Magonjwa ya Koo, Tumbo, Figo na Ini husababisha mdomo kunuka

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,622
Je Wajua? Baadhi ya Magonjwa ya Koo, Njia ya Hewa, Mfumo wa Tumbo, Figo na Kisukari husababisha Kinywa kutoa Harufu Mbaya

Watu wenye Kisukari wanaweza kuwa na kiwango kikubwa cha Sukari kwenye mate yao, ambayo husababisha bakteria wa mdomoni kuzalisha Kemikali zinazosababisha harufu mbaya.

Matezi 'tonsilitis', Uvimbe wa Koo, Uvimbe wa Pua, huweza kusababisha kinywa kutoa harufu mbaya kutokana na kuvuja kwa uchafu unaotokana na maambukizi

Uvimbe wa njia ya hewa au Pneumonia huweza kusababisha kinywa kutoa harufu mbaya kutokana na kuvuja kwa usaha au uchafu kutoka kwenye njia ya hewa.

Vidonda vya Tumbo na gastroesophageal reflux disease (GERD) au matatizo ya Ini huweza kusababisha kinywa kutoa harufu mbaya kutokana na asidi au kemikali zinazopanda kutoka tumboni

Matatizo ya Figo vile Chronic Kidney Disease (CKD) yanaweza kusababisha kinywa kutoa harufu mbaya kutokana na Kemikali zinazotolewa kupitia Mkojo.

Ni muhimu kuhakikisha kwamba unapata matibabu sahihi kwa magonjwa haya ili kupunguza au kuzuia kinywa kutoa harufu mbaya. Kwa hiyo, ni vizuri kushauriana na daktari wako ili kupata ushauri na matibabu sahihi.

Mtandao
 
Mi huwa naona asilimia kubwa ni wababu ndiyo husmell vibaya sana
 
Back
Top Bottom