DOKEZO Inadaiwa Askari Magereza wa Ukonga wanajigharamikia wenyewe wanaposafirisha Wafungwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwandishi katika moja ya magazeti hapa Nchini Tanzania na memba wa miaka mingi wa Jamii Forums, katika majukumu yangu nimefanikiwa kupata nafasi ya kuandika makala na habari mbalimbali za kijamii, kuna hii moja kuhusu Jeshi la Magereza, nilivyomgusia Mhariri wangu akakataa kuitumia.

Nikaona kuliko kuwa kimya bora na kwa kuwa nimeshaifanya bora nitumie platform ya JF kufikisha ujumbe huu hata kama sitajulikana lakini naamini nitakuwa nimewasaidia Watanzania wenzangu wengi kama mamlaka zitaamua kuchukua hatua:

Makala yenyewe inahusu hivi:
Baadhi ya Askari wa Magereza wa Gereza la Ukonga Jijini Dar es Salaam inadaiwa wanajigharamikia kuwasafirisha watuhumiwa kwenda mikoani bila kurejeshewa pesa zao kwa wakati huku wakidai kuna ubaguzi katika kulipa pesa hiyo.

Mmoja kati ya maofisa wa Gereza hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe amedai changamoto hiyo ni kubwa ambapo amedai wanaodai pesa yao ni wengi lakini hawana sehemu ya kueleza kero hiyo kwa kuwa mazingira yaliyopo ni kwamba Askari akikosoa suala hilo au kuhoji anatishiwa kuhamishwa kupelekwa maeneo ya pembezoni, hali hiyo imeendelea kuwafanya wawe na hofu ya kueleza changamoto zao.

"Malalamiko makubwa ambayo yapo kwetu ni kwamba tunadai kuanzia malipo yetu ya kuanzia Mwaka 2015 mpaka mwaka huu (2023) lakini inaonekana kwamba madeni ya 2015 yameshalipwa na yamefutwa lakini walilipwa watu wachache sana wengine hatukulipwa" ameeleza Ofisa huyo.

Anaendelea kueleza "Na sasa hivi wanasema watalipa madeni kwamba waliomba Shilingi Bilioni 6 lakini wamepewa Shilingi Bilioni 3, cha kushangaza mfano mimi kuna watu unaweza kwenda nao safari wao wanalipwa baada ya kutumia gharama zao lakini wewe ulipwi miaka na miaka.

“Wanaopewa kipaumbele cha kulipwa kama mkisafiri nao mara nyingi ni wale Maafisa wakubwa lakini wenzangu na mimi huku chini Mungu saidia.

“Hakuna sababu za wazi kwa nini hawatulipi, tunahisi kuna upigaji maana wanajua hakuna wa kusema popote huo ndio utamaduni uliojengwa.

"Yaani kinachoonekana zile hela zimeshatolewa lakini watu wamezipiga na kila tunapojaribu kuhoji chinichini tunatishiwa kuhamishwa kupelekwa porini ambako huwezi kuonana na mtu yeyote anayeweza kukusaidia.

"Tunaomba mtusaidie sisi kupaza sauti hatuna pa kusemea tunapokuwa tunasema wanatukandamiza tunaonekana kabisa tunaonewa na ukitaka kusema utaambiwa askari unatakiwa kuwa mvumilivu.

"Mfano inapotokea unampeleka mtuhumiwa Tabora, Mwanza, Mbeya, Kagera au Rukwa yule mtuhumiwa analipiwa nauli na kila kitu na Serikali lakini mimi nauli najigharamikia, hela ya gesti mimi, nauli na chakula kila kitu mimi unakuta tayari nimeshadhulumu familia yangu kisha malipo yenyewe yanakaa kwa muda mrefu.

“Unaweza kukuta yamekaa miaka saba ndio mnakuja kulipwa na kulipwa kwenyewe hamlipwi madeni yote," anasema Ofisa huyo.

Anadai kuwa changamoto hiyo pia ipo kwenye baadhi ya magereza mengine yaliyopo Nchini.

Katika kufahamu sababu ambazo upelekea watuhumiwa kutumia usafiri wa umma Ofisa huyo anasema "Kulingana na kwamba magari ni shida tunatumia mabasi na tunalipa nauli kutoka mifukoni mwetu."

Aidha, Ofisa mwingine (jina kapuni) kutoka Gereza la Ukonga amedai changamoto hiyo ipo lakini kumekuwepo na hofu kubwa ya wadai kuchukua hatua kutokana na mazingira yanayowazunguka.

"Hili jambo tungekuwa kwenye sekta nyingine lingeshasikika sana lakini huku sisi hatuna sauti, tunaumia sana, wanakwambia uende na risiti, lakini inapita miaka bila kulipwa, tunavunjika moyo tunaomba mtusemee sisi huku hatuwezi kusema utaamka asubuhi umeamishwa."

Naongeza kuwa kutokana kuwepo kwa utamaduni wa hofu imepelekea pia baadhi ya Askari Magereza kukosa pesa za likizo pamoja na pesa nyingine ambazo hutakiwa kutolewa kwa nyakati tofauti kulingana na taratibu.
 
hiyo wizara imejaaa vibaka tupu.kawekwa huyo amee hajui hata kufoka amepooza kama udenda wa mgonjwa.

kuna wizara huwa zinapewa watu waliouzubaa kimkakati.

by the way wenye kuamua swala hilo ni askari wenyewe,huwezi isaidia serikali iliyojisahau kwenye majukumu yake halafu ukaanza kulalamika.
 
Naweza kuungana na wewe.Hii tabia ya Polisi kuishiwa mafuta na kuja kuomba kwenye taasisi imekithiri.

Serikali na Wizara ya mambo ya ndani mna mambo ya kipumbavu sana yaani idara nyeti za ulinzi wa raia zinaishiwa vitu vya msingi kama hivyo? Angalia hata magari ya Polisi nk vimechakaa hatari.

Kwa nini Serikali hamuwatengei Jeshi la Polisi mahitaji Yao na kuleta Kwa wakati.?
 
Kama wewe ni mwandishi ni wazi unafahamu fika mhariri ana haki ya kukataa sababu ni stori ya upande mmoja. Uonevu mnaofanyiwa ni sababu ya kukosa kuwa na umoja.

Ushauri wangu ni mgumu ila ndio utakaoweza kuwasaidia; kwa magereza ya Dar es salaam na mikoani nyie wenye vyeo vya chini hakikisheni siku moja mnafanya uamuzi mgumu ambao matokeo yake yatakuwa ni GUMZO LA KITAIFA.

WAACHENI WAFUNGWA NA MAHABUSU WAWE HURU.

Matokeo yake yatakuwa ni uwajibikaji jumuishi na hakuna atakayekuwa msafi na kuweza kumuwajibisha mwenzake.

Am sure baada ya andiko hili na kabla ya ushauri wangu wa kipuuzi haujaanza kufanyiwa kazi na kutekelezwa mamlaka husika zitajipanga kuwalipa stahiki zenu na haki zenu.
 
hiyo wizara imejaaa vibaka tupu.kawekwa huyo amee hajui hata kufoka amepooza kama udenda wa mgonjwa.

kuna wizara huwa zinapewa watu waliouzubaa kimkakati.

by the way wenye kuamua swala hilo ni askari wenyewe,huwezi isaidia serikali iliyojisahau kwenye majukumu yake halafu ukaanza kulalamika.
Wizara Ya Ajabu Ambayo Ina Majeshi Ya Ajabu
Jeshi La Police
Jeshi La Uhamiaji
Jeshi La Zimamoto

Yaani Kuna Shida
 
Ukitaka ufilisike fanya kazi supply na Magereza nndio utakuwa mwisho wako.....utafilisika .....askari hata uniform zao wananunua wenyewe kutoka bohari
....
Huko no uozo mtupu ....sikia tu ....police nako wanapiga hivyo hivyo......hadi Waziri wao kapiga juzi tu kupitia mkewe....chezea home boy wa mama ?
 
Siyo hao tu civil servants wengi wanajitolea sana nchi hii chini ya kivuli cha uzalendo, kuonekana au promosheni. Na mwisho wanaambulia kikokotoo cha utosi.

Wabunge na Mawazri ndiyo wanaolipwa vizuri ndiyo maana leo Kila mtu anakmbilia siasa.
 
Ukitaka ufilisike fanya kazi supply na Magereza nndio utakuwa mwisho wako.....utafilisika .....askari hata uniform zao wananunua wenyewe kutoka bohari
....
Huko no uozo mtupu ....sikia tu ....police nako wanapiga hivyo hivyo......hadi Waziri wao kapiga juzi tu kupitia mkewe....chezea home boy wa mama ?
Bhalaa Sana Yaani Sijui Nini
Msukuma Anasema Mnasoma Mje Mtuibie

Wizara Hiyo Imejaa Makandokando
 
Mimi ni mwandishi katika moja ya magazeti hapa Nchini Tanzania na memba wa miaka mingi wa Jamii Forums, katika majukumu yangu nimefanikiwa kupata nafasi ya kuandika makala na habari mbalimbali za kijamii, kuna hii moja kuhusu Jeshi la Magereza, nilivyomgusia Mhariri wangu akakataa kuitumia.

Nikaona kuliko kuwa kimya bora na kwa kuwa nimeshaifanya bora nitumie platform ya JF kufikisha ujumbe huu hata kama sitajulikana lakini naamini nitakuwa nimewasaidia Watanzania wenzangu wengi kama mamlaka zitaamua kuchukua hatua:

Makala yenyewe inahusu hivi:
Baadhi ya Askari wa Magereza wa Gereza la Ukonga Jijini Dar es Salaam inadaiwa wanajigharamikia kuwasafirisha watuhumiwa kwenda mikoani bila kurejeshewa pesa zao kwa wakati huku wakidai kuna ubaguzi katika kulipa pesa hiyo.

Mmoja kati ya maofisa wa Gereza hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe amedai changamoto hiyo ni kubwa ambapo amedai wanaodai pesa yao ni wengi lakini hawana sehemu ya kueleza kero hiyo kwa kuwa mazingira yaliyopo ni kwamba Askari akikosoa suala hilo au kuhoji anatishiwa kuhamishwa kupelekwa maeneo ya pembezoni, hali hiyo imeendelea kuwafanya wawe na hofu ya kueleza changamoto zao.

"Malalamiko makubwa ambayo yapo kwetu ni kwamba tunadai kuanzia malipo yetu ya kuanzia Mwaka 2015 mpaka mwaka huu (2023) lakini inaonekana kwamba madeni ya 2015 yameshalipwa na yamefutwa lakini walilipwa watu wachache sana wengine hatukulipwa" ameeleza Ofisa huyo.

Anaendelea kueleza "Na sasa hivi wanasema watalipa madeni kwamba waliomba Shilingi Bilioni 6 lakini wamepewa Shilingi Bilioni 3, cha kushangaza mfano mimi kuna watu unaweza kwenda nao safari wao wanalipwa baada ya kutumia gharama zao lakini wewe ulipwi miaka na miaka.

“Wanaopewa kipaumbele cha kulipwa kama mkisafiri nao mara nyingi ni wale Maafisa wakubwa lakini wenzangu na mimi huku chini Mungu saidia.

“Hakuna sababu za wazi kwa nini hawatulipi, tunahisi kuna upigaji maana wanajua hakuna wa kusema popote huo ndio utamaduni uliojengwa.

"Yaani kinachoonekana zile hela zimeshatolewa lakini watu wamezipiga na kila tunapojaribu kuhoji chinichini tunatishiwa kuhamishwa kupelekwa porini ambako huwezi kuonana na mtu yeyote anayeweza kukusaidia.

"Tunaomba mtusaidie sisi kupaza sauti hatuna pa kusemea tunapokuwa tunasema wanatukandamiza tunaonekana kabisa tunaonewa na ukitaka kusema utaambiwa askari unatakiwa kuwa mvumilivu.

"Mfano inapotokea unampeleka mtuhumiwa Tabora, Mwanza, Mbeya, Kagera au Rukwa yule mtuhumiwa analipiwa nauli na kila kitu na Serikali lakini mimi nauli najigharamikia, hela ya gesti mimi, nauli na chakula kila kitu mimi unakuta tayari nimeshadhulumu familia yangu kisha malipo yenyewe yanakaa kwa muda mrefu.

“Unaweza kukuta yamekaa miaka saba ndio mnakuja kulipwa na kulipwa kwenyewe hamlipwi madeni yote," anasema Ofisa huyo.

Anadai kuwa changamoto hiyo pia ipo kwenye baadhi ya magereza mengine yaliyopo Nchini.

Katika kufahamu sababu ambazo upelekea watuhumiwa kutumia usafiri wa umma Ofisa huyo anasema "Kulingana na kwamba magari ni shida tunatumia mabasi na tunalipa nauli kutoka mifukoni mwetu."

Aidha, Ofisa mwingine (jina kapuni) kutoka Gereza la Ukonga amedai changamoto hiyo hipo lakini kumekuwepo na hofu kubwa ya wadai kuchukua hatua kutokana na mazingira yanayowazunguka.

"Hili jambo tungekuwa kwenye sekta nyingine lingeshasikika sana lakini huku sisi hatuna sauti, tunaumia sana, wanakwambia uende na risiti, lakini inapita miaka bila kulipwa, tunavunjika moyo tunaomba mtusemee sisi huku atuwezi kusema utaamka asubuhi umeamishwa."

Naongeza kuwa kutokana kuwepo kwa utamaduni wa hofu imepelekea pia baadhi ya Askari Magereza kukosa pesa za likizo pamoja na pesa nyingine ambazo utakiwa kutolewa kwa nyakati tofauti kulingana na taratibu.

Hawa askari wanazulumu sana raia, nishawahi enda magereza kipindi cha Magufuli one weekend (nayo ilikuwa zuluma na figisi za askari)

Wacha waonje tabu ya zuluma!

Wazulumiwe tu.
 
huwezi jua madhara ya wao kudhurumiwa na serikali yao mpaka watakapoamua kujilipa kupitia wewe.
 
Naweza kuungana na wewe.Hii tabia ya Polisi kuishiwa mafuta na kuja kuomba kwenye taasisi imekithiri.

Serikali na Wizara ya mambo ya ndani mna mambo ya kipumbavu sana yaani idara nyeti za ulinzi wa raia zinaishiwa vitu vya msingi kama hivyo? Angalia hata magari ya Polisi nk vimechakaa hatari.

Kwa nini Serikali hamuwatengei Jeshi la Polisi mahitaji Yao na kuleta Kwa wakati.?
Serikali pesa inatoka ila washenzi wachache wanaziminya na kutisha watu.
....Hili suala kila kona lipo hata makazni stahiki unazungushwa mwaka na zipo katika bajeti wanaweka fixed account wapate kidogo
 
Mafuta ya taasisi nani anayaminya?

Yaani usafirishaje mfungwa Kwa pesa Yako ya mfukoni?
 
Hizo Kazi za kukaa na wafungwa ni ngumu Sana na mshahara Mdogo hivyo serikali ijitafakari. Haki ya Mtu ni muhimu Nina imani Mama atalifanyia Kazi hili Jambo.
 
Mimi ni mwandishi katika moja ya magazeti hapa Nchini Tanzania na memba wa miaka mingi wa Jamii Forums, katika majukumu yangu nimefanikiwa kupata nafasi ya kuandika makala na habari mbalimbali za kijamii, kuna hii moja kuhusu Jeshi la Magereza, nilivyomgusia Mhariri wangu akakataa kuitumia.

Nikaona kuliko kuwa kimya bora na kwa kuwa nimeshaifanya bora nitumie platform ya JF kufikisha ujumbe huu hata kama sitajulikana lakini naamini nitakuwa nimewasaidia Watanzania wenzangu wengi kama mamlaka zitaamua kuchukua hatua:

Makala yenyewe inahusu hivi:
Baadhi ya Askari wa Magereza wa Gereza la Ukonga Jijini Dar es Salaam inadaiwa wanajigharamikia kuwasafirisha watuhumiwa kwenda mikoani bila kurejeshewa pesa zao kwa wakati huku wakidai kuna ubaguzi katika kulipa pesa hiyo.

Mmoja kati ya maofisa wa Gereza hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe amedai changamoto hiyo ni kubwa ambapo amedai wanaodai pesa yao ni wengi lakini hawana sehemu ya kueleza kero hiyo kwa kuwa mazingira yaliyopo ni kwamba Askari akikosoa suala hilo au kuhoji anatishiwa kuhamishwa kupelekwa maeneo ya pembezoni, hali hiyo imeendelea kuwafanya wawe na hofu ya kueleza changamoto zao.

"Malalamiko makubwa ambayo yapo kwetu ni kwamba tunadai kuanzia malipo yetu ya kuanzia Mwaka 2015 mpaka mwaka huu (2023) lakini inaonekana kwamba madeni ya 2015 yameshalipwa na yamefutwa lakini walilipwa watu wachache sana wengine hatukulipwa" ameeleza Ofisa huyo.

Anaendelea kueleza "Na sasa hivi wanasema watalipa madeni kwamba waliomba Shilingi Bilioni 6 lakini wamepewa Shilingi Bilioni 3, cha kushangaza mfano mimi kuna watu unaweza kwenda nao safari wao wanalipwa baada ya kutumia gharama zao lakini wewe ulipwi miaka na miaka.

“Wanaopewa kipaumbele cha kulipwa kama mkisafiri nao mara nyingi ni wale Maafisa wakubwa lakini wenzangu na mimi huku chini Mungu saidia.

“Hakuna sababu za wazi kwa nini hawatulipi, tunahisi kuna upigaji maana wanajua hakuna wa kusema popote huo ndio utamaduni uliojengwa.

"Yaani kinachoonekana zile hela zimeshatolewa lakini watu wamezipiga na kila tunapojaribu kuhoji chinichini tunatishiwa kuhamishwa kupelekwa porini ambako huwezi kuonana na mtu yeyote anayeweza kukusaidia.

"Tunaomba mtusaidie sisi kupaza sauti hatuna pa kusemea tunapokuwa tunasema wanatukandamiza tunaonekana kabisa tunaonewa na ukitaka kusema utaambiwa askari unatakiwa kuwa mvumilivu.

"Mfano inapotokea unampeleka mtuhumiwa Tabora, Mwanza, Mbeya, Kagera au Rukwa yule mtuhumiwa analipiwa nauli na kila kitu na Serikali lakini mimi nauli najigharamikia, hela ya gesti mimi, nauli na chakula kila kitu mimi unakuta tayari nimeshadhulumu familia yangu kisha malipo yenyewe yanakaa kwa muda mrefu.

“Unaweza kukuta yamekaa miaka saba ndio mnakuja kulipwa na kulipwa kwenyewe hamlipwi madeni yote," anasema Ofisa huyo.

Anadai kuwa changamoto hiyo pia ipo kwenye baadhi ya magereza mengine yaliyopo Nchini.

Katika kufahamu sababu ambazo upelekea watuhumiwa kutumia usafiri wa umma Ofisa huyo anasema "Kulingana na kwamba magari ni shida tunatumia mabasi na tunalipa nauli kutoka mifukoni mwetu."

Aidha, Ofisa mwingine (jina kapuni) kutoka Gereza la Ukonga amedai changamoto hiyo hipo lakini kumekuwepo na hofu kubwa ya wadai kuchukua hatua kutokana na mazingira yanayowazunguka.

"Hili jambo tungekuwa kwenye sekta nyingine lingeshasikika sana lakini huku sisi hatuna sauti, tunaumia sana, wanakwambia uende na risiti, lakini inapita miaka bila kulipwa, tunavunjika moyo tunaomba mtusemee sisi huku atuwezi kusema utaamka asubuhi umeamishwa."

Naongeza kuwa kutokana kuwepo kwa utamaduni wa hofu imepelekea pia baadhi ya Askari Magereza kukosa pesa za likizo pamoja na pesa nyingine ambazo utakiwa kutolewa kwa nyakati tofauti kulingana na taratibu.
Wakiambiwa ni wizara ya form four failures wanawaka, ndiyo maana hata wakipewa budget nzima ya nchi hawatafanikiwa
 
Back
Top Bottom