Hamna kitu hio simu ni kwajili ya fashion tu... Uhondo wote upo simu za Android (Samsung, lg, nokia, sony, Google pixel, n.k na hata hizi simu za bei rahisi kama Tecno na infinix, japokuwa zimetengenezwa kwa vifaa vya bei rahisi bado nazo zina sifa nyingi muhimu kuzidi iphone).
-Iphone sio simu yenye kamera nzuri kuliko simu zote kama wengi wanavyo danganywa, Android ina simu zinakimbiza hii sekta, Simu kama google pixel zinamgaragaza iphone, hata wachina kama kina xiaomi wana camera bora kuzidi iphone.
-Cable za iphone zinachaji taratibu, zina kasi ndogo ya kuhamisha mafaili na zina ubora mdogo, walishupaza shingo mda mrefu lakini hatimae wamekubali kuanza kutengeneza simu zitazotumia usb cable za android.
-iphone haina tundu la earphones, ni mpaka uwe na earphones za kuchaji chaii kila mara.
-android kuna apps nyingi zaidi kuliko iphone,
-iphone haiwezi kurekodi simu unazopiga / kupokea
-iphone inatengenezewa vifaa vyake kibao na makampuni ya simu za android
-iphone haina apps za kutumia internet bure, kwa android kuna apps kama ha tunnel watu wanatumia internet bure bila vifurushi.
-iphone haina memori kadi, yani simu yako ikiungua au ikifa inaenda na mafaili, android hata simu ikipata hitilafu unabaki na kopi ya mafaili kwenye kadi.
-iphone ni ngumu kuhamisha mafaili kwenda kwa computer, mfano mrahisi simu za android ukitaka kuprint file unachomeka tu cable unahamisha file lakini iphone process kibao inabidi ubebe na flash.
-iphone haina radio, kusikiliza radio ni mpaka uwe na data, sasa sijui utasikilizaje kama huna data, ukienda sehemu haikamati internet ama internet inazimwa kipindi cha uchaguzi
n.k,,,,
pitia
>> uzi huu << utaona kwamba iphone ni kopo tu la gharama lisilo na utofauti na vile vimbwa vidogo vya mapambo haviwezi hata kumtisha paka ila vinauzwa milioni 3, hapo kuna mbwa anauzwa laki 8 kaoitia mafunzo, ana mwili mkubwa vipaka havisogei, anaweza kubweka ukadata, ana mbio, haumwi magonjwa hovyo hovyo, mwizi akiruka ukuta kayakanyaga, anakuchangamkia akikuona, n.k.