Watu wa Mbeya, badala ya kujichubua na kuwa kama vishetani, kwa nini msitumie mafuta ya kujikinga na jua?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,237
12,751
Tz hii sidhani kama kuna mkoa unaongoza kwa watu kujichubua kama Mbeya. Ukikuta mwanamke aliyejichubua kikweli anatisha. Sura inakuwa kama kokaragosi au kashetani hivi.

Lakini si wakulaumu. Habari ya kujichubua ipo duniani pote. Wazungu walifanikiwa kuteka akili za watu kuwa weupe ndiyo urembo. Nchi kama Korea, India, na nchi nyingine za Asia wanajichubua WaCongo na Watu wa Mbeya cha mtoto. Mafuta ya kujichubua ya Fair and Lovely yalianzia huko India. Jamaa imani yao kuwa kuwa mweupe ni urembo ni kali sana.

Sasa basi, ni nini kinasababisha watu kuwa weusi? Ni kemikali inayoitwa melanin. Hii hutengenezwa na ngozi ili kujikinga na mionzi mikali ya jua. Ni kemikali muhimu sana. Sasa hii hutengenezwa kwa wingi mtu anapochomwa na jua kali.

Sasa tuje huko Mbeya. Watu huwa wana dhana potofu kuwa baridi la Mbeya na mikoa mingine ya nyanda za juu kusini ndiyo husababisha weusi. Si kweli hata kidogo. Weusi ule unasababishwa na jua kali linalowachoma. Sehemu hizi zipo umbali kama wa wastani wa kilomita moja na nusu kutoka usawa wa bahari. Maana yake mtu wa sehemu kama Dar ana layer kubwa zaidi ya hewa inayopunguza nguvu za mionzi na kulinda ngozi yake kuliko yule wa sehemu kama Mbeya au Iringa.

Jambo jingine ni kuwa unyevunyevu(humidity) kwenye hewa kwenye mikoa hii ni mdogo kuliko sehemu kama Dar, Tanga nk. Unyevunyevu husaidia kupunguza ukali wa mionzi.

Utaona kuwa mtu wa nyanda za juu jua linampiga sana kuliko watu wa pwani. Na wengi wakienda pwani utaona ule weusi wao mzito unaanza kupungua.

Sasa basi, kwa vile tatizo ni jua kali(kama kuwa na weusi wa mkaa ni tatizo)basi hata solution iwe kuzuia kupigwa na jua kali. Moja ya njia nzuri ya kufanya hivyo ni kutumia mafuta, lotion na cream zinazosaidia kupunguza madhara ya miale ya jua kwenye ngozi.

Utaona madukani lotions zimeandikwa SPF-yaani sun protection factor- unakuta kuna za SPF-30. Ambayo inazuia zaidi ya 90% percent ya mionzi. Na zingine za juu kama SPF 40, 50 na kuendelea.

Nashauri watu wa Mbeya, Iringa, Njombe nk mnaojichubua na kuwa kama vishetani, mtumie hizi lotion, zitasaidia kwa kiasi kuweka ngozi zenu sawa.
 
Chief, umeniacha kidogo hapo, jua Dar lilivo kali kiasi kile kuliko mbeya then useme mionzi ya jua ukiwa mbeya ni mikali zaid? Baridi na ubichi wote wa mbeya na iringa na njombe afu useme dar kuna hali ya unyevu unyevu kuliko kusini?
dadavua mkuu
 
Chief, umeniacha kidogo hapo, jua dar lilivo kali kiasi kile kuliko mbeya then useme mionzi ya jua ukiwa mbeya ni mikali zaid? Baridi na ubichi wote wa mbeya na iringa na njombe afu useme dar kuna hali ya unyevu unyevu kuliko kusini?
dadavua mkuu
Pwani kuna moisture kubwa, ndio maana hata jasho linatoka jingi,
Iringa unaweza ukakaa week nzima hujatoka jasho lile la kutiririka
 
Kumbe!! Kwahiyo tufanyaje na sie wa Iringa tutoke jasho? Kama sio nzuri kiafya
 
Pwani kuna moisture kubwa, ndio maana hata jasho linatoka jingi,
Iringa unaweza ukakaa week nzima hujatoka jasho lile la kutiririka
Yes yes mkali,.ukitoa chupa ya maji batidi kwenye fridge ukiwa dar na mikoani.

Ya dar, itapata matone mengi kwa juu, ni air ina moisture nyingi..ya mkoani inaweza ikapata vimaji kidg tu..

Upo sahihi, dar humidity ni high
 
Ukipiga mechi usiku, taa zimezimwa, mwanamke mweusi na mweupe 'wanafanana'.
Thread closed...
Ndio maana wengine huwa tunazima taa ili kukwepa mengi.
20230112_044816.jpg

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Tz hii sidhani kama kuna mkoa unaongoza kwa watu kujichubua kama Mbeya. Ukikuta mwanamke aliyejichubua kikweli anatisha. Sura inakuwa kama kokaragosi au kashetani hivi.

Lakini si wakulaumu. Habari ya kujichubua ipo duniani pote. Wazungu walifanikiwa kuteka akili za watu kuwa weupe ndiyo urembo. Nchi kama Korea, India, na nchi nyingine za Asia wanajichubua WaCongo na Watu wa Mbeya cha mtoto. Mafuta ya kujichubua ya Fair and Lovely yalianzia huko India. Jamaa imani yao kuwa kuwa mweupe ni urembo ni kali sana.
Sasa basi, ni nini kinasababisha watu kuwa weusi? Ni kemikali inayoitwa melanin. Hii hutengenezwa na ngozi ili kujikinga na mionzi mikali ya jua. Ni kemikali muhimu sana. Sasa hii hutengenezwa kwa wingi mtu anapochomwa na jua kali.

Sasa tuje huko Mbeya. Watu huwa wana dhana potofu kuwa baridi la Mbeya na mikoa mingine ya nyanda za juu kusini ndiyo husababisha weusi. Si kweli hata kidogo. Weusi ule unasababishwa na jua kali linalowachoma. Sehemu hizi zipo umbali kama wa wastani wa kilomita moja na nusu kutoka usawa wa bahari. Maana yake mtu wa sehemu kama Dar ana layer kubwa zaidi ya hewa inayopunguza nguvu za mionzi na kulinda ngozi yake kuliko yule wa sehemu kama Mbeya au Iringa.

Jambo jingine ni kuwa unyevunyevu(humidity) kwenye hewa kwenye mikoa hii ni mdogo kuliko sehemu kama Dar, Tanga nk. Unyevunyevu husaidia kupunguza ukali wa mionzi.

Utaona kuwa mtu wa nyanda za juu jua linampiga sana kuliko watu wa pwani. Na wengi wakienda pwani utaona ule weusi wao mzito unaanza kupungua.

Sasa basi, kwa vile tatizo ni jua kali(kama kuwa na weusi wa mkaa ni tatizo)basi hata solution iwe kuzuia kupigwa na jua kali. Moja ya njia nzuri ya kufanya hivyo ni kutumia mafuta, lotion na cream zinazosaidia kupunguza madhara ya miale ya jua kwenye ngozi.
Utaona madukani lotions zimeandikwa SPF-yaani sun protection factor- unakuta kuna za SPF-30. Ambayo inazuia zaidi ya 90% percent ya mionzi. Na zingine za juu kama SPF 40, 50 na kuendelea.

Nashauri watu wa Mbeya, Iringa, Njombe nk mnaojichubua na kuwa kama vishetani, mtumie hizi lotion, zitasaidia kwa kiasi kuweka ngozi zenu sawa.
Weka picha ya demo mkuu.
 
Back
Top Bottom