Watuhumiwa wa EPA wasamehewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watuhumiwa wa EPA wasamehewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Andrew Nyerere, Nov 17, 2008.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Nov 17, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani ingekuwa bora kama watuhumiwa wote wa EPA wangesamehewa. Siyo wasamehewe na Rais au Mahakama,ila wasamehewe na wananchi. Watanzania ni bora tujifunze kusamehe,kwa sababu Allah ni msamehevu.

  Huu ni mwanzo mpya,awamu mpya,siyo kwetu sisi,lakini awamu mpya imeanza Marekani baada ya Obama kuchaguliwa. Kwa hiyo,awamu mpya zozote,zinapaswa kuanza na watu kusameheana.

  Let us begin a New Dispensation. Dispensation[katika Kanisa Katoliki] ni uwezo wa kiongozi mpya kuyasamehe makosa yaliyotokea wakati wa kiongozi aliyepita. Tutambue kwamba sasa kuna madiliko ya uongozi. Viongozi wa zamani hawapo. Viongozi wapya wapewe nafasi ya kutekeleza sera zao,sera mpya.

  Mtume Muhammad alisema katika hotuba yake ya mwisho,kwamba wasamehewe wale wote waiotenda makosa kabla ya Uislamu kuanza.

  Kwenye Biblia imeandikwa kwamba mtu akiua kwa bahati mbaya[manslaughter],apelekwe,au akimbilie kwenye City of Refuge,na akae huko mpaka High Priest atakapokufa,halafu anaweza kurudi. Kwa hiyo Wayahudi wahalifu walikuwa wanakimbila kwenye miji hiyo,kama vile Hebron.

  Siku za karibuni BBC kipindi cha World Have Your Say walifika Mwanza. Walikuwa kule St Marys School. Wakakuta vijana kule wanaunga mkono rushwa,wanaunga mkono kila uovu,inaelekea. Yule BBC reporter alishtuka sana,na mwalimu wao wale wanafunzi akaongea apologetic remarks. Lakini ukweli ni kwamba hawa ni vijana wa siku hizi ambao inaonekana wapo tayari kusamehe maovu ambayo wazazi wao walikuwa hawako tayari kuyasamehe,ili tuweze kujenga Dunia Mpya.

  Tuwasamehe hawa mafisadi sasa hivi,au tuwasikilize,lakini hatimaye tuwasamehe.

  Tuwe na roho hii ya kusameheana,tuwasamehe watu waliolikosea Taifa,yaani waliotukosea sisi wote;au mtu yeyote ambaye ametukosea sisi wenyewe,labda kwa mfano mtu amemuua ndugu yako.

  Pia tujisamehe sisi wenyewe,makosa ambayo tumefanya. Kwa sababu inatokea,mtu hajafanya kosa lolote,lakini hata hivyo anaona kwamba ni lazima ajilaumu sana kwa mambo mengine ambayo aliruhusu yatokee,au aliyafanya,basi,anaona taabu sana kujisamehe.
  barua ya jumatatu,tusameheane.
   
 2. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kusamehe 7 mara 70 ama! Mhhh Hii ni ngumu bro, lazima wawgawie na Mahakimu, waendesha mashtaka na makarani wa pale kisutu ndo MAHAKAMA iwasamehe.
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wakitaka tuwasamehe na waje hadharani watuombe msamaha live kwamba kweli wametuibia, sasa tutawasemeheje wezi wasio taka hata tujue walituibia? tutawasemeheje wezi wanao tumia mamlaka iliyopo kututisha kwamba tukiwagusa nchi yetu itadondoka? Tuta wasemeheje maharamia walio mteka baba yetu 'serikali' na wako wanamtisha kwamba ukijitingisha tunakumaliza??

  Hawa siyo watu wa kusamehewa, ni watu wa kumalizwa kabisa na hata kutokomeza unyayo wao!

  Hawa ni watu wa kupewa wanacho stahili, pia iwe fundisho kwa maharamia wengine wenye mawazo kama hayo! Tusikimbilie kuwasamehe kwani wapo wezi/maharamia wengine wano nyemelea keki yetu kwa macho mia mia!

  NATOA WITO, TUWASHUGHULIKIE NA SI KUWASAMEHE KAMWE!!
   
 4. L

  Lorah JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  kweli kabisa tuwasamehe maana hasira tulizonazo ndo zinatufanya tugomegome maana laiti skendo ya EPA isingetoka wanafunzi wa vyuo vikuu wasingekuwa na hasira kiasi hiki kwani wote tuliamini Tanzania ni nchi masikini serikali yetu haiwezi hata kukopesha na MAANISHA kuwaazima watoto wetu hela halafu baada ya miaka mitatu au minne waanze kurudisha kidogokidogo yani pamoja na kwamba wanasoma kwa ajili ya kunyanyua uchumi huohuo wa serikali....

  hata hivyo wazee wetu wasingelela barabarani kama wasingekaa wakafikiria zile hela za EPA ndo hizo walizotakiwa kulipiwa madai yao kwani serikali ilisema hazikuwa hela za walipa kodi so ni za EAC?????

  walimu wetu wasingegoma kama wasingekaa nakufikiria kwamba wenzao walioko mabenki wanapata madili ya kuhamishahamisha hela kisanii while wao waliowafundisha kwa msoto wananyimwa hata haki yao ya kupewa kilicho chao, na ninaogopa mkisamamisha mgomo wa hawa walimu watoto wetu watagoma kwenda shule maan watachapwaaaaaaaaaaaaaaa na mgomo utageuka kuwa WANAFUNZI WAGOMA MPAKA WALIMU WALIPWE HELA ZAO maana frastration za walimu wao zimewachosha sijui nani atazuia mgomo chama cha wazazi au????

  Tuwasamehe maana nia yao ilikuwa kuonekana kuthaminiwa na kutambuliwa na watu kwamba wao ndo wenye pesa sasa vyote hivyo hawana wamebakiwa na jina moja MAFISADI --- adhabu tosha.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tuwasamehe wakati wenyewe wamekana mahakamani kuwa wameiba!! Tutawasamehe kwa kosa gani sasa?
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Muanzisha mada utanisamehe ila huu ni upuuzi uliopitiliza kikomo!Watu waibe then tuwasemehe kisa Marekani wameingia a new era?
  What does USA has to do with us?
  Mpaka lini tutakuwa wapuuzi wa sheria kiasi hiki?Raisi mwenyewe nawasamehe lakini nadhani wameshindwa kumwambia kama amevunja katiba ya nchi maana raisi ana uwezo wa kumsamehe mtuhumiwa iwapo tuu atagundulika kuwa na kosa!
  Inapaswa waadhibiwe wote kwa pamoja iwe amelipa ama hajalipa!
   
 7. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  MKUU AEKA MANGI MBONA UMEKUWA NA DHARAU SANA KWA HAO MAHAKIMU AS IF WEWE NI MHANGA WA MATENDO UNAYOYAHUBIRI HUMU!!! AU WEWE NI SEHEMU YA WALE MAHAKIMU WALIOKIMBIZWA KATIKATI YA JIJI KWA TUHUMA HIZI UNAZOZIRUSHA KWAO SASA? MAANA HIYO UNDERLINED STATEMENT HAIONYESHI UKAKAMAVU WA HOJA ZAKO JUU YA HAO UNAOWATUHUMU, KUNA THREAD HUMU NDANI NILIKUOMBENI MUIFANYE HOME WORK YENU UPYA LAKINI NIKAJIBIWA ETI NILETE MIMI NILIYEKWISHA IFANYA!!!, KAMA DPP NA TEAM YAKE YA WANA SHERIA WAKISHINDWA KUITHIBITISHIA MAHAKAMA BASI HAKI ITAENDA KWA MTUHUMIWA LAKINI DPP AKIWEZA NA WATUHUMIWA WAKISHINDWA KUTHIBITISHA BASI HAKI ITAKUWA YA SERIKALI, SASA KWANINI TUNAINGIZA GAME YA SHEIKH YAHAYA KTK ULINGO ULIO WAZI KITAALUMA KTK MAAMUZI, TUWE NA SUBIRA HUKU TUKIHIMIZA SERIKALI NA TIMU YAO IKOMAE ITHIBITISHE BEYOND MASHAKA KTK KUTHIBITISHA TUHUMA, KTK HALI HIYO HAKUNA REFARII WA SHERIA ATAKAYETHUBUTU KUUPINDA UKWELI HUO. ZAIDI YA HAPO, UKAE UKIJUA KUWA KISUTU NI STARTING POINT BADO KUNA FURSA KWA MZEE JK(Jaji kiongozi-mahakama kuu) NA PIA CJ(Jaji mkuu-rUFAA), SASA KWA UTARATIBU HUU USIJESHANGAA HII NGOMA ISIISHE MPAKA JMK ANAKABIDHI NCHI KWA MRITHI WAKE 2015. MAAMUZI YA HAKIMU WA KISUTU YANAHESHIMIWA NA MAHAKAMA HIYO ILA YANAWEZA KUPINGWA NA MAHAKAMA YA JUU YAKE, VIVYO HIVYO MPAKA MWISHO NI COURT OF APPEAL KWA HAPA KWETU........, KWA HIYO HAKIMU ANAWEZA KUWAFURAHISHA WANANCHI LAKINI MAJAJI WA MAHAKAMA KUU AU RUFANI WAKATOFAUTIANA NAYE KTK MAAMUZI, HAYA TUTAYAJUA BAADA YA KESI NA SIYO SASA MKUU MANGI.
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kesi hamna

  hakuna cha kusameheana mle

  in short hakuna kesi na ninachokiona wanaofaidika ni ma lawyers tuu kwenye hili
   
 9. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Vyovyote utakavyo niita, mhanga ama vipi ni haki yako, ila huo nao ni mtizamo wangu kama ulivyo mtizamo wako wewe. Una uhuru wa kufikiria chochote as long as you are not insulting anybody.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145


  Mkuu jina lako linaonyesha kuwa wewe ni mhindi kwa hiyo kama unawapigia magoti wahindi wenzio kinamna hapa hicho kitu sahau....Kama wale ni ndugu zako mbona hawakukumbuka kuwaonea huruma ndugu zetu wanao ishi kwa shiida na tabu kweli kweli utafikiri hii sio Tanzania yao kwa nini hawakuwasahidia ndipo tuseme fedha za EPA zimewasaidia walalahoi.
   
 11. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Si bure, kama hujatumwa basi kuna jambo ama unataka kuondoa focus zetu kwenye mambo muhim ya Taifa. Tuwasamehe wakatia ndugu zetu wanakufa kwa kukosa shs 1,500 za kununua dawa ya malaria?

  Status yako inaonyesha wewe ni new member (hata kwa muda) ingawa pa waweza kuwa ni Expert member ambaye umeingia kwa jina jipya ili kupima joto letu. Tafadhali usitupotezee muda.
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ningekuwa na uwezo ningefutilia mbali hii hadithi inayonifanya nipate ukungu kwenye macho!! Unamsamehe nani wakati hata wezi wenyewe huwajui? Unasemehe vipi wakati unaendelea kuibiwa?

  Hebu twambie kama unaweza kumsamehe mtu uliyemkamata live anakula uroda na mkeo au mmeo na bado anaendelea kukuibia? Kama unaweza basi jaribu kutafuta dunia yako peke yako mkawasamehe mafisadi wenu. Sisi tutakomaa nao na kama tungekuwa na uwezo vichwa vyao ndo halali yetu! Siku moja ndoto yetu itatimia, tutaweka mafuvu yao kwenye makumbusho kwa ajili ya wajukuu wetu kuona na kupata kumbukumbu ya watu waliotunyonya damu! Hakuna msamaha wowote kwa fisadi asiyetubu, iwe mbinguni au ahera! .....Usilete hadithi za paka na panya hapa kutuchanganya.
   
 13. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thread hii ilekezwe kwenye forum ya Jokes/Utani.
   
 14. O

  Omr JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2008
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wasamehewe kitu gani, wizi ulifanyika sio mdogo na karibu pesa zote ziko india na dubai. Hakuna msamaha tena ikiwezekana wahukumiwe kifo
   
 15. M

  Mama JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Ufisadi walioufanya umesababisha vifo vingi, hasa vya kina mama wajawazito, watoto na wanavijiji wengine kwa kukosa huduma muhimu za kijamii kama vile hospitali.
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  GT unadhani hakuna zaidi ya lawyers wanaofaidika au watakaofaidika na hizi kesi?... kwa taarifa yako hata kodi zitakusanywa kwenye fees za hao lawyers na wengine kwenye chain, waandishi wa habari watauza stories, magazeti yatauza sana... kampuni za uchapishaji nazo zitafaidika, ni mlolongo mrefu....
   
 17. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wanyongwe ama wa appoint a firing squad kuwahukumu hawa mabaradhuli!
   
 18. M

  Masatu JF-Expert Member

  #18
  Nov 18, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Msamaha huo kwa watu EPA tu? mbona kwenye magereza kumejaa walioba kuku, simu, cheni na wengine wamehukumiwa kwa makosa tu wala si wahalifu.

  Kwa kutumia logic ya Bwana mkubwa hapo juu basi tufungue milango ya magereza yote na tuanze upya!

  Msitu mpya na komba wapya!
   
 19. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Inaonekana kina Patel wanakutishia maisha mkuu...
   
Loading...