Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Kifungu cha 29 cha sheria ya ushahidi ya Tanzania kipo wazi kabisa, kuwa mahakama haitakataa kupokea ushahidi wa mtuhumiwa kukubali kutenda kosa hata kama alipata vitisho, mateso na au bakshishi iwapo ni kweli alihusika, ila kama alipigwa na kuteswa na polisi wakageuza uongo uwe kweli hapo ndipo itakataa kupokea huo ushahidi.
Kesi ya Mbowe na wenzake inaendelea naona wafuasi wa CHADEMA wanashupaa sana kudhania kuwa watuhumiwa wenzake na Mbowe kutoa maelezo kuwa walipigwa na kuteswa itakuwa ni sababu ya kutotenda kosa. Ni wazi kuwa mtu anatakiwa akiri kosa kwa hiari kama kifungu cha 27 cha sheria ya ushahidi inavyosema.
Lakini kama akikiri kwa lazima halafu ikawa kweli alitenda kosa basi hapo kuna hatia. Je, wakati hizi kesi ndogo juu ya kesi kubwa zikiendelea na tuhuma za kupigwa na kuteswa zikiibuka, Je hawakushiriki kipanga kulipua vituo vya mafuta?
Factum probandum?