Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,650
- 218,121
Leo Jumamosi Okt. 23, 2021 Jeshi la Magereza limewazuia watu wote waliokwenda Gereza la Ukonga kumwona Mhe. Freeman Mbowe kwa kile walichodai kuwa wamepokea maelekezo Ila hawasemi yametoka kwa nani. Ikumbukwe kuwa ni siku rasmi ya kutembelea Mahabusu na Wafungwa.
Askari Magereza walitoa agizo kwa watu waliofika Gereza la Ukonga kuwaona Mahabusu na Wafungwa kusubiri nje ya gereza mpaka utaratibu utakapokamilika. Wakati wakisubiri utaratibu magari ya Polisi yaliwasili na kuwakata kutawanyika, Jeshi hilo lilidai ni mkusanyiko usio halali.
Baada ya kauli ya Jeshi la Polisi, watu walichukua hatua ya kuingia ndani ya geti la gereza na kufuata utaratibu wa kujiandikisha ili kumwona mwenyekiti. Askari magereza waliwatenga wote waliokuja kumwona Mhe. Freeman Mbowe na kuwambiwa wanatakiwa kuwa na kibali cha kumwona.