Ngoja nipangue point zako moja baada ya zingine. Ambako uko sahihi nitakupa [emoji736] pia sina nia mbaya. Twende kazi.
-Kuhusu Camera [emoji736]. Kweli iphone sio simu yenye Camera kali kuliko zote. Kuna simu zina Camera nzuri sana kuliko iphone (in theory - hapa sijajua nitumie kiswahili gani) ila practical (yaani uwanjani) iphone ina camera rahisi zaidi kutumia. Unafungua unapiga picha. Settings za camera ya iphone ni very minimal. Ukija kuzama ndani kwenye mambo kama ya QR scanning, 3D modeling na AR virtualization utaona poa iphone wako more advanced.
- cable za iphone zinachaji taratibu na zina kasi ndogo [emoji736]. Hii iko sahihi haihitaji mjadala.
Ila unakosea unaposema Cable za android. Kumbuka Lightning cable ni specific au maalumu kwa iPhone tuu ila Android hana umiliki wowote kwenye type -C na ndo maana iPad, Macbooks, apple TV, iMac, apple Pods na bidhaa tofauti tofauti za apple nazo zinatumia Type C. Huu mfumo unamilikiwa na USB Implimenters Forum na sio android.
-iPhone haina tundu la earphone. [emoji23]. Mkuu kwanza nicheke maana haya mambo nadhani yalikua debates za mwaka 2017-2019 baada ya hapo tulimove on na kutafta sababu zingine.
Kwa sasa sim ambayo haina earphone Jack sio iphone tuu. Zipo nyingi. Fanya tafiti alafu njoo tena.
In theory tundu la earphone litapotea kabisa kwa sababu muziki utakaokua unatokea kwenye port ya Type C ni wa tofauti na utakaokua unapatikana kwenye port ya earphone ambayo itakua either ni TS ama TRS.
-Android kuna apps nyingi kuliko iphone [emoji736] hii nakupa bila ubishi ila pia, katika kila app ambayo ipo android kuna mbadala ama app inayofanya kazi sawa au kwa ukaribu kwenye iphone.
-iphone haiwezi kurekodi sim unazopiga ama kupigiwa [emoji736] hii nakupa ni kweli lakini je? Unajua kisheri ni kosa kumrecord mtu bila yeye kujua? Unajua kwanini huduma kwa wateja wanakuambia kwanza sim hii itarekodiwa?
Ila pia ukitaka kuweza kurekodi sim kwa iphone inawezekana. Tumia Cydia (Checkrain) japo kila muda software ya iphone hufuta apps ambazo haziwekwa kutoka app store.
- iPhone inatengenezwa vifaa kibao na makampuni ya android. Hii ni point nyepesi sana. Tuzungumzie simu kama Samsung. Samsung Electronics ananunua vioo vya sim zake kutoka sub branch yake SAMSUNG DISPAYS. Apple ananua vioo kutoka Samsung Display. Hii haimaanishi kwamba kioo cha iphone sio imara kuliko samsung. Kampuni hii ya Samsung Displays baada ya kuacha kutengeneza panels iliuza hati miliki zake zote kwa TCL na samsung Displays amebaki anatengeneza LcD na Oled.
-iphone haina apps za kutumia internet bure, kwa android kuna apps kama ha tunnel watu wanatumia internet bure bila vifurushi. [emoji736]
Hii ni sahihi sina la kupinga. Ila pia kuna way around to archive this. Kaa tulia Fanya research utapata hio net ya bure.
-iphone haina memori kadi, yani simu yako ikiungua au ikifa inaenda na mafaili, android hata simu ikipata hitilafu unabaki na kopi ya mafaili kwenye kadi. [emoji736]
Hii iko sawa kwa asilimia kadhaa. Kwanza kabisa, iphone kama zilivo sim za android ambazo hazina external memory card (ambazo zipo nyingi tuu maana point yako imekaa as if all androids have memory cards) inakupa option ya kuweka nakala ya vitu vyako online (cloud base storage)
-iphone ni ngumu kuhamisha mafaili kwenda kwa computer, mfano mrahisi simu za android ukitaka kuprint file unachomeka tu cable unahamisha file lakini iphone process kibao inabidi ubebe na flash.
[emoji23][emoji23] inaonekana wewe swala la security ni kipaumwisho kabisa. Hujali kabisa. Ndo maana ishu ya kuskia mtu anakuambia kuna app imeingia kwenye sim yake hajui imeingia vipi ni ngumu sana kwenye iphone. Android users wengi sana wanakutana na Malware na Ransomware kibao zinaingia kwenye simu zao hasa pale wanapohamisha data zao.
-iphone haina radio, kusikiliza radio ni mpaka uwe na data, sasa sijui utasikilizaje kama huna data, ukienda sehemu haikamati internet ama internet inazimwa kipindi cha uchaguzi [emoji275][emoji275][emoji275] Naanza kuona hili bandiko lako ni la kukopy na kupaste. Hio android yako yenye redio ni ipi? Ni android gani ya mwaka 2020-2023 ina redio? Je ni android zote? Je wenye android ambazo hazina redio? Hawa tunawaweka wapi?
-SASA NATAMANI SANA NIKUPE UMUHIMU WA KUA NA IPHONE. ILA NINA WASIWASI UNAWEZA ICHUKULIA HII KAMA BATTLE YA ANDROID VS IPHONE. MIMI NAONGEA AT A NEUTRAL POINT.
NATUMIA REDMI NA IPHONE.
UKITAKA KUJUA ZAIDI NJOO PM NITAKUELEZA MENGI NA KWA UNDANI ZAIDI KUHUSU IPHONE.