri.
 
Unadhani naweza kubishana na shabiki wa mtu? Nina uwezo wa kujadili hoja na mtu mwenye uelewa na anae hitaji kujadili uhalisia na sio nadharia zenye kushabikia mtu.kila la heri.

Umeshindwa kujibu maswali very simple. Huwezi kubishana na mimi, huwa sikisii.
 
ichunguzwe hiyo mishahara ya watumishi hewa waliokuwa wanaifaidi ni kinanani na hatua kali za kinidhamu zichukuliwe na mamlaka husika.
Ivi Takukuru hilijambo haliwahusu? Wakati mwingine nivigumu kujua takukuru wanahusika na jambogani haswa...institution kubwaa,mishahara mikubwaaa,waajiriwa watoto Wa wakubwaa kilakitu kikubwaa ispokuwa utendaji!!
 
Huyo mchangiaji wa mwisho
Nimependa alivyo fichua hilo.
Ila kiukweli bado mambo nimagumu
 
Umeshindwa kujibu maswali very simple. Huwezi kubishana na mimi, huwa sikisii.
Nimekusoma mara kadhaa Faiza, unawelewa mzuri sana Ila umekingwa na udini na uchama. Tutakusoma vizuri ukitoka ndani ya ilobox.
 
Nimekusoma mara kadhaa Faiza, unawelewa mzuri sana Ila umekingwa na udini na uchama. Tutakusoma vizuri ukitoka ndani ya ilobox.

Wasiwasi wako ndiyo tatizo lako, nioneshe kwenye huu uzi huo udini na uchama uko wapi?

Ukishindwa kuonesha, ujuwe tatizo lipo kichwani mwako.
 
Siku 15 zilizotolewa na Rais Magufuli kwa Wakuu Wapya wa Mikoa kuhakikisha wanawabainisha na kuwaondoa wafanyakazi hewa zimeanza kutoa picha kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa nchini.

Mpaka sasa imebainika kuna wafanyakazi 515 katika mikoa mitatu ambayo ni Kigoma (169), Dodoma (144) na Singida (202).

Taswira hii inaonyesha jinsi ambavyo tatizo la wafanyakazi hewa linaweza kuwa ni kubwa zaidi ya ilivyofikiriwa hasa ikichukuliwa limekuwepo kwa muda mrefu huku mamilioni ya pesa za walipa kodi yakienda kwenye mifuko ya wajanja wachache.

Inakadiriwa serikali ina wafanyakazi zaidi 500,000 na inalipa mishahara takriban Sh. bilioni 549 kwa mwezi, ambayo kati ya fedha hizo kuna malipo ya wafanyakazi hewa.

Katika repoti yake ya mwaka 2013/14, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alibainisha kuna zaidi ya Sh141.4bn zimelipwa kwa wafanyakazi hewa katika mwaka wa fedha.


===============================
Mdau mmoja ametoa angalizo muhimu kuhusu kinachoendelea kwenye zoezi la kuhakiki wafanyakazi ambapo amesema;

Mwingine amesema/ameandika hivi;

Baada ya kuona ubadhirifu huo wa fedha za Ummma tunaomba hutua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wale wote wanao husika kwa namna moja au nyingine, maana lazima walikuwa wanajua uovu huo ambao umeitia hasara Serikali yetu kwa kipindi kirefu.
 
Ndugu yangu kuna vitu hujui, swala swala la dawa kukosekana hospital tatizo la kuibiwa na watumishi wa afya lina contribution ndogo sana tatizo lipo kwenye budget zisizo tekelezwa hata kwa asilimia hamsini, na pia wanasiasa hawasemi kuwa huduma zinauzwa!!!@bintishomvi, post #18.
 
Haya yote unaoyaona na matokeo ya Kikwete kuanzisha system ya kuyabaini hayo, jisomee:

Katika repoti yake ya mwaka 2013/14, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alibainisha kuna zaidi ya Sh141.4bn zimelipwa kwa wafanyakazi hewa katika mwaka wa fedha.
Faiza..dont embarass yourself,kuna upuuzi mwingine uko wazi,haujifichi,unapotetea uozo,hauitendei haki hii nchi.
 
so Magu ana safari ndefu ya kuinyoosha na kufika tunapopataka. Tuliambiwa, kwa kutumia vyanzo hivi hivi, ila mianya ya ukwepaji ikibanwa kila kona, tunaweza kuboost bajetin yetu kwa 40%. Sasa naamini inawezekana

Rais atoe agizo kwa Takukuru kuwa kokote watakapogunduliwa wafanyakazi hewa viongozi wote wakamatwe na kufunguliwa mashtaka ya wizi na uzembe kazini na kutumia madaraka vibaya na wanaohusika walipe fedha zote zilizoibiwa. Wakaguzi wa CAG nao wanahusika na uozo huo kwa hiyo nao wanahongwa kama sivyo waboreshe mfumo wa ukaguzi.
 
Faiza..dont embarass yourself,kuna upuuzi mwingine uko wazi,haujifichi,unapotetea uozo,hauitendei haki hii nchi.

Jibu hoja achana na mimi, ni nani aliyefanya zaidi ya Kikwete wa kabla yake?
 
Kuna eneo nyeti sana la wafanyakazi hewa ambalo linahitaji utulivu,commitment na uzalendo katika kuwabaini hawa wafanyakazi hewa.

ni muhimu Magufuli akaunda timu maalum itakayoenda halmashauri za wilaya kuverify hizo taarifa walizoandaa....hii timu ikifika huko iangalie maeneo yafuatayo...

-Wastaafu wa miaka kama mitano nyuma kama bado wako kwenye mfumo wa lawson.

-Waliofukizwa kazi

--Majina yaliyofanana...kuna baadhi ni mtu mmoja lakini check no ni mbili tofauti.

-waliohama vituo hasa kutoka mkoa A kwenda B...waangalie kule alikotoka na hapo alipo.

Watumishi waliohama kutoka serikalini na kwenda kwenye NGO au kutoka Taasisi za kidini kuingia serikalini.

Watumishi walioomba likizo bila malipo.

Hii timu ikimaliza kuhakiki ichapishe orodha ya watumishi kwa kila kituo na kuibandika kwenye vituo vya kazi.
Hayo maeneo nyeti. Hapo kwenye Wastaafu ni Jipu kubwa.... Likitumbuliwa wataumia wengi
 
Ndo maana wakati wa Kikwete nchi ilifika hatua imenock, system ilifail kabisa.
Acha unafiki kijana, tena koma kabisa kufikiria kuwa haya yalikuwepo wakati wa KIKWETE TU. Haya yalikuwepo wakati wote na kwa taarifa yako hayo ni tone tu ktk bahari, machafu ni kila sehemu.

UKWELI NI KWAMBA SERIKALI ZOTE ZA CCM, NYAKATI ZOTE ZIMEOZA NA WALA MAGUFULI HAWEZI KUREKEBISHA CHOCHOTE. LA MUHIMU NI KUIWEKA CCM PEMBENI NDIO UTAONA MAAJABU YA MUSA.

NAKUOMBA USEME TENE NA RUDIA KUWA CCM IMEOZA NA INANUKA.
 
mzee mkubwa hakosekani kwenye izi dili! naskia adi ku supply maji ya ofc alikua anaingilia! Mzee magu hatuna chakukulipa piga kz tu!
 
Tatizo la ajira serikalini/mashirika hapa Tanzania sio tu wafanyakazi hewa. Kuna wale ambao naweza kuwaita viongozi wasio na umuhimu. Kwa mfano kila mkoa una utitiri wa vyeo vinavyoenda sambamba na mkuu wa mkoa. Kwenye wilaya ni hivyo hivyo. Na zaidi mimi nadhani wakuu wa wilaya hawana umuhimu wowote. Ukirudi kwa wabunge ni wengi sana. Bila kufumua system nzima na kubaki na viongozi wachache hatutafika mbali.

Umegusa kwenye moyo! Hapa ndipo hisia zangu zinanituma kuingia barabarani na kuidai katiba mpya maarufu katiba ya jaji Joseph Sinde Warioba.
 
taasisi yoyote au shirika lolote litakalopatikana na wafanyakazi hewa kitu cha kwanza kiwe kumfukuza Mkurugenzi wa sehemu husika na kumshitaki,maana kuna mashirika mengine hayataki kuutambua uongozi wa chama cha wafanyakazi ili wazidi kupiga dili na kuficha maovu yao kwa mfano TPRI Arusha
 
Hii tatizo ni kubwa na imelelewa na CCM siku wakitoka madarakani mtashuhudia mengi
Huu ushabiki wa kisiasa ya kuwa kila kitu kibaya ni CCM hautuendelezi po pote. Unazungumzia siku CCM watakapoondoka madarakani tutashuhudia mengi; mbona sasa bado wapo madarakani na wao wenyewe ndiyo wameyagundua hayo maovu? Ni chuki yako tu kwa CCM ndiyo inakufanya usione mazuri yanayofanyika kwa kufichua maovu hayo.
 
Haya yote JK aliyajua ila hakua na utashi wa kuyafanyia maamuzi manake alijua kwa kiasi kikumbwa wanaojilipa ni hao hao watu wa system na makada wa chama,inasikitisha jinsi alivyofanya nchi shamba la bibi kila mtu anachota anaondoka zake.Kuna haja ya kufuta kinga ya Raisi kushitakiwa kwy katiba mpya ya Magu km alivyoahidi ili haki itendeke.Km Zambia iliwezekana hata bongo inawezekana.
 
Back
Top Bottom