Faida sita kubwa za kula ndizi mbivu na angalizo la kutokuweka ndizi kwenye friji

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose, Fructose na Glucose na pia ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre), ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.

Pia, ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi ya muda wa dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu. Ndizi husaidia masuala mbalimbali
katika mwili wa binadamu ambazo ni;

1. MFADHAIKO WA AKILI (DEPRESSION)
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha Afya ya Akili cha Taifa (MIND) nchini Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, wengi waliondokana na tatizo hilo na
kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu.

Hali hii inatokana na ukweli kwamba, ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.

2. MATATIZO WAKATIWA HEDHI (PMS)
Kama wewe ni miongoni mwa kinamama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza kupona. Vitamin B6 vilivyomo katika ndizi, hurekebisha kiwango cha sukari ambacho huathiri hali ya mtu.

3. UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)
Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upungufu wa damu kwa sababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.

4. SHINIKIZO LA DAMU
Tunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango kikubwa cha madini уа potasiamu (potassium) na
wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha chumvi (sodium), hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.

Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka Dawa na Chakula ya nchi ya Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaii wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.

5. NGUVU YA AKILI
Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa
kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wa chakula cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao.

Utafiti unaonesha kuwa, potasiamu iliyojazana katika ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha uwezo wake wa kulisomea.

6. MZIO (HANGOVER)
Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover), ni kunywa 'Milkshake' iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa па
asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua katika damu wakati maziwa hutuliza na kurejesha maji katika mfumo wake. Pia, husaidia matatizo mengine kama vile kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo, kuondoa asidi tumboni, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo ya moyo, n.k.

Hivyo, ndizi ni tiba ya magoniwa mengi na ni bora. Ukiilinganisha na apple (tufaa) ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili, vitamini A na chuma mara tano, na madini mengine mara mbili zaidi ya apple.

MWISHO:
Unashauriwa kutokuweka ndizi katika Jokofu.
 
Tatizo ndizi zenyewe siku hizi zishachakachuliwa ni ndizi za Maabara so sijui kama hizo faida Bado zimo

Ndizi asili upatikanaji wake ushaanza kuwa mtihani

Ukienda kununua ukiuliza Vipi hizi ndizi ni za kisasa au kienyeji? fasta tu anakujibu za kienyeji, Sasa nenda ukale yani utadhan unakula makande ya Mkoa ule
 
Majibu mengi ya faida za ndizi yanapatikana Bukoba, Mbeya na Moshi.
 
safi sana! Siku hizi nimejiwekea utaratibu wa kula ndizi kadhaa kiasi cha kushiba japo ndizi si tunda la asili yangu na halilimwi nilikozaliwa ila ndio msosi wangu wa nguvu, nakula sahani imejaa
 
Kwenye majamboz ndizi inasaidia sana, kitu hichoo! Kinakuwa mnara, shoo unapiga mpaka unasema asante
 
Yule janabi wa jkci anasema sukari ya kwenye matunda ndio mbaya zaidi kuliko artificial. Yeye anasema tangu 1998 anakunywa maji tu maana vyakula vyote ni sumu.
Anakunywa maji pasipo kula chakula kingine chochote ama vipi? Ufafanuzi ndugu
 
Yule janabi wa jkci anasema sukari ya kwenye matunda ndio mbaya zaidi kuliko artificial. Yeye anasema tangu 1998 anakunywa maji tu maana vyakula vyote ni sumu.
Jamaa ni wa kupuuza.

Ukimsikiliza sana ndo utapata hicho kisukari na utakufa kweli kwa magonjwa ya moyo!
 
Yule janabi wa jkci anasema sukari ya kwenye matunda ndio mbaya zaidi kuliko artificial. Yeye anasema tangu 1998 anakunywa maji tu maana vyakula vyote ni sumu.

Diet plan n ngumu sana,nafkir kila chakula kitumike kwa kias na kwa uangalifu mkubwa..tumepewa maisha na vyakula tuvifurahie hvyo n busara vikatumika kwa utaratibu vingnevyo n ngumu sana kuacha wanga sukar kwa maisha yako yote
 
Back
Top Bottom