Watu wa zamani walipandishaje yale mawe ya tani 4 ghorofani pasipo crane?

Huna haja ya kwenda mbali jiulize tu Reli ya kati wakati inajengwa enzi za mjerumani kama kulikuwa na crane au Yale mataluma yalibebwa na waafrika enzi hizo ,sasa hivi kijana jabali kabisa katoka mkoani anatembeza soksi na boksa .Kiufupi binadamu nguvu na akili anayo basi tu.Hakuna kitu kinanikera kama kuona kijana mwenye nguvu zake eti anatembeza karanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungeshauri afanyaje mkuu?
 
Huko misri kuna pyramid kubwa ambazo juu zina mawe makubwa kukadiliwa uzito wa tan 4 na zilijengwa enzi za zamani kabla ya kuja mitambo ya kunyanyua vitu vizito (crane).

Hata pale Zanzibar ukipita baadhi ya mitaa utaona magofu ambayo juu kuna majabali ya mawe mazito na inasemekana ni watu wa kale waliyapandisha.

Je; watu Wa zamani waliwezaje kupandisha blocks/mawe mazito urefu wote huo bila kutumia crane? au walitumia ndumba?
View attachment 1019253
Mimi kinachonisikitisha in kuwa pyramids zimeweza kidumu takriban miaka 3000 iliyopita lakini ghotofa zetu zilizoplaniwa na mainjinia kwa teknolojia ya kisaa haziwezi kudumu hata karne mbili!
 
Mimi kinachonisikitisha in kuwa pyramids zimeweza kidumu takriban miaka 3000 iliyopita lakini ghotofa zetu zilizoplaniwa na mainjinia kwa teknolojia ya kisaa haziwezi kudumu hata karne mbili!
Ndo hapo sasa
 
Walitumia principle za physics
"Pulley system" ambayo ilikuepo tangu karne ya 17

Kwa sasa,
Pulley System imekua modified zaidi kuweza kuunda hizo cranes, lift Elevators n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uongo, kuna hii pia ukiweza kujibu basi pulleys zako zipo sahihi..
Kule Beirut, Lebanon
Kuna jengo maarufu kama "Baalbek" limewekwa jiwe juu lenye Tani 1600 na hilo lilivutwa na pulleys? Au...
Wengi mmekaririshwa na hizo degree za engineering na physics mnajiona mnajua, ujinga tu
Nyingine kule Peru, Machupichu wonders hebu fuatilia au zile Stone Henge kule Scotland.
Kwa taarifa yako hata zile pyramid za Giza kule Egypt zipo katikati kabisa ya dunia, je walijuaje na hapakuwa na satelite .
Tafakarini, acheni kujifanya mnajua
 
Mimi kinachonisikitisha in kuwa pyramids zimeweza kidumu takriban miaka 3000 iliyopita lakini ghotofa zetu zilizoplaniwa na mainjinia kwa teknolojia ya kisaa haziwezi kudumu hata karne mbili!
Umejuaje?, Hata haya maghorofa yatadumu maelfu ya miaka
 
Mkuu karne ya 17 sijuzi tu hapo ...pyramids zinazaidi ya miaka 4000 iliyopita
Anaongelea BC... Mfano karne ya 14BC ndo miaka hiyo ya akina moses, sasa 17BC itakua ama zama za mawe au bronze Age,, au zama za akina Abraham
 
Kabla ya kujiuliza hayo mawe yalipandishwaje hapo juu, jiulize yalitolewa/ yalichimbwa wapi?

Eneo ambalo limechimbwa 2.3 million m³ za mawe lazima wangekua wameshalipata kusupport hiyo theory ya ujenzi wa pyramids.

Kuna research wameitengenezea documentary kama ya masaa mawili wanaelezea theory ya matumizi ya solar lens katika ujenzi wa hizo pyramids. Nitaitafuta title ya hiyo documentary niiatach kwenye hii comment
 
Ndio ninyi mnaosoma history kwa dictionary halafu mnakuja kujaza matangopori humu!
Tuanze na mawe yenyewe tools gani enzi hizo (precision instruments) kama micrometer, zilitumika kupima, kuchonga au kuyakata na kuyasafirisha mawe yale hadi kwenye sites? Hao "wanaume" au watumwa wote kwa mamia na maelfu waliishije mbona yamebaki mummies wa wafalme tu? Na hakuna kifaa hata kimoja kilichoonekana maeneo hayo, viliondoleewa au viliyeyukaje? Yaani msumeno utumike kukatia jiwe haupo, halafu mwili wa binadamu (mfalme) aliyeutumia uonekane leo lakini vitendeakazi vyake kama msumeno wake uyeyuke kabisa hata jino lake moja tu hakuna! Ni ajabu sana. Inatupasa kujiuliza sisi je! Tutaacha ustaarabu gani kwa vizazi vijavyo?
Bro fundi wako alishawahi kusahau vifaa site? Wanaopita nao wakavitizama tu?
 
Mmefikia wapi? Binadam ni kakiumbe ka juzi juzi tu 😂😂. Hakijijui kilipo tokea ,kapo ugenini halafu wenyeji hawaonekani patam hapo
 
Tecknologia iliyotumika hapa chanzo chake ni mfalme Solomon ndio aliyotumia kujenga kanisa kubwa sana Kwa usiku mmoja tu.
Infact kulikuwa na elimu ya juu mno ya kumtumikisha jinn ifrit akalijenga hilo dude Kwa usiku mmoja tu,dhambi zimezidi mno hata elimu hizi haziwezi kutumika katika dunia ya leo.

Solomon had demons working for him and under his authority.

The Holy Bible says that demons know God is one:

"You believe that God is one; you do well. Even the demons believe--and shudder!" James 2:19
They even know that Jesus is the Holy Son of God who can destroy them:
 
Huna haja ya kwenda mbali jiulize tu Reli ya kati wakati inajengwa enzi za mjerumani kama kulikuwa na crane au Yale mataluma yalibebwa na waafrika enzi hizo ,sasa hivi kijana jabali kabisa katoka mkoani anatembeza soksi na boksa .Kiufupi binadamu nguvu na akili anayo basi tu.Hakuna kitu kinanikera kama kuona kijana mwenye nguvu zake eti anatembeza karanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ulitaka afanye Nini? Je,hiyo shughuli km ndo inampa riziki??.
 
Huko misri kuna pyramid kubwa ambazo juu zina mawe makubwa kukadiliwa uzito wa tan 4 na zilijengwa enzi za zamani kabla ya kuja mitambo ya kunyanyua vitu vizito (crane).

Hata pale Zanzibar ukipita baadhi ya mitaa utaona magofu ambayo juu kuna majabali ya mawe mazito na inasemekana ni watu wa kale waliyapandisha.

Je; watu Wa zamani waliwezaje kupandisha blocks/mawe mazito urefu wote huo bila kutumia crane? au walitumia ndumba?
View attachment 1019253
Kuna pyramid zingine zipo Sudan . Ila za Egypt ndio maarufu zaidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom