KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Mada yako inalenga uchokonozi tu.Cha ajabu baada ya Mbowe kutoka jela amekuwa hana tena msisitizo wa kuzungumzia katiba mpya, hata anapopata nafasi ya kuongea ni kama anakwepakwepa kuzungumzia katiba mpya.
Aliyoyaeleza Mbowe baada ya kukutana na Samia hukuyaelewa?
Kwa hiyo kwa maoni yako unataka CHADEMA wafanye kana kwamba hapakuwepo kabisa na mazungumzo kati ya Mwenyekiti wao na Rais na kukawa na mambo waliyokubaliana?
Hawakupeana muda, kuona jinsi hali itakavyoendelea baada ha mkutano huo?
Wape muda CHADEMA, wachambue mambo yao vizuri. Wamepitia katika hali ngumu sana, na wakati wote huo baadhi ya watu wakiwacheka na kuwaona kama wapuuzi.
Sasa inapojitokeza nafasi nzuri ya kuonyesha ukomavu wao, baadhi ya watu hawa wanataka chama hicho kirukeruke kama hawana akili? Na hawa watu ndio watakaokuwa mbele kusema, si mnawaona CHADEMA wasivyoweza kujiheshimu?
Wape muda wayapime waliyoahidiwa, na wakiona ni maneno matamu yanayolenga kupoteza muda, hapo wasipozinduka, lawama iwaandame.