Watu wote mliojiua nikawasema vibaya naomba mnisamehe sana

Watu wote mliojiua nikawasema vibaya naomba mnisamehe sana

Kwa mtazamo wako umedhani Mungu ana makosa! Wakati tatizo ni pale mwanadamu alipochagua kumtii ibirisi.
nilikua nawashangaa sana wasioamini kuhusu mungu sasa hivi siwashangai tena, kwann mwngne azaliwe kwenye shida akulie kwenye shida hadi afe kwenye shida mwngne raha kuzaliwa mpk kufa ila mungu yuleyule mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awazavyo mtu, ndivyo alivyo.
1. Kosa la kwanza kubwa, ni kuwaza kifo kama moja ya suluhu ya matatizo yako.

2. Jiulize jambo moja tu, katika watu wote duniani, ni wewe peke yako una hali ngumu kuliko wote? Na hakuna anaepitia au kuwahi kuwa kwenye hali kama yako akavuka?

3. Kama ni kweli unamcha Mungu kama unavyodai, ukifa utaenda mbinguni lakini ukijiua njia ya jehunum taa imewaka ya kijani.

Kuna mtu akisalitiwa, anajiua.
Mwingine akiwa na madeni au kufilisiwa, anajiua.
Kujiua sio kipimo cha ukubwa wa tatizo kwa sababu wapo wengi wanaopitia nyakati ngumu na wameendelea kuishi.

Wagonjwa wa saratani wengi wamepitia mateso makali lakini bado walisubiri hadi muda wa kumaliza safari ulipofika wakatangulia mbele za haki. Wengine wamebahatika kupona.

Narudiia tena, awazavyo mtu, ndivyo alivyo.
Pinga kwanza na futa kabisa kifo kama suluhisho la hali yako.

Una habari hadi sasa hivi hapo ulipo una kesi ya kujibu kuhusu kusudio la kujiua?
 
Na ukweli ni kwamba huwa wanakuwa depressed maana mtu kufikiria tu kuandika uzi wa aina hiyo tayari ujue ana tatizo no matter una kiwango gani cha kupuuzia, ila kuna watu wanawakandamizia maneno mazito yenye kukatisha tamaa kejeli, kashfa, na hata matusi.
Mmh Daaah, nimekosa hata cha kuongea........wengi waliokuja na nyuzi za aina hii hapa jf, wameishia kujiua kweli. Mpka naogopa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah!...Mkuu usikubali kukata tamaa, uhai wako una thamani kubwa sana usijidhuru.
 
😀😀😀😀😀

Sawa, umeiona mada?? Sisi tunaambiwa hakuna kukata tamaa na rehma za Mwenyezi mungu na kujiua ni miongoni mwa dhambi zitakazompeleka mtu peponi bila hesaab. Tuwe makini kabisa.
Kwa kweli ndugu dunia ina mengi sana hii Allah atuepushe na roho hizo inshallah
 
Jambo pekee linaloweza kukufanya uwaze kujiua ni kutengwa na ndugu, marafiki, mke, mume wakati wa shida hasa hasa ugonjwa wa muda mrefu. Maranyingi unapokuwa katika maumivu ya muda mrefu unayachukia maisha, unakata tamaa ya kuishi, unapata msongo wa mawazo.pamoja na yote usije kujidhuru, usiwaze kujiua hutalala kwa amani.
Muachie MUNGU nafasi yake atende sawasawa na mapenzi yake. Duniani kote kuna watu wanashida kuliko yako hata nguvu ya kuandika thread kama hii uliyoandika hawana.kuna mtu anapumua Kwa msaada wa mashine kila siku na bado anatamani kupona, wapo wanaosafishwa figo kila baada ya mwezi na hawajawahi kuwaza kujiua.
Kila Jambo na wakati wake unaweza ona umekosa suluhisho sasa lakini saa yaja utasahau yote.Ukipenda ni PM.
#HAUFI#
 
pole sana, lkn usikate tamaa. elewa mungu yupo. tumia muda wako kusoma vitabu vitakatifu biblia au Quran pia fanya ibada. mungu atakusaidia kukuondolea matatizo uliyonayo
 
Naogopa kuchangia mada kama hizi, kwa kuwa huyu hahitaji ushauri kashafikia maamuzi.... sitaki kuleta mizaha nikajuta baadae.
 
Back
Top Bottom