Msemaji wa Magereza aanika sababu Makada wa CHADEMA kuzuiwa kumuona Mbowe

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Dar es Salaam. Baadhi ya makada wa Chadema waliofika kumuona Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe juzi katika gereza Ukonga jijini Dar es Salaam, hawakutimiza lengo lao baada ya askari Magereza waliokuwa getini kuwazuia wakisema kuwa wamepata maelekezo kutoka juu.

Hata hivyo, Msemaji wa Magereza Kamishna Msaidizi, Justin Kaziulaya alipoulizwa kwa simu jana alikiri kuwazuia akisema ni kutokana na idadi yao kuwa kubwa jambo alilosema linaakiuka masharti ya kupambana na maambukizo ya Uviko-19.

“Ukiangalia kwa haraka haraka picha za watu walioenda kumuona Mbowe jana, Mkuu wa Gereza alikuwa anatekeleza maagizo ambayo yanafuatwa kwa magereza yote nchini na sio kwa mhalifu fulani,” alisema.

Mbowe alikamatwa Julai 30 jijini Mwanza na kuunganishwa na wenzake watatu katika kesi inayohusisha kupanga njama za kufanya ugaidi inayoendelea kusikilizwa na Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia taarifa hizo kwa simu, Mkurugenzi wa Uhusiano, Itifaki na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema hatua ya kuwazuia kumwona Mwenyekiti wao inazua hofu kuhusu hali yake.

“Walisema kuwa wanaoruhusiwa ni wenye vibali tu, jambo ambalo sio sahihi kwani siku za mwisho mwa juma na sikukuu ni siku ya kutembelea wafungwa na mahabusu.

“Wenye vibali wanaweza kwenda siku yoyote kama ambavyo Mawakili wanaweza kwenda Gerezani siku yoyote,” alisema.

Mrema aliwataja waliozuiwa ni John Heche, Julius Mwita na wagombea Ubunge wa mwaka 2020 kutoka majimbo mbalimbali nchini na wanachama wengine wa Mkoa wa Dar es Salaam na hata walipoomba kumuona Mkuu wa gereza hawakufanikiwa kwa hoja kwamba yuko kwenye kikao.

Alisema iliwafanya kukaa pale mpaka mchana na kulazimika kuondoka bila kumuona.

Chanzo:
Mwananchi
 
Wanataka kwenda kuleta fujogerezani hao watu wote hao mkarundikane gerezani wakati kuna covid 19? kwanini wasiende mmojammoja waache uhuni wao
 
Yaani CHADEMA wamekalia kutaka kushindana na serikali tu kilasiku wanataka waandikwe magazetini na kuitisha presszisizo na maana
 
Dar es Salaam. Baadhi ya makada wa Chadema waliofika kumuona Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe juzi katika gereza Ukonga jijini Dar es Salaam...
Asante kazi ulaya sisi tunamtaka kazibongo Sasa ili tumalizane na kadhia za ubambikaji na ijazaji magereza .
 
Hata ningekuwa mimi ndio nalinda Magereza nisinge ruhusu watu kujazana. Eti kumuona mtuhumiwa, kwani magereza imekuwa Hospitalini?!

Magereza ni sehemu nyeti sana lazima iwe na mipaka na masharti bila kujali nani atasema nini! Hiyo ni sehemu inayo hifadhi wahalifu wa kila aina hivyo usalama wa magereza ni muhimu zaidi kuliko vikundi vinavyo enda kumuona Mbowe.

Lazima magereza wawe imara, kamwe wasikubali hawa watu/vikundi wakapanda kichwani, ni hatari. Sio mbowe tu aliyepo hapo magereza wapo wengi, hivyo lazima utaratibu uzingatiwe sawa kwa wote.
 
wanataka kwenda kuleta fujogerezani hao watu wote hao mkarundikane gerezani wakati kuna covid 19? kwanini wasiende mmojammoja waache uhuni wao
Inatakiwa kichwa kiwe tupu ndiyo unaweza kuwa na mawazo ya namba hii.

COVID gani tena jamani wakati jana uwanja wa Mkapa watu walijazana ,pia mwenyekiti wenu juzi kule Moshi ali kuwa na msafara wa magali zaidi ya 50
 
Mrema aliwataja waliozuiwa ni John Heche, Julius Mwita na wagombea Ubunge wa mwaka 2020 kutoka majimbo mbalimbali nchini na wanachama...
Masikini anavyojigonga utafikiri kinyeo kinamuwasha! oh corona oh maagizo khaa! Magufuli is alive and active!!
 
yaani chadema wamekalia kutaka kushindana na serikali tu kilasiku wanataka waandikwe magazetini na kuitisha presszisizo na maana
Acha kujitoa ufahamu. Kuna siku itakuwa upande wako. Kama sio gerezani basi hospitali.
 
Back
Top Bottom