Watu wengi wana kiasi kidogo cha asidi tumboni lakini hawafahamu

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,223
12,728
Kwa siku mwili wa binadamu unatengeneza kiasi cha asidi kati ya lita 1 hadi 1.5. Yaani ile asidi ya kujaa kopo kubwa la maji la lita 1.5! Asidi hiyo ni nyingi na kali sana. Ukali wake unafika PH ya 1.5. Manyama, matobolwa, samaki, minyofoo, pweza, vyakula vyote vigumu na laini husagwa na asidi. Mbali na hilo pia huua vijidudu vilivyoingia na chakula na kuweka mazingira mazuri kwa vimeng'enya vya tumboni kufanya kazi yake vyema.

TATIZO LA UKOSEFU WA ASIDI NA KIUNGULIA(Reflux)
Tumbo limeumbwa kwa namna ambayo linaweza kuhimili asidi hiyo kali. Kuta zake zipo imara na zina utando unaosaidia zisidhurike na asidi. Lakini huku juu kwenye koo la chakula kuta zake siyo imara kuweza kuhimili kiasi cha asidi iliyopo tumboni. Ndiyo maana kati ya tumbo na koo la chakula kuna valve ambayo inazuia asidi ya tumboni isipande juu kwenye koo la chakula. Valve hii hujifunga vyema pale kiasi cha asidi tumboni kinapokuwa juu.

Ikitokea kiasi cha asidi tumboni kikashuka valve hii hulegea na hivyo kufanya vitu vya tumboni kupanda juu kwenye koo la chakula. Asidi hii japo haina nguvu lakini kwa mazingira ya koo la chakula na hata mdomoni ni asidi kali sana. Ndiyo maana huwa inachoma kifuani na ikifika mdomoni inaleta uchachu mkali.

Kwa haraka haraka unawza dhani asidi imezidi tumboni ndiyo maana umepata tatizo hilo kumbe ni kinyume chake.

Mara nyingi tatizo hili hutibiwa kwa dawa za kupunguza asidi. Dawa(kama 'magnesium' )hizi zinasaidia ili kulinda koo la chakula lisiathiriwe na asidi na kuleta matatizo kama kansa ya koo na hata kuharibu meno. Lakini kutibu tatizo hili kwa namna hii huongeza tatizo la upungufu wa asidi tumboni. Hapo inatokea cyle mbaya ya kutibu-tatizo kuongeza tatizo.

UPUNGUFU WA ASIDI NA TUMBO KUJAA
Upungufu wa asidi tumboni husababisha chakula kukaa tumboni kwa muda mrefu sababu hakimeng'enywi haraka. So tumbo kujaa jaa na kutuna inaweza kuwa sababu ya upungufu wa asidi tumboni.

UPUNGUFU WA ASIDI NA KUNUKA MDOMO
Asidi ikiwa chini maana yake vyakula vigumu kama nyama vitachukua muda mrefu sana au havitavunjwa vunjwa. Jambo hili litafanya vyakula hivi vianze kuliwa na bakteria wa tumboni na kuvunda. Bakteria hawa katika kula huko chakula hutokeza gesi mbalimbali. Sasa kwa kuwa valve kati ya tumbo na koo la chakula imelegea sababu ya upungufu wa asidi, gesi hizi hutoka na kuja mdomoni na kusababisha harufu mbaya. Mtu wa hivi hata apige mswaki tatizo lake bado haliishi. Maana shida ipo tumboni. Dawa ni kupunguza ulaji wa vyakula vigumu kumengenya kama nyama ngumu au kupata dawa za kusaidia umeng'enyaji.

VIDONDA VYA TUMBO NA UPUNGUFU WA ACID.
Inasemekana wadudu wanaosababisha vidonda vya tumbo husababisha kuta za tumbo zisitengeneze asidi ya kutosha. Kwa hiyo wagonjwa wengi wa vidonda vya tumbo huwa na kiasi kidogo cha asidi. Lakini wengi huwa wanapewa dawa za kupunguza asidi( zinasaidia kupunguza asidi kuchoma vidonda na kufanya vipone haraka) japo zinafanya tatizo la upungufu wa asidi kuwa baya zaidi.

SABABU YA UPUNGUFU WA ASIDI TUMBONI
Mbali na wadudu wa vidonda vya tumbo, sababu nyingine ambayo ni kubwa sana ni maumbile na magonjwa mengineyo. Kuna watu wameumbwa na matumbo yasiyoweza kutengeneza asidi ya kutosha tumboni.

UTAJUAJE UNA ASIDI KIDOGO TUMBONI
Mbali na kuangalia dalili hizo na vipimo vya hospitali, mtu unaweza kuangalia kama unaupungufu wa asidi tumboni hata ukiwa nyumbani. Chukua maji kwenye kikombe kama ml 125. Changanya na robo kijiko cha baking soda na unywe. Ukiona dakika tatu hadi tano zimepita bila kubeua jua kuwa una tatizo la upungufu wa asidi.

MATIBABU
Hospitali kuna njia na dawa mbalimbali za kutibu upungufu wa asidi kulingana na chanzo chake.
 
Upotoshaji upotoshaji, upotoshaji, upotoshaji.

Unapoandika kitu hasa afya tips hakikisha unauelewa mzuri.

Gas na acid kuzidi tumboni ndio tatizo Kubwa Sasa hivi na siyo upungufu.

Watu wanapaswa kutumia Acid controller tablets ili kujikinga kupatwa na Vidonda Vya Tumbo.
 
Tueleze na ww tujue wapi katupotosha, ili wadau na sisi tuelimike

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Dah! Mi kiungulia kinanisumbua sana hasa nikila dagaa au soda ila sina vidonda vya tumbo na dawa yangu ya kutuliza hii hali huwa ni omeplazoo au sometimes natumia majivu tu.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
sawa tumekuelewa mkuu lakini kati ya asidi kuzidi tumboni na asidi kupungua tumboni kipi kina madhara zaidi
 
Kwa siku mwili wa binadamu unatengeneza kiasi cha asidi kati ya lita 1 hadi 1.5. Yaani ile asidi ya kujaa kopo kubwa la maji la lita 1.5! Asidi hiyo ni nyingi na kali sana. Ukali wake unafika PH ya 1.5. Manyama, matobolwa, samaki, minyofoo, pweza, vyakula vyote vigumu na laini husagwa na asidi. Mbali na hilo pia huua vijidudu vilivyoingia na chakula na kuweka mazingira mazuri kwa vimeng'enya vya tumboni kufanya kazi yake vyema.

TATIZO LA UKOSEFU WA ASIDI NA KIUNGULIA(Reflux)
Tumbo limeumbwa kwa namna ambayo linaweza kuhimili asidi hiyo kali. Kuta zake zipo imara na zina utando unaosaidia zisidhurike na asidi. Lakini huku juu kwenye koo la chakula kuta zake siyo imara kuweza kuhimili kiasi cha asidi iliyopo tumboni. Ndiyo maana kati ya tumbo na koo la chakula kuna valve ambayo inazuia asidi ya tumboni isipande juu kwenye koo la chakula. Valve hii hujifunga vyema pale kiasi cha asidi tumboni kinapokuwa juu.

Ikitokea kiasi cha asidi tumboni kikashuka valve hii hulegea na hivyo kufanya vitu vya tumboni kupanda juu kwenye koo la chakula. Asidi hii japo haina nguvu lakini kwa mazingira ya koo la chakula na hata mdomoni ni asidi kali sana. Ndiyo maana huwa inachoma kifuani na ikifika mdomoni inaleta uchachu mkali.

Kwa haraka haraka unawza dhani asidi imezidi tumboni ndiyo maana umepata tatizo hilo kumbe ni kinyume chake.

Mara nyingi tatizo hili hutibiwa kwa dawa za kupunguza asidi. Dawa(kama 'magnesium' )hizi zinasaidia ili kulinda koo la chakula lisiathiriwe na asidi na kuleta matatizo kama kansa ya koo na hata kuharibu meno. Lakini kutibu tatizo hili kwa namna hii huongeza tatizo la upungufu wa asidi tumboni. Hapo inatokea cyle mbaya ya kutibu-tatizo kuongeza tatizo.

UPUNGUFU WA ASIDI NA TUMBO KUJAA
Upungufu wa asidi tumboni husababisha chakula kukaa tumboni kwa muda mrefu sababu hakimeng'enywi haraka. So tumbo kujaa jaa na kutuna inaweza kuwa sababu ya upungufu wa asidi tumboni.

UPUNGUFU WA ASIDI NA KUNUKA MDOMO
Asidi ikiwa chini maana yake vyakula vigumu kama nyama vitachukua muda mrefu sana au havitavunjwa vunjwa. Jambo hili litafanya vyakula hivi vianze kuliwa na bakteria wa tumboni na kuvunda. Bakteria hawa katika kula huko chakula hutokeza gesi mbalimbali. Sasa kwa kuwa valve kati ya tumbo na koo la chakula imelegea sababu ya upungufu wa asidi, gesi hizi hutoka na kuja mdomoni na kusababisha harufu mbaya. Mtu wa hivi hata apige mswaki tatizo lake bado haliishi. Maana shida ipo tumboni. Dawa ni kupunguza ulaji wa vyakula vigumu kumengenya kama nyama ngumu au kupata dawa za kusaidia umeng'enyaji.

VIDONDA VYA TUMBO NA UPUNGUFU WA ACID.
Inasemekana wadudu wanaosababisha vidonda vya tumbo husababisha kuta za tumbo zisitengeneze asidi ya kutosha. Kwa hiyo wagonjwa wengi wa vidonda vya tumbo huwa na kiasi kidogo cha asidi. Lakini wengi huwa wanapewa dawa za kupunguza asidi( zinasaidia kupunguza asidi kuchoma vidonda na kufanya vipone haraka) japo zinafanya tatizo la upungufu wa asidi kuwa baya zaidi.

SABABU YA UPUNGUFU WA ASIDI TUMBONI
Mbali na wadudu wa vidonda vya tumbo, sababu nyingine ambayo ni kubwa sana ni maumbile na magonjwa mengineyo. Kuna watu wameumbwa na matumbo yasiyoweza kutengeneza asidi ya kutosha tumboni.

UTAJUAJE UNA ASIDI KIDOGO TUMBONI
Mbali na kuangalia dalili hizo na vipimo vya hospitali, mtu unaweza kuangalia kama unaupungufu wa asidi tumboni hata ukiwa nyumbani. Chukua maji kwenye kikombe kama ml 125. Changanya na robo kijiko cha baking soda na unywe. Ukiona dakika tatu hadi tano zimepita bila kubeua jua kuwa una tatizo la upungufu wa asidi.

MATIBABU
Hospitali kuna njia na dawa mbalimbali za kutibu upungufu wa asidi kulingana na chanzo chake.
Sasa hiyo acid Lita nzima mbona mbegu za mapera na tikiti nakunya hivyohivyo au Nina uhaba wa acid
 
Back
Top Bottom